Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Hivi ni lini mtaniheshimisha na hata Kunijengea Mnara wangu GENTAMYCINE hapa JamiiForums? Mna uhakika kuwa sikuwahi Kuanzisha Uzi hapa hapa JamiiFoums tena nikisema na kuna mahala nikayafumba Majina ya hawa hawa waliotajwa jana na Makonda na baadhi ya Intelligent Members hapa wakayajua?

Mna uhakika kabisa hakuna Uzi hapa JamiiForums wa mwaka Juzi au mwaka Jana ambao GENTAMYCINE niliuandika tena kwa kumtaka Mheshimiwa Rais Samia awe makini sana na Watu wanaomzunguka na kumtaka awe nao makini na tena Kimafumbo kabisa na hadi kule Kijiweni Kwao Mbezi Beach wanakokaaga nikawataja?

Nasisitiza tena kubalini tu kuwa kuna Watu wengine hapa duniani hatukubarikiwa tu Akili Kubwa bali tuna Maono pia. Hivi mnadhani GENTAMYCINE kuwa na Signature yangu hii pendwa na Tukuka ya "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Enterainer" nilikurupuka tu? Signature yangu inaelezea Uhalisia wangu.
Uzieako niliouna, makonda kacheza mle mle lakini nani atamfunga paka kengele? Je out of team aliyonayo mhe rais anasikiliza shauri za nje ya mfumo? Maana huo mfumo ndio unamfunga na kuchuja yapi ya kumpelekea
 
Tamko alilotamka Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni tamko mbaya sana na linaleta uchochezi na chuki. Ni aibu kutamka mbele ya kadamnasi ya watu kuwa kuna watu wanamtukana Mhe. Rais. Jambo hili alitakiwa amueleze Mhe. Rais kwa siri kubwa. Mhe. Rais Mkuu wa Mkoa wa Arusha hakufai ni bora umtumbue mapema atakuletea uadui mkubwa na Watanzania. Kikubwa anajipendekeza kwako.
hukutakiwa na nani?🐒
 
Hivi ni lini mtaniheshimisha na hata Kunijengea Mnara wangu GENTAMYCINE hapa JamiiForums? Mna uhakika kuwa sikuwahi Kuanzisha Uzi hapa hapa JamiiFoums tena nikisema na kuna mahala nikayafumba Majina ya hawa hawa waliotajwa jana na Makonda na baadhi ya Intelligent Members hapa wakayajua?

Mna uhakika kabisa hakuna Uzi hapa JamiiForums wa mwaka Juzi au mwaka Jana ambao GENTAMYCINE niliuandika tena kwa kumtaka Mheshimiwa Rais Samia awe makini sana na Watu wanaomzunguka na kumtaka awe nao makini na tena Kimafumbo kabisa na hadi kule Kijiweni Kwao Mbezi Beach wanakokaaga nikawataja?

Nasisitiza tena kubalini tu kuwa kuna Watu wengine hapa duniani hatukubarikiwa tu Akili Kubwa bali tuna Maono pia. Hivi mnadhani GENTAMYCINE kuwa na Signature yangu hii pendwa na Tukuka ya "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Enterainer" nilikurupuka tu? Signature yangu inaelezea Uhalisia wangu.
Attach uzi husika..!!
 
Kiukweli Uhuru wa kuongea tuna utumia vibaya
hautumiki vibaya neno uhuru unatambua maana yake?unatambua maana ya demokrasia?kwenye demokrasia unatakiwa kuvumilia (political torelance) sababu binadamu tumetafautiana wapo ambao njia yao ya kutuma ujumbe mpaka afokee,mwingine aseme kwa upole,mwengine atukane,mwengine afikiriee sana hivyo vyote unatakiwa kukubali.
 
Kujua kipi useme, useme wapi, wakati gani, na kwenye mazingira gani, kunahitaji akili ya kiwango fulani. Kama huna hiyo akili utabakia kuropoka chochote, wakati wowote na mahali popote.

Rais Samia ameyataka mwenyewe. Hakuna aliyemlazimisha amteue Makonda kwenye nafasi yoyote ile. Haya ni madogo, asubirie makubwa zaidi. Magufuli aliamua kuachana naye kabisa alipokuja kugundua kuwa aliyekuwa anamwamini alikuwa tapeli. Akaenda kugombea ubunge huku akiwadanganya watu kuwa ametumwa na Magufuli agombee ubunge ili ateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani. Hayati Magufuli alipoambiwa, aling'aka na kusema kuwa yeye hajamtuma mtu yeyote akagombee ubunge. Ndipo akaomba arudi kwenye ukuu wa mkoa, marehemu akamkatalia katakata, wakati huo akiwa tayari amefikishiwa taarifa kuwa jamaa amewatapeli GSM nyumba kwa kuwadanganya kuwa Rais alikuwa ameomba wamjengee, kumbe ni yeye ndiye aliyekuwa anahitaji kujengewa nyumba. Hapo akawa takataka mbele ya JPM.

Samia, takataka aliyoitupa mtangulizi wake, ameiona lulu. Asubirie kashfa zitakazompata kwa kupitia huyu mtu. Atapora magari, fedha na nyumba za watu kwa kutumia jina la anayemwita eti ni mama yake. Rais ameyataka mwenyewe, hajajua kuwa tumbili huwa hafugiki.
Pamoja na yote hayo unadhani kwanini Samia alimchukua huyo Makonda?
 
sio hoja tu,

bali pia kijana ana maono ya mbali, nia ya dhati, uwezo na ujasiri wa kipekee sana, si tu wa kusema kwa maneno, bali pia kutenda kwa vitendo 🐒

ana tofauti ndogo sana na Hayati Edward Moringe Sokoine.
Itoshe tu kusema, Makonda ni Sokoine wa nyakati hizi, atafika mbali 🐒
 
Makonda hafai kuwa kiongozi
Hafai kuwa kiongozi wa wapi au akina nani? Hilo ni la msingi kujiuliza, kwa nchi kama Tanzania sidhani kama Makonda hafai labda ingekuwa nchi nyengine. Ndio maana hapo wengine wanakwambia pengine Rais mwenyewe ndio anamtuma Makonda kufanya hicho anachofanya.
 
Back
Top Bottom