Makinda aunda tume ya bunge kwenda Mtwara

Makinda aunda tume ya bunge kwenda Mtwara

Makinda has no clue kabisa, anategemea 'maagizo' toka kwa hao waliompa uspika, na matokeo yake ni bunge kukosa mwelekeo. Inakuwaje Makinda anaonekana kuguswa haraka haraka na issue ya Mtwara na sio ile ya mgomo wa madaktari, ambapo wagonjwa walikuwa walikuwa wanakufa kwa kukosa huduma? Mara 6 (six times) wabunge - toka vyama vyote - wanaomba kujadiliwa kwa mgomo wa madaktari lakini Makinda akakataa!

Leo hii anakuwa na haraka ya kuunda tume kwa sababu gesi ni sekta iliyojaa wawekezaji? Hapa maslahi yanayolindwa ni ya wazungu (rejea kauli ya Prof Muhongo)

Na Makinda angekuwa anajua anafanya nini angeshaunda Kamati ya Bunge inayohusika na Nishati na Madini baada ya kuivunja ile nyingine. Ni muda mrefu sasa sekta hii haina usimamizi wa bunge kama inavyotakiwa, lakini Makinda amekuwa busy akibadilisha ndege. Leo hii anaunda tume, Kamati ya bunge iko wapi?

Wadau, Spika naye ana madaraka makubwa bungeni kama alivyo Rais. Wabunge wanaweza wakata hoja fulani ijadiliwe, lakini nguvu aliyo nayo anakataa hoja ya wengi. Katiba iainishe wazi madaraka ya Spika na sio kuwa na mamlaka ya kukataa matakwa ya wengi bungeni kama ilivyo sasa. Una hoja ya msingi FJM
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wadau, katika mchakato wote wa katiba mpya naona wadau wamesahau madaraka ya spika. Spika kwa mtindo wa sasa ana madaraka makubwa kama yalivyo ya Rais. Ninavyofahamu ni kuwa anaweza kukataa hoja yoyote ambayo imeletwa mbele ya bunge kama haina maslahi kwake/chama chake/waliomweka madarakani etc. Nimenukuu maoni ya FJM kama mfano hapa chini in red! huu ni mfano mmoja tu.......

"Inakuwaje Makinda anaonekana kuguswa haraka haraka na issue ya Mtwara na sio ile ya mgomo wa madaktari, ambapo wagonjwa walikuwa walikuwa wanakufa kwa kukosa huduma? Mara 6 (six times) wabunge - toka vyama vyote - wanaomba kujadiliwa kwa mgomo wa madaktari lakini Makinda akakataa!"
 
Wadau, katika mchakato wote wa katiba mpya naona wadau wamesahau madaraka ya spika. Spika kwa mtindo wa sasa ana madaraka makubwa kama yalivyo ya Rais. Ninavyofahamu ni kuwa anaweza kukataa hoja yoyote ambayo imeletwa mbele ya bunge kama haina maslahi kwake/chama chake/waliomweka madarakani etc. Nimenukuu maoni ya FJM kama mfano hapa chini in red! huu ni mfano mmoja tu
......."Inakuwaje Makinda anaonekana kuguswa haraka haraka na issue ya Mtwara na sio ile ya mgomo wa madaktari, ambapo wagonjwa walikuwa walikuwa wanakufa kwa kukosa huduma? Mara 6 (six times) wabunge - toka vyama vyote - wanaomba kujadiliwa kwa mgomo wa madaktari lakini Makinda akakataa!"
kuanzia spika mpaka vyombo vya utangazaji wote ni wanamgamba,kutokuoonyesha bunge live tunajua kinachoogopwa ni kusikia ukweli utakaokuwa unasemwa na wabunge wa upinzani.na wanachutuambia kuhusu kinachoongelewa bungeni ni maoni ya wanamagamba tu,lakini hizo ni mbinu za maji taka,yote hayo yataisha baada ya 2015
 
Hata madaraka yeu sisi wananchi ni makubwa mno,ni vema katiba mpya iyaangalie namna ya kuyapunguza,tunaweza kujisajili kwa akaunt feki katika mitandao ya kijamii na kuanza kutukana watu hovyo,kukashifu ini za watu,kutukana viongozi wa vyama na serikali ,na hata wakati mwingine kujitukana sisi wenyewe.
 
magazeti ya leo yamemsifa sana waziri mkuu kumaliza sakata la gesi kwa kuwafahamisha wanaichi wa mtwarawatakavyofaidika na gesi kabla ya kupelekwa dar es salaam, bunge limeunda tume huu sio uaribivu wa pesa? mnasemaje wana jamiiforum?
 
magazeti ya leo yamemsifa sana waziri mkuu kumaliza sakata la gesi kwa kuwafahamisha wanaichi wa mtwarawatakavyofaidika na gesi kabla ya kupelekwa dar es salaam, bunge limeunda tume huu sio uaribivu wa pesa? mnasemaje wana jamiiforum?

