Makosa 10 aliyotenda Mungu

Yote yanajibika kiurahisi sana.
 


Ila bro wewe ni mwepesi sana,kuna mwanachuoni mmoja simtaji kwa kulinda heshima yake anasem "Miongoni mwa misingi ya watu wa mantiki (Ahlul Kalam,al Mantiqiyuun) ni kuongea jambo wasilo kuwa na elimu nalo"

Yaani nyinyi huwa mnaongea mambo pasi na elimu na kufanya hivyo ndio mnaona sawa. Sasa hapa umeongea nini ?

Eti maafa haya yantokana na mifumo ya kumomonyoka. Hiki ni kituko cha karne. Vipi kuhusu mabadiliko ya usiku na mchana,vipi kuhusu mvua ?

Bro umeshawahi kujiuliza kwanini maafa hayatokei hovyo hovyo ?

Halafu kusema kutokuzuia maafa yasitokee sio sababu ya kuthibitisha kutokuwepo kwake. Huo ndio ukamilifu,yeye anaya achia na yeye ndio anaysitisha,hivi hujiulizi kwanini maafa huwa yana muda fulani kisha yanapita ?

Vipi kuhusu Tsunami ? Jaribu kuwa unafikiri kinyume na unavyofikiri,kufanya hivyo bila shaka kutakutoa gizani.
 
Unaelewa kwamba ukishaanza kusema "miongoni mwa misingi ya watu wa mantiki" umeshatumia mantiki tayari?

Unaainisha seti ya misingi ya watu wa mantiki ikoje.

Na ukishaanza kuainisha seti tu, umetumia mantiki.

Kwa hiyo unaitukana mantiki, wakati unatumia mantiki!

Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
 
Logic ni nini?
Nilishakuelezea kitambo nini maana ya mantiki na nikakupa mifano kadha wa kadha,katika mada nyingine.

Kwahiyo sina muda wa kirudi nyuma tena. Leta hoja mpya tuijadilo bro.
 
1)Uwepo wa maovu ni maamuzi ya mtu binafsi ,Mungu kakuumba wewe na kakupa uhuru wa maisha unayoyataka bila kukuendesha kama roboti, na lengo kuu la kukuumba ni kumuabudu yeye.

Zawadi kuu kwa wale wote watakaotii maamrisho yake ni kuwapa pepo ambamo humo ndani watapata kila kitu watakachohitaji, na adhabu aliyowaandalia wale waliomkufuru na kuwatendea maovu binadamu wenzao ni kuwachoma moto.
Mfano hapa duniani kuna masikini wananyanyaswa sana na matajiri lakini hawapati haki zao kila sehemu wanayokwenda kutokana na hongo wanazotoa matajiri ili kuwakandamiza masikini, hivyo basi Mungu anasimama kama hakimu kuhakikisha anatetea wanyonge wote wanaonyanyasika hapa duniani.
 
Unaelewa kwamba ukishaanza kusema "miongoni mwa misingi ya watu wa mantiki" umeshatumia mantiki tayari?
Hahaha,sijatumia mantiki kaka,usitake kulazimisha mambo yaende kama mnavyotaka nyinyi.

Nyinyi mnatakiwa mpaka mlipofika hapa muanze kuwalaumu wanafalsafa wa kale wa magharibi kwa kuwafanya mzidi kuwa wajinga wajinga.
 
2)Wapi Mungu kasema anachagu nani wa kumjua na nani asimjue?

3)Sio kweli kwamba mtoto ataadhibiwa kwa kosa aliotenda mzazi wake ndio maana unaambiwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe na siku ya qiyama kila mmoja ataingia peponi kulingana na amali alizochuma hapa duniani.
 
Haelewi huyu kaka,hawa dawa yao kwenda nao kibishi bishi tu,kama mimi huko nyuma nilikuwa natumia lugha za huruma lugha laini,lakini wao wanajitutumua kijinga jinga,yaani sasa hivi hawa siwapi muda wa kunitoa katika lengo langu.
 
Hahaha,sijatumia mantiki kaka,usitake kulazimisha mambo yaende kama mnavyotaka nyinyi.

Nyinyi mnatakiwa mpaka mlipofika hapa muanze kuwalaumu wanafalsafa wa kale wa magharibi kwa kuwafanya mzidi kuwa wajinga wajinga.

Sio tu umetumia mantiki, bali pia umetumia mantki bila hata kujua kwamba umetumia mantiki.

Unaelewa kwamba ukishaanza kusema "miongoni mwa misingi ya watu wa mantiki" umeshatumia mantiki tayari?

Unaainisha seti ya misingi ya watu wa mantiki ikoje.

Na ukishaanza kuainisha seti tu, umetumia mantiki.

Kwa hiyo unaitukana mantiki, wakati unatumia mantiki!

Baniani mbaya, kiatu chake dawa
 
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani kuwepo kabisa wala hayawezi kujulikana?
 
Unaamini Quran na/ au Bibliakama vitabu vya Mungu?
 
4)Suala la Mungu kuona future ya mtu kama haijatendeka na uhuru wa mtu huyo vinaingiliana vipi?

5)
 

Na usiku huu, anaitaka roho yako.
 
Vitabu vya Mungu ni vinne tu ambavyo ni

1)Taulati
2)Zaburi
3)Injili
4)Quraan.
 
4)Suala la Mungu kuona future ya mtu kama haijatendeka na uhuru wa mtu huyo vinaingiliana vipi?

5)
Mungu anaweza kuona Hance Mtanashati ataua, kabla Hance Mtanashati hajazaliwa, halafu Hance Mtanashati akaepuka kuua?
 
Vitabu vya Mungu ni vinne tu ambavyo ni

1)Taulati
2)Zaburi
3)Injiri
4)Quraan.
Basi hujavisoma hivyo vizuri, ungevisoma vizuri usingeuliza swali ulilouliza.

Kwa nini unaamini hivyo tu na si vingine? Vingine vipi ulivyovisoma?
 
6)Mungu anathibitishika na watu enzi za Musa walimuomba Musa amuombe Mungu aje, Mungu aliwajia ili kutimiza ombi lao.
 
Kaka sikufichi unajua kwamba mimi nina weza kukufundisha elimu ya mantiki kuliko huko ulikoisikia wewe ? Maana wewe unaonekana hata elimu hii hujaisoma bali umeisikia na ukazuzuka na msamiati na maneno ya kivutia tu.

Kaka elimu ya mantiki haina jipya zaidi ya kufikia hitimisho moja kutokana na hoja mbili.

Yaani :

Kama P----->R na Q----->R basi P----->Q

Sasa huo ni ujinga uliopea. Yaani kama nikisema :

Mungu ni mwema,Yesu ni mwema basi Yesu ni Mungu. Sasa hitimisho la kimantiki mara nyingi huwa limegubikwa na ujinga wa hali ya juu. Ndio maana nikasema hivi,msingi mmoja wapo wa mantiki ni kuongea jambo bila elimu.


Yaani hapo huwa hamna muda wa kujadili tofauti ya huyu na yule na mfano wake.


Narudi.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…