Makontena 100 ya bidhaa bandia yakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makontena 100 ya bidhaa bandia yakamatwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BabuK, Feb 27, 2011.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  ZAIDI ya makontena 101, yalikamatwa hadi kufikia mwaka jana yakiwa na bidhaa bandia na bidhaa hizo kuharibiwa huku wahusika wakifikishwa mahakamani.

  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, ameliambia Bunge mjini hapa kuwa kukamatwa kwa bidhaa hizo bandia ni mojawapo ya mikakati inayochukuliwa na
  Serikali katika kukabiliana na uingizaji wa bidhaa bandia.

  Alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoathirika na uingizaji wa bidhaa bandia kutokana na utaalamu unaotumika kumpotosha mlaji juu ya uhalisia wa bidhaa kuwa ni wa hali ya juu hivyo ni vigumu kubaini mara moja udanganyifu huo.

  Alisema ili kukabiliana na uingizaji wa bidhaa bandia nchini, Wizara ya Viwanda na Biashara
  kupitia Tume ya Ushindani imechukua hatua mbalimbali ikiwemo ya kuimarisha idara ya kupambana na bidhaa bandia katika bandari zote nchini na kutoa elimu kwa waagizaji wa bidhaa.

  Nyalandu alisema hatua nyingine ni kushirikiana na wamiliki wa nembo na alama za bidhaa (Brand Owners) ili kupata taarifa za uingizaji wa bidhaa kutoka nje.

  Alisema mkakati mwingine ni kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma juu ya namna ya kutambua bidhaa bandia na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kudhibiti uingizaji wake.

  Naibu Waziri alisema mwenye kumiliki Nembo au Alama ya Bidhaa, ndiye mwenye nafasi kubwa ya kutambua udanganyifu uliofanyika katika bidhaa kuliko mtu mwingine.

  Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Hamis (CUF), aliyeuliza je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza udhibiti wa uingizaji wa bidhaa bandia nchini?  cChanzo: Habarileo
   
 2. c

  comrade mponda Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli serikali haipo serious,hebu tazama kama tungekuwa serious kwenye items za bandari na madini nchi ingekuwa wapi.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,433
  Trophy Points: 280
  Bila shaka nyingi ya mali hizi zitakuwa ni kutoka China.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  BAK nakubaliana na wewe na kuongezea tu ni kwamba wenye mokontena hayo watakuwa ama waligoma kuchangia CCM au hawakufanya jitihada za makusudi za kuchangia "ushindi ni lazima"
   
 5. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sasa hawa wanaokamata wanatakiwa wayarudishe yalikotoka sio kuchoma moto. Ni heri wahusika wakayauzie huko walikoyatoa
   
 6. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ufisadi umezidi kila mtu anajaribu kuchukua chake mapema.....hii hatari sana kwa kweli na inasikitisha sana!
   
 7. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hii nchi yetu hii tunakoelekea siko kabisa nina kila sababu ya kusema imepoteza mwelekeo, wanaohusika na uingizaji wa hizi bandia sio kuwa ni wafanyabiashara pekee bali hata hawa viongozi wetu wa ngazi za juu wanahusika pia, ninao mfano hai wa pale bandarini kuna mizigo ikifika pale huwa hailipiwi ushuru wala kukaguliwa kwa kisingizio kuwa ni mizigo ya mama( 1st Lady) jamaa wakileta ubishi tu wanamvutia waya kuongea na mama moja kwa moja sasa kwa namna hii tusitegemee kama hizi bidhaa bandia zitaisha ikiwa walioko ngazi za juu ndio wahusika wakubwa wa hili jambo
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  sidhani kama huko walikoyatoa yanakubalika.
   
Loading...