Makonda atoa bima ya afya kwa watoto 625

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,327
6,850
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amegawa kadi za bima ya afya za Mfuko wa Jamii (CHF) kwa watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu 625.

Akizungumza wakati wa kutoa bima hizo, Makonda alisema anatoa zawadi ya sikukuu za Christmas, mwaka mpya na Maulid baada ya kubaini changamoto ya matibabu kwa watoto hao.

Makonda alisema uandaaji wa bima hizo kwa watoto umewezekana kutokana na ufadhili wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

“Bima za watoto zimetokana na ufadhili kutoka nchi za Falme za Kiarabu, Niliwaza niandae chakula nile na yatima? Nikaona tutakula, tutakunywa kwa siku moja vitaisha lakini matibabu watatibiwa mwaka mzima mahali popote watakapokuwa hapa nchini”

“Balozi wa nchi Falme za Kiarabu Balozi wa UAE, Khalifa Abdulrahman, aliponitembelea na kuuliza eneo la kusaidia niliwakumbuka watoto yatima na wasiojiweza nikaomba kuugwa mkono kuwapatia bima ya afya”alisema Makonda

Aidha Makonda alimpongeza John Magufuri kwa maendeleo anayoyafanya kwenye sekta ya afya na kuwataka Watanzania wajitaidi kuwa na bima ya afya haswa madereva bodaboda ili kuwasaidia kupata matibabu wanapopata matatizo.

Pia Balozi Abdulahman alisema anashukuru umoja na ushirikiano baina ya nchi yake na Tanzania na wanapenda kusaidia watu wenye uhitaji katika secta ya elimu na afya kusaidia maendeleo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Yudas Ndungile, alisema bima walizopatiwa watoto hawa zitawasaidia kutibiwa katika hospital, zahanati na vituo vya afya viliyopo eneo lolote wilayani na mkoani.


Chanzo: Mtanzania
 
Back
Top Bottom