Imalamawazo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2021
- 1,343
- 3,286
Ndugu japo unasema huna imani lakini mimi nakuona ni Mungu amekupa muda wa kutafakari. Ulikuwa unaelekea kuwa imani kali. Muombe Mungu aufupishe huo muda wako wa tafakari.Stuxnet sikuwa nataka kusema hili na wala sijawahi kulisema kwenye jukwaa hili.
Niseme ukweli mimi ni Mkatoliki niliyebatizwa na kupata Komnio na kipaaimara.
Niliacha kwenda Kanisani Tangu 2016 baada ya kuona Muunganiko wa JPM, Makonda na Pengo.
Huu muunganiko ulinikwaza sana kwenye Imani ya Kristo Yesu.
Hadi leo sina imani sana.
Mbele za Mungu sote tu wadhambi wala hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia mtu yeyote asiifikie huruma ya Mungu. Mbele za Mungu hakuna dhambi nyingi bali kuna huruma nyingi. Mdhambi yeyote anayetubu muda wowote anapokelewa. Hivyo tusikwazike pale tunapowaona wale tunaodhani ni wadhambi wanapokaribia watumishi wa Mungu.