Makonda: Wakuu wa mikoa tuliwapinga machinga, Magufuli akawaunga mkono, nasi tumewaunga mkono

Mmachinga amiliki kiwanda....... loading

....error 550 .... try again later or check your software connection.....
.....sorry dear customer, WISHES ARE NOT HORSES, IF THEY WERE HORSES EVEN BEGGERS WOULD RID

Mtu unakosaje msimamo na haya kiasi hiki?
Leo unasimamia hiki, kesho unafanya U - turn baada ya mtukufu kusema halafu unajivunia U - turn yako.
Sasa tuamini msimamo wako wa jana au the revised standard version ya leo?

Na mtukufu akibadilika tena na wewe unabadilika tena, na sisi tukufuate tu?

Haki ya nani njaa ni mbaya na ni busara kuomba afya ya akili kabla ya afya ya mwili.
 
Ninataka mpaka Matonya afundishe chuo kikuu,
ndiyo mzee!

Jamani si ninakubalika?,
ndiyo mzee

Basi endeleeni kunisifu kwa nyimbo na mapambio?

Walimu zawadi zenu nimezificha moyoni
Wanafunzi mtafanyia practical mwezini
nina mpango kila baamedi atamiliki benzi!

Jamani si ninakubalika?
Ndiyo mzee!
 
Hongera mkuu wa mkoa kwa maono mema, kutoka umachinga hadi kumiliki kiwanda na viwa nda!!!!


Tusifie tu jamani mtando usifungiwe!!
 
Ngoja tusubiri viwanda vya wamachinga, safi sana makonda


Hee kumbe nimeweza kusifia
Nenda nchi za Thailand, hongkong, Guangzhou Taiwan, Indonesia, Philippines, na kwingineko Asia utakubaliana na makonda na magufuli. Hizo bidhaa ndogondogo zinazouzwa na wamachinga kama vile midoli, vifaa vya nyumbani (cheap home appliances) electronics zote zinatengenezwa na makundi ya wamachinga na wamepewa nafasi za masoko maeneo ya mijini kati hasa wakati wa usiku. Wana uongozi wao na wanadhibitiana wao kwa wao ktk Mambo Ya kodi, usalama na hata usafi..
Kwa mfano mjini Bangkok Thailand kuanzia saa 12:00asubuhi mama ntilie wote hupanga vyakula vyao mbele ya maduka na ifikapo saa 2:00asubuhi hutamwona hata mmoja na wala kipande cha uchafu. Kuanzia saa 10:00 jioni wenye ulemavu kama vile viziwi na wasioona hupanga bidhaa zao mbele ya maduka yenye bidhaa zisizofanana mfano huweka nguo mbele ya duka la madawa au spea. Muda wa usiku wamachinga humwagika mitaa ya kati na bidhaa zao ambazo hutengenezwa na vikundi vyao.. Basi watalii wanapenda sana magulio haya mitaa ya Silom, Sukhumvit, platinium na kadhalika. Kuna maelefu ya bodaboda na bajaj maarufu Tuktuk zinazoingia mitaa ya kati kutwa nzima. Huwezi kuona accident wala watu kufukuzana na police bali wanatii sheria na wamepewa mamlaka ya kudhibitiana wao kwa wao. Ni heri ushitakiwe kwa polisi kuliko kwenye uongozi wa umoja wao kwa maana ya makundi hayo ya bodaboda, mama ntilie, walemavu, wenye taxi n.k.
Kwa nini sisi tunashindwa? Sera za kuwapitia wanachi hasa vijana hazichukuliwi katika uhalisia wa maisha yetu. Sisi wananchi na wamachinga pia tumepagawa na kujazwa viburi na wanasiasa kwamba watatutetea.tuigeni mifano hii ya wenzetu wa Asia Tuacheni kufukuzana hovyo ila iwepo mipango ya muda mfupi na mrefu katika kuboresha shughuli za makundi ya chini na ya kati katika uchumi ili twende na speed ya magufuli.
 
Makonda ajifunze kwa Polepole kusimamia anachokiamini.

Pole pole kupitia Katiba Mpya aliamini hakuna haja ya kuwa na Wakuu wa Wilaya akasimamia anachokiamini akawa Mkuu wa Wilaya ya Musoma na baadae Ubungo!
 
Makonda ajifunze kwa Polepole kusimamia anachokiamini.
Pole Pole anasimamia nini mkuu...Note:Vyeo vya ukuu wa Wilaya na Mkoa havina maana ni mizigo kwa wananchi nani kiteuliwa siwezi kukubali...eti nani alitamka hivyo
 
Back
Top Bottom