Makonda aombwa azuie filamu za nje

maatope

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
1,424
956
stevevee.jpg
Steve Nyerere

MSANII wa filamu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameshikilia bango la kutaka filamu za nje zizuiwe hapa nchini kwa kuamini kuwa, soko la filamu za Kibongo litazidi kutanuka na kufanya vizuri.

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kila anapofikiria masuala ya filamu jambo hilo huwa linazidi kumnyima raha na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulishughulikia kwa kuwa yeye ni kiongozi wa serikali kuhakikisha wasanii wa filamu za Kibongo wanakuwa na amani katika kazi zao.

“Nimefurahi sana Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar. Namuomba alifanyie kazi suala la filamu za kigeni, ahakikishe hazipati nafasi kubwa isipokuwa filamu zetu,” alisema Steve.
 
Upupu mtupu.

Kwani kaambiwa filamu za nje ndo zinazofanya watu wasihangaike na maigizo yao? Kama wangekuwa wanatumia muda wa kutosha, utaalamu na ubunifu wa kutosha kuandaa kazi zao watu wangeangalia na kuzipenda kazi zao bila kujali za nje zipo au la.

Hata wangekuwa na uwezo wa kuzuia kuziuza mtaani na ku-download pia hamna mtu ambae huwa haangalii maigizo yao ataangalia kisa hana access na filamu za nje.
 
Uyu jamaa atakua ni mwanaume wa Dar bila shaka,mtu mzima uwezi kuongea ujinga kama huu.
Kama Movie zenu hazipendwi tafuteni sababu ya kwanini hazipendwi au haziuziki mkipata tatizo tafuteni njia ya kutatua tatizo.
 
Yan wanizuie kuiangalia London has fallen kwa ajili ya muvie ya tajiri mfupi mweee waigizaji wenyewe ndo hao wanywa maji na wengine makalio yao yana pelembeka
Mpyeeee
hahahaaaaa siangaliagi kabisa movie za bongo sema kuna siku nasafiri niliiona hiyo movie kwenye basi, hivi yule jamaa ni mtoto au mtu mzima?
 
Steve Amtwisha Jukumu la Filamu Makonda

******sual hili ni la kizalendo na bwana makonda kwa hakika tunaamini ataliweza. Makonda akifanikisha hili tunaomba pia Nape nnauye azuie watu kuangalia ligi ya Uingereza na Hispania ili wananchi waelekeze mapenzi kwa ligi bora kabisa ya Tanzania bara.
Cheeers

stevevee.jpg
Steve Nyerere

Stori: MAYASA MARIWATA

MSANII wa filamu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameshikilia bango la kutaka filamu za nje zizuiwe hapa nchini kwa kuamini kuwa, soko la filamu za Kibongo litazidi kutanuka na kufanya vizuri.

Paul-Makonda-1.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kila anapofikiria masuala ya filamu jambo hilo huwa linazidi kumnyima raha na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulishughulikia kwa kuwa yeye ni kiongozi wa serikali kuhakikisha wasanii wa filamu za Kibongo wanakuwa na amani katika kazi zao.

“Nimefurahi sana Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar. Namuomba alifanyie kazi suala la filamu za kigeni, ahakikishe hazipati nafasi kubwa isipokuwa filamu zetu,” alisema Steve.
Huyu Stive Ni Mpuuzi kabisa, unaweza kuona hawa watu WA Bongo movie walivyokua wababaishaji, Ni mjinga Tu NA mwenye uwezo WA chini Sana wa kufikiri anaweza kuwaza hivyo...Kazi zao mbovu, hazina ubunifu wowote, wanawaibia Tu walaji kwa part 1&2 zao, story mbovu, quality ovyo, hafu wanalazimisha watanzania kutizama ujinga!
 
Kwa dunia hii kama kijiji azuie Movie za nje ??
Hawa ndugu zetu wa bongo movie sijui nini kimewakumba ,bora hata niangalie Mambo hayo ya kina Bishanga, Kaole ile ya kina Muhogo mchungu ,Kibakuli ,nyamayao ,na kidedea ya kina Jengua
 
uwezo mdogo wa kufikiri unalitesa sana taifa letu... ni aibu kubwa mtu kuhusisha filamu za nje kuwa zinaua soko la bongo movies.. very little poor understanding which leads us to be more than poor
 
Anafikiri nayo imekuwa sukari enhee.Sukari hatuwezi ku-download ila filamu,muziki n.k.tushindwe kuangalia?Kwa wazo hilo la mtoto wa chekechea ataonesha nini kizuri kwa hiyo tasnia yao ya kibongo.Mtu mmoja mtunzi mwenyewe,director mwenyewe yaani kila kitu anafanya yeye then kitu kiwe bora?Mtu anaoneshwa anatembea weeee hadi dakika 5 zinaisha nimuangalie yeye.Filamu nzima wapo wahusika watatu tu hivi hata kama ni utunzi sidhani kuwa unaweza kuwa hivyo....damn!!!

Waongeze ujuzi,maarifa na ubora wa filamu zao kwanza japo hawawezi kumwekea mipaka mtazamaji kuhusu hilo.
 
Back
Top Bottom