Makonda acha kuwaingiza wanawake mkenge

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,841
52,821
Na, Robert Heriel.

Mhe. Makonda sijui wapi unakwama, mara nyingi umekuwa mtu wa kutoa Boko. Huenda unamawazo mazuri lakini hujui namna ya kuyatekeleza.

Lakini nina uhakika kuwa wewe ni mtu wa kutafuta kuzungumzwa mitandaoni, vijana wa siku hizi wanaita Mzee wa Kiki. Katika hili nadhani ndio unalimudu kuliko jambo lolote.

Kwanza nataka ujue kuwa Mshahara ni wa mtu mmoja. Hata ukienda kuomba kazi, iwe ni serikalini au sekta binafsi mshahara haupigiwi mahesabu ya watu wawili, ati sijui umeoa au haujaoa. Sijui unafamilia au hauna. Mshahara unapigiwa mahesabu ya mtu mmoja, tena yule anayefanyakazi. Wala masuala ya familia yako hayapo hapo.

Mshahara pia unazingatia ujuzi wa mtu, elimu yake, uzoefu, uzalishaji wake katika ofisi husika. Mara chache mshahara unazingatia hali ya maisha ya wakati husika.

Hata ukiulizwa kwenye usaili, kuna swali linauliza; unataka ulipwe kiasi gani. Sio tuwalipe kiasi gani. Mfanyakazi hafanyi kazi kwa niaba ya familia. Hufanya kazi kwa niaba yake mwenyewe. Yeye kama yeye. Hata ikitokea amekufa, kinachofanyika yale mafao sio kwamba familia huchukua kwa sababu ya nini. Bali huchukua kwa haki ya ndugu yao.

Mhe. Makonda umekuwa mtu wa kupenda kuingilia mambo ya familia za watu yasiyokuhusu, bila kujua yapi ni madhara ya kuingilia kwako.

Kusema 40% ya mshahara wa mwanaume mfanyakazi apewe mkewe ambaye hafanyi kazi ni kuzua migogoro isiyo na maana.

Kama ungekuwa kiongozi mwenye maono ungetakiwa utoe fursa kwa wanawake walioolewa ambao hawana kazi ili wapate kazi za kuzisaidia familia zao. Wewe unataka kuleta utegemezi ndani ya familia na ndani ya nchi.

Badala utoe mikopo yenye unafuu kwa kinamama ili wafanye ujasiriamali ambapo watapata fedha za kujikimu wao na familia zao, wewe unasema mwanaume akatwe. Hivi hiyo ni akili au matope. Kesho mwanaume amekufa, au kafukuzwa kazi, embu tuambie nini kinafuata kwa wanawake waliokuwa wanapewa 40% ya mishahara za waume zao waliokuwa wanafanya kazi.

Makonda umekuwa mtu wa kuwatetea wanawake kwa namna isiyowahi kuwasaidia. Kila jambo unalolianzisha linaishiaga hewani, ni hii ni dalili ya kuwa hukuwa umejipanga na kudhamiria kuwasaidia.

Makonda, umesema utapeleka muswada bungeni kuwa wanaume wafanyakazi wakatwe 40% ziende kwa mke. Sijajua kama ulifikiria kuwa wapo wanaume wenye wake watatu mpaka wanne ambao sio wafanyakazi. Sijajua kwa hakika kama uliliwaza jambo hilo.

Je hiyo asilimia 40% mgawanyo wake umekaaje kwa Mtu mwenye wake wawili, watatu, wanne na kuendelea.

Hujaeleza kwa wale wenye wake wanaofanya kazi kuwa wao utaratibu ukoje. Haya kama wao hawakatwi. Huoni utazua balaa na kuwapa wakati mgumu wanawake wasio na kazi?

Huoni kama utasababisha wanawake wasio na kazi kukosa soko kwa vijana wanaotaka kuchumbia. Hukufikiri kuwa Wanawake wasio na kazi kuwa watakosa wanaume wa kuwaoa? Hakuona kuwa wanaume wengi vijana watawapuuza wanawake wasio na kazi na kuwang'ang'ania wenye kazi kisa kuogopa makato ya 40%.

Mhe. Makonda huoni unawaingiza mkenge wanawake na kuwafanya wadode bila kuolewa hasa wale wasio na kazi?

Huoni kuwa kitendo cha mwanaume kukatwa 40% kitawafanya wanawake wengi kuwa wavivu na kuwadumaza?

Huoni kuwa utazidisha utegemezi katika taifa, nakupunguza nguvu kazi ya uzalishaji ndani ya nchi?

Mimi sioni kama unamantiki katika mawazo yako, japo nakushukuru tuu kwa kutoa maoni yako ambayo tunayaheshimu ingawaje ni maoni ya hovyo ambayo utekelezaji wake utaleta madhara kama nilivyobainisha hapo juu.

Kitu pekee ambacho Makonda angesifiwa na watu wenye akili ni kuwapa wanawake hao kazi za kufanya au kuwapa mikopo ya kufanyia ujasiriamali, kuandaa mikakati kabambe ya kusambaza elimu ya ndoa ya namna ya watu kuishi kwa amani bila manyanyaso kwa kuwahusisha viongozi wa dini, asasi za kiraia zinazohusiana na mambo ya familia, kukaa bega kwa bega na vyombo vya habari kueneza propaganda na namna ya kuwafanya wanandoa waishi vizuri kila mmoja kwa nafasi yake, Kutoa elimu ya maadili ya ndoa kwa jamii, tena ikiwezekana iundwe kozi maalumu utakaoingizwa kwenye mitaala ya vyuo vikuu, vyuo vya kati na hata iwe Mada kwenye elimu ya sekondari (kidato cha nne na sita).

Binti au kijana aliyefikisha kuanzia miaka kumi na tano, anaweza kufundishwa somo la ndoa kwani huo ndio wakati wa kuoa au kueolewa. Hivyo iwe mada kabisa. Wakati mwingine migogor ndani ya ndoa ni matokeo ya elimu duni ya mambo ya ndoa baina ya wanandoa.

Kazi ya serikali na waajiri wengine ni kufanyiwa kazi na wafanyakazi waliowaajiri na sio kupangia watu matumizi ya mishahara. Tofauti na hapo huo huitwa utumwa.

Makonda aacha kuwaingiza wanawake Mkenge.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Niliwahi kumwambia wife kwamba, nikija kumsikia ameenda kwenye mikutano ya kipuuzi kama hii, na nikisikia ameenda kwenye yale makanisa ya sijui nabii nani nani/upako and the like..... Basi ajiandae kuipokea talaka straight away without any kind of discussion
 
Niliwahi kukwambia wife kwamba, nikija kumsikia ameenda kwenye mikutano ya kipuuzi kama hii, na nikisikia ameenda kwenye yale makanisa ya sijui nabii nani nani/upako and the like..... Basi ajiandae kuipokea talaka straight away without any kind of discussion

Sent using Jamii Forums mobile app


Mimi nimejipambanua muda mrefu sana Mkuu. Hilo analijua na watu wote wanajua, kinachosubiriwa na utekelezaji siku lakutokea likitokea
 
Wanawake wenyewe wanashangaa! 40% ya mshahara...huyu mkuu limbwata tayari sio bure Anataka kufanya ndoa iwe Ajira huyu.
 
Inawezekana jamaa anafanya kazi pasipo kuwa na washauri Maana kunabaadhi ya mambo inatakiawa yajadiliwe na kamati maalumu then mtengeneze muswada usio na mashaka,

kikubwa ajaribu kuchunga mdomo wake maana tuna nchi yenye katiba yake.
 
Back
Top Bottom