Makosa katika upishi

Umenikumbusha demu wangu wakichaga alikuja geto kwangu nikajitutumua nikanunua Sato wa 16k kipindi hicho ili anipikie nilikuta kampika kama alivyo hajamparua magamba na hajamchuna kutoa uchafu (utumbo) tumboni!!

Aiseee basi tu upendo huu nilijifanya kula lakini nikashindwa ikabidi kesho yake ninunue mwingine na nimfundishe kupika.

Kimoyo moyo nilikuwa najisemea huyu ndo nioe huyu?
 
Amini nakuambia, hawa dada zetu wa sasa wa hapa mjini (hususani wasomi, modern girls) kwa sasa, huenda zaidi ya 80% yao hawajui na hawapendi kabisa kupika chochote, sio ugali, wali, pilau, kuunga mboga, hata kupika chai hawajui.
Huyo uliyekutana naye ndio sampuli yao.

Kwa wanaume tunaopenda kupikiwa misosi tukiwa nyumbani, mwanamke wa kuoa kwa sasa ni beki tatu tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…