Makosa ambayo vyuo vingi vya Tanzania wanafanya

Nov 20, 2017
12
45
Wakuu habari zenu, kuna jambo nimeliona kwenye vyuo vyetu vya Tanzania maana kwa hawa walimu wetu, waliotufundisha mavyuoni, nimekuja kugundua kumbe ndio chanzo kikubwa cha wanafunzi wetu kutokuwa na uwezo wa kutokuthubutu hata kuomba kazi nchi za watu, kujiajiri wenyewe hata kama hiyo course unaweza kujiajiri wenyewe ,

wahitimu wengi kutokupata kazi na kusema ajira ngumu, maana unashangaa walimu wote walioajiriwa mavyuoni wana GPA kubwa tu lakini hawana experience ya kufanya kazi kwenye ofisi yeyote kwa kile wanachokifundisha na maanisha kwa mfano kama mwalimu wa statistics awe ameshawahi kufanya kazi kama
mfano statistician, data manager, research officer.

Kama mwalimu wa sheria awe ameshawahi kufanya kwa vitendo kwa kuwatetea watu vizimbani pale.

Kingine ni hawajawahi kupublish research paper sehemu yeyote na wala hawajui wao ni theory tu jinsi walivyofundishwa na walimu wao ambao na wenyewe ambao hawana experience na kazi hata kidogo, walimu wengi ni theory tu practical weupe kuna prof mmoja wa kike alishawahi kunifundisha nikikumbuka saizi nipo ofisini na cheka sana na nilivyoelewa mambo sasa hivi yaani yule prof wa kike hajui chochote kuhusiana na software alikuwa anafundisha econometrics kwenye upande wa kutumia statistical package hakuna anachokijua na hizo software ndio zinazo tumika sana huku makazini watu wanataka matokeo na sio tu theory.

Fanya watu waone.sifa za mwalimu bora wa chuo anatakiwa awe ame fanya kazi sio ya kufundisha tu ya kile atakachoenda kufundisha, awe pia ameandika research paper na imekuwa published na awe anajua kufanya hivyo na sio awe amefanyiwa na mtu na mwisho awe ana GPA kubwa, na sio GPA kubwa tu peke yake.

Unakuta kwenye presentation za research paper za mwisho kwa wanafunzi wengi wanapika data na zinakuwa mtu kakaa ndani tu anaandika au kuandikiwa haendi kukusanya data na hakuna mwalimu anaweza kugundua hilo, watagunduaaje na wakati wenyewe hata hawana uzoefu na hayo mambo, wao wanasoma notes tu mbele hapo tu muda ukiisha wanasepa .

Ndio maana wanafunzi wanatoka vilaza mpaka unashangaa na wakati mitaala iko vizuri, wakienda kuomba kazi wanaambiwa mpaka uwe na experience hapo tafsiri yake ni kwamba huna unachokijua kuhusiana na kazi hiyo kwa vitendo, na wakati wewe tayari umeshafundishwa hayo mambo tayari miaka mitatu, na wakikupima kweli unaonekana hakuna unachokijua kwa vitendo.

Sasa mtu hajawahi kufanya kazi unataka anifundishe kazi hataijulia wapi? wakuu hayo ni baadhi tu niliyoyagundua wakati na soma nalipokuja kufanya kazi, wakuu kwa upande wenu mmeona mapungufu gani kwenye uwezo wa hawa walimu wetu wa vyuoni kwa ujumla?
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,649
2,000
Hiyo ni kwa Vyuo vya uchwara nenda UDSM, walimu wengi wanakiishi wanachofundisha na ofisi zao zipoo...mfano kitivo cha sheria....kituo cha msaada wa kisheria kinaendeshwa na walimu ambao ni mawakili wazuri sana...
 
Mzila nkende

Member
May 16, 2017
51
125
Uzi mzuri sana mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa sana. Lkn shida si wahadhiri wa vyuo vyetu bali shida ni mfumo wa elimu na utekelezaji wake.

Tanzania tunashida sana na namna ambavyo elimu yetu imeplaniwa na utekelezaji wake. Naomba kutoa mifano kadhaa.

Asilimia 60 ya walimu wa sekondari hajui kingereza lkn wanatakiwa wafundishe kwa Kiingereza.

