Makonda: Suala la Pauline Gekul, CCM ina taratibu na kanuni zake kuanzia Ngazi ya Tawi, hivyo kama likifika Taifani tutalitolea taarifa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,140
Mwenezi wa CCM Komredi Makonda amesema kuhusiana na swala la mbunge wa Babati mh Gekul, CCM ni Chama kikubwa na kina taratibu makini

Kuna Vikao Vya nidhamu na Maadili kuanzia Tawini na kuendelea hivyo kama kuna lolote litathibitika Vikao husika vitachukua hatua stahiki na kama litafika Ngazi ya taifa tutalitolea Taarifa

Source: Ayo TV
 
Kutuhumiwa sio kosa, kosa nikukutwa na hatia.
Kama ikibainika anakosa then sheria itachukuwa mkondowake atapata adhabu sawasawa na makosayake.

Hayo mambo ya kichama sionikama kunakitu watakacho mfanya.
 
Imeisha hiyo hakuna kitu kitaendelea tena
Makonda hana mamlaka ya kufanya chochote hata Katibu kata tu hawezi kumfanya chochote, hizo kelele zake ni kupayuka tu, NEC na CC ndio vyombo vya maamuzi kwenye chama.

Mtu mwenye mamlaka kwenye chama ni Chongolo ndio alipaswa kuulizwa na siyo huyo mpiga domo, tatizo waandishi wa Tanzania ni bure kabisa.

Ni sawa na mtu kudhani Ahmed Ally ana mamlaka ya kufanya chochote Simba wakati waamuzi ni kina Mangungu na Try again na CEO.
 
Mwenezi wa CCM Komredi Makonda amesema kuhusiana na swala la mbunge wa Babati mh Gekul, CCM ni Chama kikubwa na kina taratibu makini

Kuna Vikao Vya nidhamu na Maadili kuanzia Tawini na kuendelea hivyo kama kuna lolote litathibitika Vikao husika vitachukua hatua stahiki na kama litafika Ngazi ya taifa tutalitolea Taarifa

Source: Ayo TV
Makonda mwenye anatakiwa kuchukuliwa hatua.
 
Back
Top Bottom