Makinika! Hakuna tofauti ya ndoto na mtu, ndoto ndiyo mtu mwenyewe

Makinika! Hakuna tofauti ya ndoto na mtu, ndoto ndiyo mtu mwenyewe

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam, Shalom!

Ndoto ni Nini?

Umewahi ota ndoto ukadhani unaota?

Usilolijua ni kuwa, hakuna kinaitwa kuota ndoto!

Ukisikia Imeandikwa akalala, Kisha akaota ndoto, SI maigizo, ni tukio halisi la wewe mwenyewe kuona kwa macho ya Roho Katika ulimwengu wa Roho.

Mtu alalapo, afungapo macho ya mwili, hufungua macho ya Roho, hivyo ndoto ni tukio halisi, ndoto ndio WEWE mwenyewe,


WEWE ndio ndoto yenyewe.

Sasa kuanzia Leo, ukiona mambo au matukio Katika lugha ya picha ulipolala, usippuuze🙏

Yupo Mungu kukusaidia kuyajua uliyoyaona ullipolala.

Mbarikiwe nyote .

Karibuni kwa maswali.

Source: Ayoub 33:15
 
Katika maisha yangu yote hakuna ndoto nmeota ikaja tokea kweli.

Kwa hiyo unaniambia kule tunapoota ni dunia nyingine? Haihusiani na hii tuliyopo? Na wale watu tunaowajua na kuwaota tunakutana kweli huko ndotoni?
Si kweli,

Mengi yametokea uliyoona,

Labda nikunaliane nawe, hukujua kutafsiri maana lugha inayotumika kule ni tofauti.

Ukiona maji ni watu,

Wanyama ni watu,

Miti ni watu,

Barabara ni njia, hatma yako upitiayo,

Shule ni WEWE mwenyewe, darasa/ jengo ni kanisa, na kanisa ni wewe, mafundisho ni maelekezo uyapatayo, unayoyahitaji Ili kupiga hatua mbalimbali Maishani.
 
Kwahiyo ndugu yangu Rabon nikikuona ndotoni una jinsia ya kike itakua ni kweli?

Tuchukulie upo sahihi, kipofu wa kuzaliwa anaota ndoto za audio au video?
Mbele za Mungu,

Kanisa ni bibi harusi.

So we have one Lord Jesus.

Na kuhusu kipofu kwamba huota ndoto aina gani?

JIBU: Mtu ambaye ni Roho, SI kipofu, mbinguni hakuna kipofu, upofu ni Katika mwili.

Kipofu huota ndoto sawa na aonaye,

Changamoto yake ni kutafsiri Katika ulimwengu wa mwili ambao macho yake yamefumbwa.

Sasa Kila kitu kina tafsiri yake.

Karibu
 
Si kweli,

Mengi yametokea uliyoona,

Labda nikunaliane nawe, hukujua kutafsiri maana lugha inayotumika kule ni tofauti.

Ukiona maji ni watu,

Wanyama ni watu,

Miti ni watu,

Barabara ni njia, hatma yako upitiayo,

Shule ni WEWE mwenyewe, darasa/ jengo ni kanisa, na kanisa ni wewe, mafundisho ni maelekezo uyapatayo, unayoyahitaji Ili kupiga hatua mbalimbali Maishani.
Kwa hiyo sijui kutafsiri ndoto zangu?

Haya nipe code za kutafsiri zaidi...

No reform no election
 
Halafu utaniambia unatafsiri kwa njia gani au vitabu gani?
Tafsiri ni KUPITIA Neno la Mungu kwa msaada wa Roho mtakatifu.

Mungu KUPITIA Roho mtakatifu ndiye pekee awezaye kukwambia uliota Nini na tafsiri yake hata kama ulisahau ulichoota, rejea Mfalme Nebuchadnezzar.

Hali uliyonayo na mkwamo au mafanikio yamefungwa Katika ndoto uzionazo.
 
Ushawai ota umekatwa kiongo chako
Kuwa serious.

Ndoto zingine ni taarifa ya matukio ya kutukia karibuni, hupasi kuchelewa.