Aslimia 60 ya walimu wa primary walipata division 4 kwenye mtihani wa kidato cha 4.

Asilimia zaidi ya 70 ya wahadhiri wa vyuo hawana mafunzo stahili ya kufundisha

Vyuo vingi vya juu havina miundo mbinu toshelevu kulingana na idadi ya wanafunzi.

Vitabu vingi vinavyotumiwa na wahadhiri vimepitwa na wkati na haviendani na mazingira yetu halisi.

Walimu wa sekondari na primary wengi wao hajisikii kuwa walimu sema ni sababu ya ugumu wa maisha tu.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
24,404
2,000
Aisee mtoa huo ni ukweli mtupu zaidi ya 10000% eti mwl anakufundisha Banking/Finance/Insurance/Accounting wkt hajawahi hata kufanya kazi sehemu husika yeye anachojua ni kusoma kukariri mwanzo mwisho kupata GPA kubwa then kabakishwa kua tutorial hapo chuoni anaendelea mpk anakua na PHD.

Ni mwendo wa theories tu mwanzo mwisho.
 
buzitata

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
1,723
2,000
Halafu wanatoaga mitihani migumu sana hao jamaa

Ukikutana na tcha mwenye uzoefu kazin anafundisha hadi unataman umpe pepsi apooze koo...... Shida inakuja kwa hawa jamaa walioajiliwa kutokana na ukubwa wa gpa zao
 
Nov 20, 2017
12
45
Aisee mtoa huo ni ukweli mtupu zaidi ya 10000% eti mwl anakufundisha Banking/Finance/Insurance/Accounting wkt hajawahi hata kufanya kazi sehemu husika yeye anachojua ni kusoma kukariri mwanzo mwisho kupata GPA kubwa then kabakishwa kua tutorial hapo chuoni anaendelea mpk anakua na PHD.

Ni mwendo wa theories tu mwanzo mwisho.
Well said mkuu
 
ngurumoo

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
583
500
Hiyo ni kwa Vyuo vya uchwara nenda UDSM, walimu wengi wanakiishi wanachofundisha na ofisi zao zipoo...mfano kitivo cha sheria....kituo cha msaada wa kisheria kinaendeshwa na walimu ambao ni mawakili wazuri sana...
Udsm ninaweza dhibitisha pasipo kuacha shaka yeyote, graduate Wa sheria, alishindwa kuandika mkataba Wa mauziano ya kitu,
Mtendaji Serikali za mtaa (Form 4) Anauelewa mzuri kuliko degree holder wa sheria wa Udsm.
Ingekuwa mkataba kwa lugha ya malkia ingekuwa balaaa
 
Swizzy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
774
500
Uzi mzuri sana huu mkuu, umesababisha nimkumbuke lecturer wangu enzi hizo anaitwa Joel yupo chuo cha MUST, alikuwa ananifundisha Quality Control nilikuwa sikosi pindi lake jamaa alikuwa anafundisha huku akitolea mifano ya viwandani na baadhi ya taasisi alizo wahi kufanya kazi. Mda wa kipindi chake ukifika darasa lilikuwa lina jaa wanafunzi tofauti na vipindi vingine.

Vyuo vinapokuwa vina ajiri hawa wakufunzi, viangalie wale wenye uzoefu wa kazi katika kozi husika sio kuangalia GPA tu.
 
mtena

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
2,024

Naona umekachukua kaavator kangu Mkuu ila sio kesi hakuna mwenye hak miliki ya hiyo avator
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,649
2,000
Udsm ninaweza dhibitisha pasipo kuacha shaka yeyote, graduate Wa sheria, alishindwa kuandika mkataba Wa mauziano ya kitu,
Mtendaji Serikali za mtaa (Form 4) Anauelewa mzuri kuliko degree holder wa sheria wa Udsm.
Ingekuwa mkataba kwa lugha ya malkia ingekuwa balaaa
sio lazima kwakua umesoma sheria utajua kila kitu kuhusu sheria, vingi watavijua wakivipractice, so mpe huyo graduate uzoefu alionao uyo sijui mtendaji, utajua kwanini waliosoma certificate na Diploma uwezo wao haukurusu kusomea io degree husika. Hivi mnacheza na Gamba la mlimani, hamko serious kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom