Makonda hatalipiza kisasi lakini waliomnyima Ubunge anawajua!

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Makonda kasema hatakwenda kulipa kisasi lakini mmmh!! Moyo sio kama mashine ya kusaga na kukoboa nafaka, unaongozwa na ukweli na uhalisia; na ukweli na uhalisia vinaongozwa na matukio yenye kusababisha furaha au huzuni kwa mtu.

Binadamu ana tabia ya kulipa furaha na huzuni/maumivu aliyosababishiwa kwakuwa binadamu kulipa hisani na kisasi ndiyo uhalisia wenyewe wa binadamu, kinyume chake ni uzezeta, ujinga, uzembe, woga, na kujitafutia ukosefu wa afya ya mwili na akili.

Maana huwezi kuukata mkono unaokulisha na huwezi kumpenda aliyekusuma na kuangukia kwenye kundi la siafu; ndio uhalisia. Ndiyo maana vitabu vya dini vinatuambia kulipizaa kisasi ni haki. Ni haki kwakuwa moyo ndivyo unavyotaka na ulivyoumbwa ili uwe na afya yake iliyokusudiwa. Lazima uteme mate kama kinga ya kukutana na harufu mbaya.

Makonda anawafahamu wote waliomuengua kwenye kinyang'anyilo cha kuwania nafasi ya kuwa Mgombea Ubunge kule Kigamboni, hata kama atajifanya kutaka kuwasamehe lakini moyo wake utamsukuma sana. Atatumia nguvu nyingi sana kuuzuia moyo usilpe kisasi, utapingana na maneno yake ya mdomoni.

Kutokana na ukubwa wa uzuri au ubaya wake, yako matukio ambayo ili uwe na amani na afya kamili ni lazima uyalipe kama ukiPata muda wa kufanya hivyo. Huwezi kumlipa ubaya mtu aliyekuponya na sumu kali ya nyoka, lakini huwezi kumpenda mtu aliyechoma nyumba chako ukiwa ndani na familia yako yote.

Tusidanganyane Kuna watu lazima atawaonja TU, wajitokeze kwake wenyewe kwa njia na namna zao na kusema "we are sorry" .
 
Back
Top Bottom