Yusufu anamtabiria mtumishi wa mfalme ndoto yake Leo,

Kesho yake ndoto inatimia, anakatwa kichwa.

Ukiona ndotoni ndege wanakulla mahindi au nafaka ulizobeba kichwani kwenye sinia,

Jua MAISHA yako hatarini. Hiyo ni mauti immechungulia Maishani mwako. Au Ukiniona umo shimoni, shimoni ni kaburini, stuka, kimbia haraka kwa Yesu wa msalabani.
 
Ukiniona ndotoni umetumbukia shimoni.

Tafsiri ya shimo kibiblia ni kaburi, kuzimu, nyumbani pa wafu wasiomjua Mungu,

Unaarifiwa, adui amekutegea Ili akumalize uingie kaburini kabla ya wakati wako.
 
Ukiona ndotoni, au ukimwona mtu anakula chakula kizuri Kisha ghafula a akikataa na kuondoka,

Unaarifiwa mtu huyo amechoka KUISHI na anajiombea afe mapema.

Chakula ni uhai.

Imeandikwa, Moses, Ibrahimu, Yakobo walishiba siku .

Kumbe KUISHI ni kula chakula Katika lugha ya ndoto.

Ingawa SI Kila chakula ni MAISHA, chakula pia kina tafsiri zaidi ya hiyo kutegemea na mahali ulipokula chakula, amani au hofu juu ya chakula ulacho nk nk.
 
Ukiona Katika ndoto unahubiri,

Ukiona ndotoni unaomba au unafundisha,

Tafsiri ni karama ulizijaaliwa na Mungu unaarifiwa uzitumie au ndipo unapotakiwa kuingia kazini illi ufanikiwe maana ulizaliwa utimize makusudi hayo.
 
Ukimwona mtu anakujia amevaa mavazi meupe, ni mtu mwema huyo.

Ukiona mavazi meusi amevaa mtu na ukahisi hofu au kumchukia ukaanza kupambana naye, ni mbaya huyo.
 
Ukiona nyoka ndotoni ni hila, ni uongo unakunyemelea,

Ni adui aja na ataka akuangamize.

Rudi kundini uongeze ibada ,utaishi.
 
Ukiona mahali Pako unapofanyia ibada pamejaa nyoka,

Nyoka ni ishara ya uongo ,hila nk nk

Unaarifiwa, mahali pale madhabbahu SI ya Mungu, wanatumia uchawi.

Kimbia.
 
Ukiona uko uchi, au ukimwona ndugu yako Yu uchi,

Aibu inakuja,

Uzinzi unamnnyyemmelea,

Ikiwa ni mtumishi, Mungu amemwacha, aibu inamnyemelea kwa kukaa dhambini.

Rejea Bustani ya Edeni, walipokula tunda walijiona wa uchi.

Ndiyo lugha ya picha ya ndoto.
 
Ukiona unapaa,

Unakimbizwa na kupaa na adui anakukimbiza unapaa na kumuepuka,

Usidanganywe na waovu,

Unazo nguvu Mungu amekupa za kuwashinda wabaya,

Rejea, Elia yule Nabii alinyakuliwa kuwakwepa maadui.

Yesu alipaa pia.

Hiyo ndio lugha ya picha ya ndoto.

NB: Upaaji huo uangalie, ikiwa unapaa na watu wenye mavazi meusi, stuka, unaroga bila kujua,U mchawi kipofu.
 
Ukiona umo mstuni ,

Au umeambatana na mtu akupeleka mstuni na kukuacha huko, na ukaingiwa na hhofu ndotoni,

Huyo mtu ni rafiki mbaya, amevaa sura ya urafiki nje, ila ni mtu mbaya.

Mwache haraka.
 
Ukiona umeumwa nyoka Katika kidole Cha kuvaa Pete ya ndoa,

Jua fika, adui anawinda ndoa yako aivunje, Ili nguvu ipungue uliyokuwa nayo ndani ya ndoa,

Rudi kutengeza mahusiano na Mungu wako, Jenga MAISHA ya maombi.
 
Back
Top Bottom