Makonda: Wakuu wa mikoa tuliwapinga machinga, Magufuli akawaunga mkono, nasi tumewaunga mkono

Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda akiwahutubia machinga Kariakoo amesema ana mpango wa kuwabadilisha kuwa watu wanaomiliki viwanda vidogo badala ya kutembeza bidhaa barabarani kwa kuunda uongozi wa kuwasimamia.

Amesema wakuu wa mikoa walikuwa wakiwapinga machinga ila Rais Magufuli amewaunga mkono na hana jinsi nyingine zaidi ya kuwaunga mkono ila atawabadilisha kuwa wakubwa zaidi ili waachaane na kutembeza bidhaa.


Kauli tamuuuuuu lakini yenye uongo mkubwa na uliotumika. HIVI MACHINGA ANAWEZA KUWA MTEMBEZA BIDHAA NA GHAFLA AKAMILIKI BIASHARA INAYOTOKANA NA KIWANDA CHAKE?
 
Hivi huyu kijana ni ndoto ipi aliwahi kutimiza?
1. Walimu kusafiri bure kwenye daladala / kupewa vitambulisho ...
2. Ombaomba kuondolewa jijini Dar ...
3. Shisha vipi?
.. sasa hili la kuwasaidia wamachinga kumiliki viwanda ...
Mkuu mimi simuhesabii maana tayr keshashindwa
 
siasa za uchaguzi uliokwisha pita zitatutafuna kwa muda mrefu kama hatutakua na busara za kusameheana
Busara imekuwa bidhaa adimu sana Tanzania ya Leo, namuangalia bwana yule Lipumbavu alivyokosa busara Na elimu zote alizonazo sina hamu.
 
Lakini mi wazo langu binafsi hata hizo bidhaa zingine wanazozitembeza zimetokana na viwanda vidogo kwa hiyo katika kuzipatia masoko ndio wakaibuka hawa watu ili kujipatia riziki, sasa ukisema unawabadilisha ili wawe wanamiliki hivyo viwanda inabidi hawa watu waingie darasani kwanza pia nao wakifuzu bidhaa zao nani atawauzia?
 
Mimi ni mmoja wa watu ninayemkubali rais lakini kwa Hili la wamachinga simuungi mkopo kwani anaziua sheria zinazotungwa na halmashauri zetu pili watanzania kwa asilimia kubwa tunaishi kwa kuvunja sheria na sio kwa kuheshimu sheria sasa wamachinga wamepewa jeuri na ndugu rais wanapanga bidhaa zao ovyo tu Barabarani na milangoni mwa Maduka ya watu mwisho watasema hata sebuleni ni haki yao kufanya biashara nakuomba rais tazama upya maelekezo yako kwa watendaji kwa kweli umemkatisha tamaa mongela kule mwanza kwa ushauri tu waache watendaji kazi hao wakusaidie tena wanafanyakazi vizuri wananchi wanatakiwa kufuata sheria ndipo tunaenda vizuri pili watu watafuata bidhaa na sio bidhaa zinafuata watu mongera mwanza alifanyakazi nzuri Kule nyegezi yaliandaliwa mazingila mazuri tu ya kufanyia biashara na sio mongera kuwa alikurupuka tu nawasihi watanzania tusiishi kwa mazoea
 
Back
Top Bottom