CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,388
- 6,482
Mheshimiwa Makinda, hiyo tume kama ni ya CCM haitaleta la maana. You are always extremely biased. Huwezi kumwangusha aliyekuweka madarakani. Kupoteza hela tu,waambie wananchi kwa nini leo hujatangaza majadiriano ya Bunge.
This is a bad indication!!!!!! hata makanisa waliwahi kukwambia kuwa uko biased to the love of ruling party!
This is a bad indication!!!!!! hata makanisa waliwahi kukwambia kuwa uko biased to the love of ruling party!
Frank Prosper said:...SPIKA ANNA MAKINDA AMEONYESHA NJIA, TUNAISUBIRI KAMATI MTWARA TUIELEZE UKWELI!
Kauli na kitendo kilichofanywa na Spika wa Bunge, Mama Anna Makinda ndiyo kitendo cha kiungwana ambacho sisi Watanzania tulikuwa tukikisubiria kutoka kwa Wanasiasa wetu ama viongozi wetu waandamizi wa Serikali kabla ya hata vurugu zote zile na mauaji yote yale hayajajiri Mkoani Mtwara.
Spika wa Bunge, Mama Anna Makinda amewatangazia Wabunge juu ya kuunda kamati itakayokwenda Mtwara kwa Madhumuni ya kupata mapendekezo ya Wananchi juu ya Mgogoro wa Gesi unaofukuta moto mkoani humo.Aidha pia kamati hiyo ambayo itakuwa na maudhui ya kitendaji katika kutafuta suluhu kuhusiana na suala la mgogoro wa nishati hiyo ya gesi.
Haya ndiyo mambo ambayo yalipaswa yafanyike awali na Serikali,tena kabla hata ya Bunge kupitia Spika wa Bunge kutangaza uundwaji wa kamati hiyo.
Kuna jambo ambalo limenigusa mno kwenye matamshi ya Spika wa Bunge, ni pale alipoamua ‘kuwakata ngebe' wabunge ambao walijaribu kushinikiza Spika wa bunge na bunge kwamba ni vyema suala la gesi Mtwara likajadaliwa bungeni kama hoja ya Dharura. Kwa bahati mbaya ama mzuri Spika wa Bunge aliamua kuwaeleza Wabunge hao kwamba, ile hoja si ya dharura na akaeleza pia ukweli, kwamba Wabunge ambao wanasema lijadiliwe kama suala la dharura wengi wao hawalifahamu kwa undani, kwa hiyo badala ya kujadili jambo ambalo hawalifahamu kwa undani, ni afadhali aunde kamati ambayo itakwenda Mtwara,baada ya kurudi kutoka huko Mtwara, itakuja na majibu, na mapendekezo ya Wananchi na ndipo Bunge litajadili ndani ya Mkutano huu wa kumi suala hili la gesi kwa undani.
Spika Mama Anna Makinda amerusha kombora katika hili, na bila shaka kuna kundi ameligusa.Sitaki kuhoji.Ila nachotaka kuhoji,je ni akina nani wanalifahamu suala hili kwa undani? Ikiwa wabunge waliotaka jambo hili lijadiliwe kama dharura hawalifahamu kwa undani..(kwa tafsiri yangu: wamedandia tu jambo ambalo hawalijui kwa maslahi yao). Sasa,ni nani analifahamu kwa undani? Ni serikali ya CCM au Wananchi wanaolifahamu jambo hili kwa undani?.
Mgogoro wa gesi kati ya Serikali na Wananchi,wanaofahamu kwa undani ni Wananchi wa Mkoa wa Mtwara, Rais Jakaya Kikwete na Chama chama cha Mapinduzi kama chama tawala.NDIYO, na hata nikiambiwa nithibitishe nitasema.
Kwanza: Katika Kampeni za uchaguzi mkuu Mwaka 2010, Chama cha Mapinduzi katika Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010-2015 imetamka wazi katika Ibara ya 63 kifungu cha" H" na "K" juu ya gesi ya Mnazibay Mtwara na Songo songo Kilwa, Lindi kuhusu umeme wa (240 MW) Kinyerezi na (300MW) Umeme wa Mnazi bay Mtwara..
-Vifungu hivi vinaainisha na kufafanua mambo yafuatayo:
• Gesi ya Mnazi bay itakuwa kwa ajili ya Mitambo ya kuzalisha umeme ambayo itajengwa Mtwara (300MW)
• Mitambo ya kuchakata gesi kujengwa Mtwara
• Ujenzi wa viwanda Mtwara ili malighafi itokanayo na gesi itumike kutengeneza mbolea, plastiki vikiwemo na viwanda vya Cementi
2. Gesi ya Songo songo inafafanua wazi kuwa gesi hiyo itapelekwa Kinyerezi . Dar –es –Salaam kwa madhumuni hayo hayo.
• Kuendeleza viwanda mbali mbali
• Kuzalisha umeme (240 MW)
• Kuchakata gesi kwa kujenga mitambo
Ushahidi wa Pili tunaousimamia: Katika ahadi ya Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania alizozitoa wakati wa Kampeni za uchaguzi katika hotuba yake ya tarehe 29 oktoba 2010 alitamka wazi kuwa, Mkoa wa Mtwara uwe tayari kwa maendeleo makubwa ambayo yanakuja kutokana na gesi iliyogunduliwa katika Mkoa wa Mtwara huko Mnazi bay. Rais Kikwete aliainisha juu ya viwanda mbalimbali vitakavyojengwa hapa mkoani Mtwara kama vile viwanda vya mbolea,simenti, plastiki, n.k na kuwataka wananchi wajiandae kupokea maendeleo hayo kwa kujenga nyumba nzuri zenye sifa kwa ajili ya wageni. Pia wawasomeshe watoto wao ili wawe na elimu ya juu na kupata ajira katika Makampuni yanayokuja.
