Makonda: Ujenzi wa Dar es Salaam ya viwanda umeanza rasmi

Wasi wasi wangu ni kama sheria ya mazingira aka EMA 2004 imezingatiwa katika kuanzisha eneo la viwanda.

Wanaweza simika viwanda kwenye chanzo cha maji chini ya ardhi hasa visima vya kimbiji ikawa ni ama tuendelee na viwanda ama vibomolewe maana maji yatachafuka.
 
Wasi wasi wangu ni kama sheria ya mazingira aka EMA 2004 imezingatiwa katika kuanzisha eneo la viwanda.

Wanaweza simika viwanda kwenye chanzo cha maji chini ya ardhi hasa visima vya kimbiji ikawa ni ama tuendelee na viwanda ama vibomolewe maana maji yatachafuka.
Unafikili ni nyumbu kama wewe
 
Square meter 2,000 kwa eneo la kiwanda!!!!! hata kama ni kiwanda kidogo inamana 40m x 50m??!!!! watu wa mipango miji mngemshauri mkuu ana wazo zuri ila sio kwa size hiyo ya eneo. Kidogo mno kwa shughuli za viwanda. Tatizo la mkuu naye mipango yake haikamiliki kutokana na kukosa msingi imara, siasa zimezidi sana,
 
Una issue mbili za kushugulika nazo kwa sasa..
-Kashfa ya kutumia jina ambalo sio lako.
Wewe unaitwa Daudi Bashite.. Eleza jina la Paul Makonda umelitoa wapi. Clear yourself kwenye hii kashfa mbaya ya kununua vyeti baada ya kupata div zero form 4.

-Kuitikia wito wa Mahakama.
Ulivyokuwa unataja majina ya wauza unga ulitaka watuhumiwa wote watii wito wako kwa kwenda central police. Na wewe sasa TII wito halali wa Mahakama kwa kwenda Mahakamani kwenye kesi aliyokufungulia Mh Mbowe.

Mambo ya viwanda ni usanii mwingine unaleta..!!
Viwanda bila Mtaji umewahi kuona wapi??
Acha MZAHA.
Fanya hayo niliokueleza.
 
Kutokana na wachangiaji umu jf kila atakachofanya mhe.mkuu wa mkoa lazima kitapingwa tu,mnapenda afanye ni sasa?
 
*RC MAKONDA: UJENZI WA DAR ES SALAAM YA VIWANDA UMEANZA RASMI*

Ama kwa hakika kila mmoja wetu anaifahamu dira na dhamira ya serikali ya awamu ya *tano ya Dr. John Pombe Magufuli ya kuifuta historia yetu ya aibu ya muda mrefu ya kuwa na taifa la wachuuzi kwa kuligeuza kuwa taifa la wazalishaji kupitia kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya kutosha chini ya mwamvuli wa sera ya Tanzania ya viwanda.*

Ni kwasababu hiyo tu, sisi watendaji wake aliotuamini na kutupatia dhamana, hatuna budi kuendelea kuwaza zaidi, kutenda zaidi na kushirikisha washirika wengi zaidi ili kwa pamoja tuikamilishe ndoto hii ya Rais wetu mpendwa.

Kuelekea kutimiza azma hii *tayari ninapozungumza nimekamilisha maongezi na mshirika wetu wa maendeleo Azimio Housing Estate kampuni ambayo imekubali kutupatia eneo lililopo Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 1500 la thamani ya zaidi ya bilioni 121 na milioni 470 litakalotumika kama eneo maalumu nitakaloligawa kwa wajasiriamali zaidi ya 3,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vya idadi hiyohiyo.* Pamoja na mambo mengineyo mpango huu *unakusudia kuwasaidia wamiliki wa viwanda vidogo kupata maeneo yao ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia gharama za kukodi maeneo, kuwaepusha na usumbufu wa kukaa maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwapatia uhakika wa kuwa na anuani (address) za kudumu.*

Kimsingi chini ya utaratibu huu *kila mmiliki wa kiwanda kidogo tutampatia Sqm 2,000 hivyo eneo hilo litabeba viwanda vidogo zaidi ya 3,000 ambavyo vitatengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 15,000 zitakazoambatana na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 43,000.*

Kwa namna ya kipekee niendelee kuwashukuru Azimio Housing Estate ambao *wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambayo Mpaka sasa imedhihirisha ni kwa kiasi gani uongozi wake unafanya kila jambo kwa kuzingatia maslahi mapana ya wananchi wake.*

Na mfano wa hili ni mdogo tu, badala ya kuhangaika kuomba ekari zote 1500 kwa ajili ya wamiliki hawa wa viwanda vidogo wanaopambana kubadili historia za vipato vyao usiku na Mchana ningeweza kujiombea hata ekari 10 tu kwa ajili yangu na mke wangu nikatulia.

Itoshe tu kusema kwamba, *maamuzi ya kutanguliza maslahi ya wananchi ndio yameufanya mkoa wangu Mpaka sasa kuendelea kutekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 160 ambazo nimezipata kwa wadau wa maendeleo waliotuchangia na kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo inayojumuisha ujenzi wa wodi tatu kubwa na za kisasa zenye ghorofa tatu tatu, theatre kubwa za upasuaji, hospitali kubwa ya Chanika ya zaidi ya bilioni 8 za kitanzania, Makao Makuu ya kisasa ya Bakwata ambayo yapo katika hatua za mwisho, madarasa, barabara, mahakama 20 za mwanzo na Vituo 20 vya polisi.*

Na kwa ushahidi wa haya machache niliyoyataja ibaki tu kuwa ushahidi ya kwamba, *utajiri wa Makonda ni wa watu kwa Maendeleo ya watu kwani Dar es Salaam tuitakayo ipo mikononi mwa wanadar es salaam wenyewe*.

Ameshaenda kuitika wito??Au viwanda vya kukimbizana na akina Mbowe
 
Kutokana na wachangiaji umu jf kila atakachofanya mhe.mkuu wa mkoa lazima kitapingwa tu,mnapenda afanye ni sasa?

Aitii WITO wa mahakama haya mengine hayamuhusu.Toka lini mnunua vyeti anakuwa hata na akili ya kufikiria mbali zaidi ya pua yake
 
Naona utakatishaji wa Viwanja umeanza baada ya Lukuvi kutangaza kuny'ang'anya Viwanja watu walio jimilikisha maviwanja mengi bila kuyauza Na kuviendeleza.

Ila natamani sana mkuu wangu wa mkoa Siku moja alete report ya utekelezaji wa matamko Yake yote ambayo ameyafanya mpaka sasa kuanzia walimu kupanda bure daladala, upandaji wa miti, kupita nyumba Za wageni wakati wa kazi kukamata watu etc.
 
Naona utakatishaji wa Viwanja umeanza baada ya Lukuvi kutangaza kuny'ang'anya Viwanja watu walio jimilikisha maviwanja mengi bila kuyauza Na kuviendeleza.

Ila natamani sana mkuu wangu wa mkoa Siku moja alete report ya utekelezaji wa matamko Yake yote ambayo ameyafanya mpaka sasa kuanzia walimu kupanda bure daladala, upandaji wa miti, kupita nyumba Za wageni wakati wa kazi kukamata watu etc.

Atii wito wa Mahakama kwanza,mengine ni movie za isidingo tu
 
Back
Top Bottom