Makinikia ni nini?

Siku hizi wengi tumejifunza makanikia ni mchanganyiko unaotokea ukianza kushughulika mbale wa madini kwa kemikali.
Hapa tumesikia habari za haya makanikia yenye dhahabu na madini mengine na kupulekwa nje kwa kusafishwa.
Asili au etimolojia ya neno bado sijaelewa
 
Kumbe sasa naona walipata wapi neno hili "makinikia":

makini nm [ya-] 1 attention, concentration:
kwa ~ attentively. 2 calmness with
concentration. kv attentive, calm.

makinik.a kt [sie] be calm, concentrate. (tde)
makinikia; (tdk) makinikika; (tds)
makinikisha.

Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili iliyotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar
 
Tunaweza tulaumu tu hata maana ya makanikia hatujui?
Asante kwa swali hili; kuuliza si ujinga. Nimekumbana nalo sehemu nyingi sana kule Youtube lakini bado niko hoi. Mwanzoni nilidhani ni matamshi mabaya ya neno Makenika (yaani fundi mitambo) lakini nimegundua kuwa ni neno jipya katika lugha ya kiswahili. Ukipata jibu sahihi nibipu na mimi pia!
 
Makinikia limetokana na concentration za kwenye mchanga
Makini -concentrate
Mineral concentrates/concentration ndo tunapata makinikia
 
Back
Top Bottom