Makosa makubwa tunayofanya wanaume katika mapenzi

STABILIZER

Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
10
Reaction score
13
NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,

Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.

Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).

Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.

Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.

Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.

Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?
 
ah mwana ndege kajileta mwenyewe...hapo nikumwambia bidada sikiliza mie kweli naelewa wataka kunipa tunda ila mie bwana naona nitafaidi zaidi kama utanipa na tigo.
alafu haijalishi kumpa mahitaji yake...unaweza tuma pesa na bado watu wanakugegedea mke wako. hizi story za wanandoa kuishi mbali mbali ni uzushi tuu...hamna ndoa hapo.
 
Acha kusaidia saidia wake za watu bila mpango, shauri yako utaliwa kiboga ndio upate akili.
 
Ni funzo kubwa kwa wanaume, kama wewe sifurahii kitendo alichokifanya huyo mke wa jamaa na kwa maoni yangu hana excuse ya kufanya alichofanya; lakini kweli mumewe alipaswa kuwa responsible kwa familia yake. Why start a family kama huwezi kuiendesha?
Na kitendo cha kutegemea kipato cha mtu mmoja kwa maisha ya sasa sio nzuri kbs.
 
Mke wa mwenzio usimkopeshe pesa.Mke wa mwenzio usimpikie simu.
 
cc kwa wale wwoooooooote wanaotaka wake zao wasisome wala kufanya kazi!
wakae tu kuwategemea ninyi kimapato kazi ndo hapo sasa!
japo sijafurahia pia akili ya huyo dada ila ina sababu nying nyuma yake!
na hakika hili nitusi kwa mumewe!
nikiitafsiri kike,lol!..............ngoja ninyamaze!
 
du, ke wa mtu ni sumu kaka, na mume ni maziwa, ila vitabu vitakatifu vinasema tuikimbie zinaa, hongera tena kuwa mkali kama una msimamo, ila kama ndo hvyo unakuwa mzee wa umate mate kuwa makini.
 
Loh kaka mtambuzi njoo hapa! wakaka wote njoo inawahuuu........
 
wenyewe wanakuja cuz wahusika humu ndani naamini kuwa wapo wengi tuu
 
We nawe una huruma saaanaaa... Nini kujifanya kila leo unamsaidia/mkopesha mke wa mtu hela.. Tena possibily bila hata mumewe kujua / na hata mke wako kujua???

Ona sasa kaanza kujilengesha unamshangaaa! Do u think anakupenda ... Pesa yako tu lolz.

To me sidhani kama ulichokuwa unafanya ni sahihi.. Otherwise kama mkeo na mume wa huyo dada anajua..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
/QUOTE]

Kwa nini akukope wewe badala ya mume wake? Wewe ndo buzi, anataka akuchune zaidi. Yawezekana mwanaume anaacha kila kitu, ila kwa tamaa za huyo mwanamke au kwa kutaka kukuharibia ndoa yako, ndo maana anakuleta mawenge. Wewe jitie kuzoea wake za watu, utashangaa siku yakikukuta aidha kutoka mke wako au mume wa jamaa.
 
Msaada wako umeshaisha hakuna haja kula tunda nje ya ndoa, cha msingi achana nae tena futa mawasiliano nae kabisaa. Kumbuka mla vya watu na vyake huliwa! Sa we nenda kagegede uone..
 
cc kwa wale wwoooooooote wanaotaka wake zao wasisome wala kufanya kazi!
wakae tu kuwategemea ninyi kimapato kazi ndo hapo sasa!
japo sijafurahia pia akili ya huyo dada ila ina sababu nying nyuma yake!
na hakika hili nitusi kwa mumewe!
nikiitafsiri kike,lol!..............ngoja ninyamaze!

hata kwa mke wa mtoa pesa ni tusi? Utatoaje pesa kwa mwanamke bila mkeo au mume wa mwanamke kujua?
 
NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,

Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.

Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).

Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.

Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.

Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.

Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?

Hii umenena vizuri sana Mkuu!!! Hawa akina dada hawatakiwi kuwa exposed kwenye vishawishi!!!! Ni jukumu letu WAUMME/HAWARA/WAPENZI kuwapa mahitaji yao ya muhimu.....Akitoa baada ya hapo sasa huo ni UFUSKA wake. wa kuzaliwa
 
Hilo ndio udhaifu wa wanawake, wanaweza kulipa fadhila kwa mwanamme wa nje kwa msaada aliopewa akasahau kuwa anaibomoa ndoa yake. Na wewe utacheat naye hadi lini? Na wewe huoni kama unataka kuiingiza familia yako kwenye majanga? Why don't let her go? Kata mawasiliano coz mamii wako akijua wema wako utakuwa umekuponz! Better be strong.
 
Kuna mke wa mtu nishamkopa kama 3times hivi, hiyo ya mwisho hajanirudisia!

Sijui na mm ndo anataka nifanyia mchezo huo???
 
ah mwana ndege kajileta mwenyewe...hapo nikumwambia bidada sikiliza mie kweli naelewa wataka kunipa tunda ila mie bwana naona nitafaidi zaidi kama utanipa na tigo.
alafu haijalishi kumpa mahitaji yake...unaweza tuma pesa na bado watu wanakugegedea mke wako. hizi story za wanandoa kuishi mbali mbali ni uzushi tuu...hamna ndoa hapo.

Mhh, kuna watu aisee mnayajua maneno, mweee!!!
 
Ni funzo kubwa kwa wanaume, kama wewe sifurahii kitendo alichokifanya huyo mke wa jamaa na kwa maoni yangu hana excuse ya kufanya alichofanya; lakini kweli mumewe alipaswa kuwa responsible kwa familia yake. Why start a family kama huwezi kuiendesha?
Na kitendo cha kutegemea kipato cha mtu mmoja kwa maisha ya sasa sio nzuri kbs.
ni rahisi kusema hivyo kama haujaoa.unaweza ukaoa huku ukiwa na kipato kizuri then ghafla hela ikakumbia
 
dunia yenyewe haieleweki; uamuzi wako ni bora zaidi kuliko kuchafua hekalu la Mungu na wanawake
 
Back
Top Bottom