Makonda: Ujenzi wa Dar es Salaam ya viwanda umeanza rasmi

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
388
271
*RC MAKONDA: UJENZI WA DAR ES SALAAM YA VIWANDA UMEANZA RASMI*

Ama kwa hakika kila mmoja wetu anaifahamu dira na dhamira ya serikali ya awamu ya *tano ya Dr. John Pombe Magufuli ya kuifuta historia yetu ya aibu ya muda mrefu ya kuwa na taifa la wachuuzi kwa kuligeuza kuwa taifa la wazalishaji kupitia kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya kutosha chini ya mwamvuli wa sera ya Tanzania ya viwanda.*

Ni kwasababu hiyo tu, sisi watendaji wake aliotuamini na kutupatia dhamana, hatuna budi kuendelea kuwaza zaidi, kutenda zaidi na kushirikisha washirika wengi zaidi ili kwa pamoja tuikamilishe ndoto hii ya Rais wetu mpendwa.

Kuelekea kutimiza azma hii *tayari ninapozungumza nimekamilisha maongezi na mshirika wetu wa maendeleo Azimio Housing Estate kampuni ambayo imekubali kutupatia eneo lililopo Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 1500 la thamani ya zaidi ya bilioni 121 na milioni 470 litakalotumika kama eneo maalumu nitakaloligawa kwa wajasiriamali zaidi ya 3,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vya idadi hiyohiyo.* Pamoja na mambo mengineyo mpango huu *unakusudia kuwasaidia wamiliki wa viwanda vidogo kupata maeneo yao ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia gharama za kukodi maeneo, kuwaepusha na usumbufu wa kukaa maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwapatia uhakika wa kuwa na anuani (address) za kudumu.*

Kimsingi chini ya utaratibu huu *kila mmiliki wa kiwanda kidogo tutampatia Sqm 2,000 hivyo eneo hilo litabeba viwanda vidogo zaidi ya 3,000 ambavyo vitatengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 15,000 zitakazoambatana na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 43,000.*

Kwa namna ya kipekee niendelee kuwashukuru Azimio Housing Estate ambao *wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambayo Mpaka sasa imedhihirisha ni kwa kiasi gani uongozi wake unafanya kila jambo kwa kuzingatia maslahi mapana ya wananchi wake.*

Na mfano wa hili ni mdogo tu, badala ya kuhangaika kuomba ekari zote 1500 kwa ajili ya wamiliki hawa wa viwanda vidogo wanaopambana kubadili historia za vipato vyao usiku na Mchana ningeweza kujiombea hata ekari 10 tu kwa ajili yangu na mke wangu nikatulia.

Itoshe tu kusema kwamba, *maamuzi ya kutanguliza maslahi ya wananchi ndio yameufanya mkoa wangu Mpaka sasa kuendelea kutekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 160 ambazo nimezipata kwa wadau wa maendeleo waliotuchangia na kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo inayojumuisha ujenzi wa wodi tatu kubwa na za kisasa zenye ghorofa tatu tatu, theatre kubwa za upasuaji, hospitali kubwa ya Chanika ya zaidi ya bilioni 8 za kitanzania, Makao Makuu ya kisasa ya Bakwata ambayo yapo katika hatua za mwisho, madarasa, barabara, mahakama 20 za mwanzo na Vituo 20 vya polisi.*

Na kwa ushahidi wa haya machache niliyoyataja ibaki tu kuwa ushahidi ya kwamba, *utajiri wa Makonda ni wa watu kwa Maendeleo ya watu kwani Dar es Salaam tuitakayo ipo mikononi mwa wanadar es salaam wenyewe*.
 
Kama ni viwonder sawa... Makonda msalimie Kandoro hata yeye alipita hapo ofisini.

mwambie akamuulize vipi mitaji maana mabenk hatuwez chukuwa pesa ambazo zinaenda kukomolewa kudai eti kodi pesa zinyewe za mikopo mnatuambia sheria lazima ulipe sasa nalipaje pesa yenyewe nimekopa hahahah kuna vituko asee
 
wazee watu wanafunga biashara wengine hawataki kuingiza mitaji kwenye biashara interest za mabenk ziko juu hivi viwanda kuna mazingira gani rafik kwa mtanzania kukianzisha ?
 
Idea ya viwanda ni nzuri lakini serikali ishughulike kwanza na namna ya kuokoa biashara nyingi ambazo zinafungwa na kupoteza ajira za watu

hapo ujue hawana mpango na mtu yeyote benk unamkopo wenye interest kubwa tu huku bado mambo hayaendi wateja hakuna bado kodi kama utitiri

kama sio ngonjera ni nini ?
 
Nakumbuka sana utotoni, nilipokuwa nimefanya kosa na kujua kuna adhabu inanisubiri amani ilikuwa inanitoweka kabisa. Sipati amani nikawa kama navyokuwa siku nyingine, mara nyingine nilibeba kwanja nikafyeka uwanja wote na kupanga mawe mstari kufuata ukuta, nikitaraji baba ataiona kazi yangu zaidi ya makosa yangu.

Baba naye alikuwa si mtu wa sport sport, atanipongeza kwa kufyeka uwanja lkn mikwaju iko pale pale.
 
watu bhan wamepewa eneo wanataka wapewe na mitaji
wakipewa mitaji watasema wapewe na vifaa vya kujengea hayo maeneo wakipewa watasema mbali tunataka usafili yani mweusi ni mweusi tu
 
Back
Top Bottom