Makonda kumbuka kuna kesho

Makonda kumbuka kuna kesho

Nyie vichaa kweli kila jambo anakosea. Hadi kuachia hio kazi mamlaka ya kupambana chini ya kamishna mpya nako amekosea.. Hivi hizi chuki juu ya kijana Mwenzenu mmezitolea wapi?? Makonda makonda tu kila thread makonda..
Kwako huyu bosi wako hajawahi kukosea hata siku moja, ni mungu yeye. Alipotaja watu bila kufuata taratibu ulimuunga mkono, wenzio wamemkosoa amekabidhi majina mamlaka husika, unamuunga mkono. Wewe ni bingwa wa kujipendekeza. Inawezekana wewe ndo KONDAKTA mwenyewe.
 
Sasa MAISHA nayoishi KIKWETE leo baada ya kustaafu yanafanan na wewe??....Hahta hiyo KESHO ya MAKONDA itaendelea kuwa VIZURI tu.....MSIHISHI KWA KUMEZESHWA MANENO NA HAO WANASIASA ndimi mbili.....
Mfano kina LISSU NA MBOWE walipokuwa wanamtukana LOWASSA wao walijua LEO hii watakuja kumlamba MIGUU????....na je MAISHA ya LISSU na MBOWE kipindi wana mtukana LOWASSA na LEO yanatofauti gani????....FANYA YAKO KIJANA.....tATZO HAPA KUBWA NI KUHUSISHWA KWA mbowe KWENYE HILI....ndio maana kelele kila kukicha...
Brother umekurupuka kujibu hoja bila kuusoma na kuelewa concepts yake. Tulieni mshindane kwa hoja. Hii post inatoa tu Ushauri and nothing else. Kama humu huwezi kuvumilia nenda fb kalike picha za wale wenzako. Humu ni hoja kwa hoja.
 
Yaani huyu jamaa sasa amepitiliza........

Eti ana mamlaka ya kumfukuza Raia yeyote asiyemtaka ndani ya Mkoa 'wake' wa Dar!
He......[emoji15] [emoji15] [emoji15]
Apia......!!??
 
Kama hilijambo la madawa yakulevya linaukweli basi ninashauli serikali isimuonee mtu yoyote huluma awe mwanasiasa au mchungaji au shehe au padili..sheriya ifate mkondo wake..lkn watoto waviongozi wengi tu wanausika kwenye hilijambo kwahiyo ninaiomba serikari ifanye hakhi bila upendeleo
 
Me mbona naona makonda anafanya vyema bhn hv nyie hua hamsikitiki kweli vijana wanavyopotea kene madawa ya kulevya
 
Yaani huyu jamaa sasa amepitiliza........

Eti ana mamlaka ya kumfukuza Raia yeyote asiyemtaka ndani ya Mkoa 'wake' wa Dar!
RAIA yeyote asiyemtaka ndani..

..mliozaliwa Ocean road,Muhimbili,Mwananyamala hili linawahusu zaidi..!
na nyie Wazaramo pia.

Na wamikoani wasiotakiwa wanahamishiwa daslama.
 
Kwako huyu bosi wako hajawahi kukosea hata siku moja, ni mungu yeye. Alipotaja watu bila kufuata taratibu ulimuunga mkono, wenzio wamemkosoa amekabidhi majina mamlaka husika, unamuunga mkono. Wewe ni bingwa wa kujipendekeza. Inawezekana wewe ndo KONDAKTA mwenyewe.
Tuko vitani. Rais Kwa nguvu zote anatusapoti, watanzania tunaojua madhara ya unga tunasapoti. Viongozi wa dini wanasapoti.. Mmebaki watumiaji wachache Sana.. Nakusihi Kwa hili wekA pembeni itikadi zako Tumuunge mkono ofisi ya makonda
 
