unajua tembo likisifiwa sana mgema hulitia maji, huyu jamaa akae apange strategies zake vizuri, lakini akitaka kutafuta sifa sana kazi itamshinda na kujikuta anaharibu kila kitu, mmiliki gani wa mabasi atakubali kusafirisha waalimu bure wakati wanafunzi wanalipa nauli. hao askari tu ni kwa vile wanauwezo wa kutumia mabavu, vinginevyo ingekuwa ngumi kila leo kwenye mabasimakonda ana hoja nzuri tatizo ni namna ya kuitekeleza...
Ni kweli mkuu ila ndio tuombe kasi ya ukusanyaji kodi iendelee kuwa hivi kwa mwaka mzima ndipo mengine yote mtabarikiwaMi sio mchumi hivyo siwezi kujifanya naelewa sana. Ila kwa akili za kawaid bila shule, kama mapata ya serikali yanaongezeka kupitia kodi kama tunavyoelezwa, je haiwezi saidia kuongeza mishahara? Kama unataka uadilifu na ufanisi, je? motisha si utasaidia kwa watumishi wa umma?
Uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu ni wa kimaskini ndio maana unaona wanataka watu wapate huduma bure. Hawa ndio wakikaa ofisini wanajitahidi kuandika proposal za kusaidiwa na wafadhili. Kichekesho kinakuja siku huyo mfadhili anayekuja kukuletea huo msaada yeye anakuja na gari moja tena Rav4, huyo aliyeomba msaada anakuja na msafara wa maVX V8!! Nijuavyo mimi mafuta yameshuka bei sana duniani, ni kwanini asiibane serekali yake kuhakikisha mafuta yanashushwa bei hapa nchini ambapo itapelekea nauli kushuka, sambamba na kuboresha mishahara ya waalimu kila mmoja aweze kujilipia nauli? Ama kama ni mzalendo kweli auze shangingi lake litumike kulipia nauli za walimu na yeye apande daladala aone dhahama ilipo na wakati huohuo apendekeze mishahara ya wakuu wa wilaya ipunguzwe ili kupandisha mishahara ya waalimu, potelea mbali hata kama mapendekezo yake hayatatekelezwa lakini wangalau watu wataona uzalendo wake wa yeye kupakia daladala. Kama sio kusanifu watu na kutafuta sifa za kijinga ni nini. Wewe mkuu wa wilaya tena kijana unaenda kazini na kukata mitaa na shangingi linalokula mafuta kuliko tija yake, halafu ukawaombee watu wasafiri bure kwenye magari ya wafanya biashara na wakati huohuo unataka walipe kodi!!!
Kha! Hivi daladala linamuisha mtu kazini? Na kama linawaisha watu kazini ina maana walimu wamekosa mia 4 ya nauli kwenda shuleni. Nafikiri kuwaambia wasafiri bure ndio watachelewa zaidi kazini Refer Wanafunzi gari moja wataambiwa apande mmoja wengine wasubiri magari mengine. Fikiria ukiwa nje ya Box na sio ndani ya box.makonda ana hoja nzuri tatizo ni namna ya kuitekeleza...
Tuishi madarasani?Kawaida ya Walimu wanatakiwa kuishi kwenye mazingira ya shule, huko wanakoenda kuishi sidhani kama Serikali inawapangia Walimu wakaishi mtaani.
Mawazo ya kijima haya. Hawalipwi mshahara? Hizo daladala zinapewa punguzo wakati wa matengenezo au kununua mafuta? Kwa nini wasipewe kuponi za kusafiria bure ambazo zitalipiwa na serikali?Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
Kwahiyo hata shule uliyosoma hapakuwepo na nyumba za Walimu, ama wewe ni wa juzi juzi?Tuishi madarasani?
Mkuu, kwahiyo tulijulia wapi kusoma na kuandika?Ukisoma mawazo ya watu kwenye hoja hii utagundua wengi ya wanaochangia hawajaenda shule kabisa ndo maana hawajui hata waandike nini na waache nini-WALIMU WANA KAZI PEVU
ushasema wanajeshi na askari,these guys are scary..nani anamuogopa mwalimu mbeba fimbo!kwanza hata kuchapa siku hizi hawaruhusiwi..Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
Anachojaribu Kufanya hapa huyu Paul hamjamuelewa tu.. Mimi naona kuwa hapa huyu jamaa hata kama atashindwa kufikia muafaka wa waalimu kutolipa nauli ila lazima kuna avout flan ambazo waalimu watazipata na zitawapa ahueni...ushasema wanajeshi na askari,these guys are scary..nani anamuogopa mwalimu mbeba fimbo!kwanza hata kuchapa siku hizi hawaruhusiwi..
Ngoja mkuu akazane lakini nadhan kunatakiwa mfumo mzuri wa kodi, ili iwe rahisi kwa serikali kujua nani halipi na nani analipa bila kukwepa.Ni kweli mkuu ila ndio tuombe kasi ya ukusanyaji kodi iendelee kuwa hivi kwa mwaka mzima ndipo mengine yote mtabarikiwa
Angesema kila katikati ya mwezi walimu wapewe fedha ya nauli ata 50,000 ningemwelewa,wengine wanaenda sehemu hakuna daladala wanatumia bodaboda.
Polisi pia wasikamate walimu hovyo wanapokua na viusafiri vyao na Tra wasiwaghasi kwani kodi wanayolipa inatosha.
Tabia za makondakta nichafu Sasa tusiwagonganishe na walimu kisa mia tatu tatu,walimu wasijedhalilishwa kuwa hawana hâta miatatu