Hata baada ya uchaguzi Rais Kikwete alipokuja kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa kumchagua, alitamka tena katika hotuba yake akisisitiza ahadi yake ileile ya kujenga viwanda ambavyo vitaleta maendeleo kwa Mikoa ya Kusini na kusababisha ajira kwa wana kusini, na kuagiza kwa Meya wa Manispaa Mtwara/Mikindani (Selemani Ntalika maarufu kama Shilingi) kuwapa maeneo ya kujenga viwanda hivyo, kwa kile kilichoonekana kukosa maeneo ya ujenzi huo kwa makampuni hayo. Ahadi hizi alizozitoa kwa wananchi kwa ujumla wao, walizipokea na kuendelea kuzifanyia kazi.
Chanzo cha Matatizo: Mara baada ya kuonekana kile walichokitarajia wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa kutumia gesi ya Mnazi bay kuleta maendeleo yao kuwa imeamriwa kusafirishwa kwa bomba na kupelekwa Kinyerezi Dar –Es –Salaam ili kuzalisha umeme na kuchakata gesi na mitambo hiyo iwe huko.(Mgeuko wa Ilani ya Uchaguzi, na kutozingatia ahadi zake mwenyewe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa kinyume na kauli za usemi wake mwenyewe kwa kukitangaza kituo cha Kinyerezi kuwa ni sehemu ya mitambo ya gesi ya Mnazi bay-Mtwara na Songosongo-Lindi na kwamba bomba hilo litachukua miezi (18) mpaka kukamilika kwake, kwa matamshi haya ndiyo yaliyoleta hasira na chuki kwa wananchi wa Mtwara/Lindi kwa ujumla.
Hoja hizi zinapatikana PIA katika tamko la Makanisa ya F.P.C.T kuhusiana na sakata hili la Gesi Mtwara.
Kwa mantiki ya shahidi hizo, na ndio maana Katibu Mkuu wa CCM ndg.Abdulreheman Kinana alitamka dhahiri akiwa mkoani Kigoma akiitaka Serikali iwasikilize Wana Mtwara kwani hoja zao ni za msingi.Kinana anajua wana Mtwara hawaandamani hivi kama wehu ,ni matokeo ya ungekeufu wa ilani ya CCM, ambayo hatujui ilikuwa na lengo la kutuhadaa wana Mtwara au la!
Sasa jambo la ajabu ni kuona wana Mtwara wanaitwa wahuni, Wehu,wahaini,hawajasoma pale tu wanapojaribu kudai kilicho halali yao(kwa sasbabu ilani ya CCM imeainisha wazi, na Rais Kikwete kama kiongozi wa Serikali alitoa ahadi hizo nilizoeleza hapo juu).
Na hapa sasa ndipo napoanza kupata wasiwasi na kiwango cha uelewa na uwezo wao wa kufikiri hawa ambao wanajiita WanaCCM na wanaowaita wana Mtwara Wehu,wahaini,hawajasoma na wabinafsi. Ni watu ambao wamekalia majungu,unafiki katika sakata la Gesi Mtwara, hawa wanachozingatia ni ushabiki wa kisiasa na siyo ukweli wa mambo.Hawa wanachojua ni kupewa amri tu na kuzitekeleza ila hawataki kusoma ilani ya CCM isemavyo na yanayojiri ndani ya Chama,ni wahujumu wa Chama cha Mapinduzi. Na mara zote wavivu wa kusoma huzaa uvivu wa kufikiri katika akili na fahamu zao.
Na niseme wazi jambo hili halihusiani kabisa na Upinzani,ni la Wana Mtwara wote bila kujali itikadi ya dini,kabila,rangi wala vyama,kwa sababu katika madai haya ya kutimiziwa ahadi tulizopewa: ahadi ya Rais Kikwete na ahadi za ilani ya CCM,hata wanaCCM wenye akili tupo (isipokuwa wale wehu wachache ambao wanaingiza ushabiki wa chama kuliko ushabiki wa Maendeleo, wenye laana ya Mwalimu Nyerere).
Wito wangu kwa WanaMtwara, Kamati hii ya Bunge itakapokuja Mtwara kupata Maoni ya Wakazi juu ya sakata hili, basi ni vyema tujitokeze kwa wingi na tueleze kwa hisia(tusitumie jazba) na wala tusimwogope yoyote katika kueleza yale kamati watakayokuwa wanahitaji wapate.Vijana wenzangu,tufanye hima,tusiwe nyuma.Twaendeni na nasi tukatoe dukuduku zetu,kumbukeni tulimchagua Rais Kikwete kuanzia Mwaka 2005,tukiamini(Kipindi kile) kwamba ni kijana mwenzetu na atakuwa bega kwa bega nasi katika kutatua kero zetu kama vile ukosefu wa ajira. Gesi ndiyo hiyo imekuja. Tunahitaji viwanda TULIVYOHAIDIWA tupate ajira.
''……TANZANIA YA SASA NI YA VIJANA, VIJANA NDIYO CHACHU YA MABADILIKO NA SIO CHAMA CHA SIASA. ‘Gesi Kwanza'. VYAMA BAADAE…….''
Source URL: https://www.facebook.com/JamiiForums/posts/472490069481659