Sasa MAISHA nayoishi KIKWETE leo baada ya kustaafu yanafanan na wewe??....Hahta hiyo KESHO ya MAKONDA itaendelea kuwa VIZURI tu.....MSIHISHI KWA KUMEZESHWA MANENO NA HAO WANASIASA ndimi mbili.....
Mfano kina LISSU NA MBOWE walipokuwa wanamtukana LOWASSA wao walijua LEO hii watakuja kumlamba MIGUU????....na je MAISHA ya LISSU na MBOWE kipindi wana mtukana LOWASSA na LEO yanatofauti gani????....FANYA YAKO KIJANA.....tATZO HAPA KUBWA NI KUHUSISHWA KWA mbowe KWENYE HILI....ndio maana kelele kila kukicha...
Wewe na Aggnes mume wenu mmoja kumbuka ditopile mzuzuri alivyofanya alivholipwa na Mungu
 
Tuko vitani. Rais Kwa nguvu zote anatusapoti, watanzania tunaojua madhara ya unga tunasapoti. Viongozi wa dini wanasapoti.. Mmebaki watumiaji wachache Sana.. Nakusihi Kwa hili wekA pembeni itikadi zako Tumuunge mkono ofisi ya makonda
Tutamuunga mkono yeyote anayepigana vita ya dawa za kulevya kwa kuzingatia sheria, tunaojitambua hatuwezi kuunga mkono mtu anayekamata watu kwanza, halafu anawapa tuhuma, kisha anaamuru uchunguzi, huu utaratibu wa wapi? Muungeni mkono nyie vibaraka wake na mtashindwa hata kabla ya wiki kuisha.
 
Wanao mpinga makonda inaonekana wote watumiaji na makontena kwa nn jambo kama hili tusimuunge mkono au unaona raha unavyowakuta vijana balabalan wakisinzia huku wamesimama plz tuunge mkono swala hili tuache siasi
 
amesikia. elekeza nguvu zako kujadili mambo mengine ya muhimu katika nchi yako na sio kumjadili makonda. wewe umeifanyia nini tanzania katika mapambano ya dawa za kulevya???
Kwanini Makonda asijadiliwe wakati ni kiongozi anayelipwa kwa kodi zetu, rais mwenyewe tunamjadili sembuse huyu.
 
"MAKONDA ACHA KUJIPA MAMLAKA NA WAJIBU USIOKUWA WAKO, WEWE NI MKUU WA MKOA SIYO MUNGU WA DSM."


".., Ninao uwezo wa kumfukuza mtu yoyote ndani ya mkoa wangu kwa masaa ninayotaka mimi na asiondoke na chochote zaidi Ya ndala alizovaa." - Paul Makonda, RC, Dar-es-salaam


#My_Take
.., Makonda amesema kuna watu hawajasoma sheria na wanapoga kelele tu kumkosoa yeye.., [inawezekana] ikawa ni kweli kabisa.., lakini katika kundi hilo, pia na yeye asithubutu kujiondoa, ni hali-jojo kwenye katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania..,

.., huo uwezo ambao Makonda anathubutu kuzungumzia ni upi!? Ameutoa wapi? Hata sheria ambazo zinampa mwongozo wa utendaji kazi kama mkuu wa mkoa hazimpi nafasi hiyo.., anaamua kumfukuza mtu katika misingi ipi.., anapaswa kuainisha sababu, siyo kuweka neno "mtu yoyote, wakati wowote".., amelewa madaraka huyu mtu..

Tuitazame katiba ya Tanzania; ukisoma SEHEMU YA TATU, HAKI NA WAJIBU MUHIMU, Haki ya Usawa Ibara ya 12 na 13 imeeleza vyema sana kwa kuzingatia [Usawa wa binadamu, Sheria ya 1984, Na.15 ib.6 NA Usawa mbele ya Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 NA Sheria ya Na.4 ya 1992 ib.8 Sheria ya 2000 Na.3 ib.5] ambazo zote kwa pamoja zinatoa ufafanuzi mzuri kama ifuatavyo [kwenye katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania]

