Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,334
- 72,798
Sheria inawalinda sana watoto chini ya umri wa miaka 18 na ni kosa la jinai kumtumia mtoto kueleza madhila aliyokutana nayo hasa ya kingono hadharani bila kumsitiri sura yake.
Kwa sababu ulizoziona wewe zinafaa leo kwenye mkutano wako wa madawa ya kulevya umewasimamisha watoto wadogo mbele ya kamera za television bila hata kufunika sura zao na kuwapa nafasi wazungumze yaliyowakuta ambayo ni machungu sana mbele za watu.
Pamoja na kuwa tunahitaji kujua madhila wayapatayo watoto kutokana na madawa ya kulevya lakini sisi kama watu wazima lazima tuheshimu utu wao na kuwasitiri na hali hiyo na sio kuwatangaza kwa uwazi namna ile.
Hata hivyo vituo vya TV naona nao wamekosa weledi kwa kuendelea kurusha matangazo yao pale watoto walipokuwa wakijieleza.
Unapaswa kuonywa usirudie tena jambo hilo kwani Taasisi zinazohusiana na haki za watoto wanaweza kukushukia na wewe ukadhani watu hao wanapinga vita dhidi ya madawa kumbe sivyo