Sehemu hiyo ya tatu, HAKI NA WAJIBU MUHIMU, Haki ya kuishi, imetolewa ufafanuzi vyema sana katika ibara ya 14,15,16,17 za katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kutoka katika sheria za [Haki ya kuwa hai Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 NA Haki ya Uhuru wa mtu binafsi Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 NA Haki ya faragha na usalama wa mtu Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 NA Uhuru wa mtu kwenda atakako Sheria ya 1984 Na.15 ib.6]

MAKONDA anaendeshwa na mihemko.., ni wazi hata katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania aidha haijasoma au ameisoma na hakuwahi kuielewa.., Ibara ya 17(1)(2) inaeleza wazi sana, tuitazame;

17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya -
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na kumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda anakotaka ili
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi fulani mahususi au maslahi ya sehemu fulani ya umma, kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii.

..., sheria zote hizo, zimetoa ufafanuzi vyema sana za namna mtanzania alivyo na haki ya kuishi sehemu yoyote kwa wakati wowote, kwa amani na utulivu bila kupata bugudha endapo tu, hajavunja sheria za nchi yetu.., sasa Makonda alipaswa kusema watu wa aina gani ambao wanaweza kufukuzwa wakati na muda wowote wakaondoka katika "mkoa wake" bila ndala..,

Kwanza nani alisema Dar es Salaam ni mali ya a mtu, tena mtu mmoja.. Dar es Salaam ni mkoa wenye wakazi zaidi ya milioni 4.., kuwa kiongozi [wa kuteuliwa] siyo tiketi ya kujimilikisha ardhi na mali zote za DSM na kusema "mkoa wangu".., DSM ni mali ya watanzania, kila ilivyo kwa maeneo yote ya ndani ya Mipaka ya Tanzania.., tuache hii tabia ya kujimilikisha maeneo ya utawala kama Mali yetu binafsi katika utumishi wa umma!

Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuagiza kukamatwa kwa mtu na kuwekwa rumande yako chini ya vifungu vya 7 (mamlaka ya mkuu wa mkoa) na 15 (mamlaka ya mkuu wa wilaya) vya Sheria ya Tawala za Mikoa, 1997. Vifungu hivyo vinafanana katika uandishi na hata mantiki isipokuwa tu maneno 'Mkuu wa Mkoa' na 'Mkuu wa Wilaya'., na hakuna mamlaka hayo ambayo Makonda anataka kwa lazima kujibebesha kwa lazima..,

Majukumu ya Sekretarieti ya Mkoa ambacho ni chombo cha utendaji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa [katika mikoa yote] katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania yanatamkwa bayana katika sheria ya Tawala za Mikoa Na. 19 ya mwaka 1997.., na hakuna sehemu mkuu wa mkoa ametakiwa na sheria kutekeleza wajibu wake kwa kuelezwa kwamba anaweza kumfukuza "mtu yoyote na wakati wowote katika mkoa wake na akaondoka bila kitu chochote isipokuwa ndala zake"..., haipo, na kama ipo, naomba kuoneshwa!
 
Wanao mpinga makonda inaonekana wote watumiaji na makontena kwa nn jambo kama hili tusimuunge mkono au unaona raha unavyowakuta vijana balabalan wakisinzia huku wamesimama plz tuunge mkono swala hili tuache siasi
Approach mkuu ndiyo tatizo, wenye akili wamemnyang'anya kisemeo kiaina.
 
Hapana kiumbe yeyote akishakaa kwenye kiti cha enzi hakuna wakumtoa hapo hadi mwisho wa dahali.... Kumbuka akisimama yeye mungu huyu hapa pembeni yake
 
"Rais kikwete Leo ni mstaafu"

cheo ni dhamana,basi sikiliza ushauri, unaonekana una dhubutu lakin siku zote approach zako unazikosea sana.

jifunze kutoka mawazo ya wengine sio kila ushauri ni tusi.

kabla ya kufanya Jambo kubwa tafuta wanasheria nguli wakushauri kabla ya kulifanya.
Kesho atakuwa kama Ck
 
Back
Top Bottom