Hebu hariri kidogo basi..., kuhusu kuundwa tume ni sehemu nyingine/upenyo wa kutafuna kodi zetu
 
Wewe unaishi DAR. Ungekuwa Mtwara, 100% ww ni miongoni ya wanaopinga dhuluma. "Wana Mtwara Gas kwanza uhai baadae". Kuwa mwana Mtwara pingana na dhuluma, uhai sio kitu, ukiwa kama serikali utadhalilika, sababu unaemdhurumu kila kunapokucha anakuwa na kitu kipya na kizuri zaidi ya jana. Tuache dhuluma kaka tutaumbuka.
 
magazeti ya leo yamemsifa sana waziri mkuu kumaliza sakata la gesi kwa kuwafahamisha wanaichi wa mtwarawatakavyofaidika na gesi kabla ya kupelekwa dar es salaam, bunge limeunda tume huu sio uaribivu wa pesa? mnasemaje wana jamiiforum?
nchi hii inaongozwa na maamuzi ya kipuuzi kweli kweli. sikuona haja ya kuunda Tume wakati Waziri Mkuu yuko Mtwara kushughulikia mgogoro wa gesi..sijui kwani alimpigia simu Spika kuwa ameshindwa kutatua mgogoro hivyo aunde Tume!!! huu ni ulaji wa pesa za watanzania tu. hii ni nchi ya Tume, Kamati, Warsha, Semina, Makongamano, nk.
 
nchi hii inaongozwa na maamuzi ya kipuuzi kweli kweli. sikuona haja ya kuunda Tume wakati Waziri Mkuu yuko Mtwara kushughulikia mgogoro wa gesi..sijui kwani alimpigia simu Spika kuwa ameshindwa kutatua mgogoro hivyo aunde Tume!!! huu ni ulaji wa pesa za watanzania tu. hii ni nchi ya Tume, Kamati, Warsha, Semina, Makongamano, nk.
lamsingi kamandakazi, tuhamasishane,tupeane moyo,tupeane habari, hasa kwa yale yanayotokea bungeni maana wameamua kutokuonyesha bunge live ili tusisikea hoja za wabunge wa upinzani
 
Spika anajifanya amekuja na wazo la kuunda tume, bila shinikizo la wabunge, amedai ameona pia 'vikaratasi vya wabunge wakitaka mjadala wa dharua', hapo hapo anadai hawatakuwa na cha kuzungumza maana hawajui issue nzima ni juu ya nini hasa wanamtwara wanataka. sawa mama, tumekusoma,

ila kuliko kuendelea kuharibu rasilmali fedha za wananchi kwa kupeleka watu kwenda kuuliza majibu, bora ungepotezea ukaendelea kujitoa akili hivyo hivyo, wewe si ndio spika bwana, ungesema tu hapa hamna mjadala wa mtwara/gas, kwanza serikali iko huko. kwani pm hawezi pia kukuletea jibu la kinachoendelea huko!
 
Mheshimiwa Makinda, hiyo tume kama ni ya CCM haitaleta la maana. You are always extremely biased. Huwezi kumwangusha aliyekuweka madarakani. Kupoteza hela tu,waambie wananchi kwa nini leo hujatangaza majadiriano ya Bunge.

This is a bad indication!!!!!! hata makanisa waliwahi kukwambia kuwa uko biased to the love of ruling party!
ndugu yangu chuakachara unachosema ni sawa,lakini makinda hana aja ya kujua ukweli,nia ya ccm ni kupoteza malengo na pesa, ukweli unajulikana bila hata kuunda tume,wabuge wa mtwara siwako bungeni wanawakilisha mawazo ya wanamtwara,kitakachofanyika hapo ni kuweka mawazo ya ccm na kuyatupa ya wanamtwara,kama walivyoanza kwa kutokuonyesha bunge live ili tusisikie oja za nguvu za wabunge wa upinzani
 
Wana jf,kume kuwa na matamko mengi kutoka ndani ya nchi yetu kuhusu kuisimamia serkali
Tume sikia kauli nyingi kutoka vyama vya siasa vya upinzani kuwa wao ndio wanapaswa kuisimimamia serkal na kuichallenge ili iweze kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Kuna kauli nyingi hasa siku za hivi karibuni kutoka chama tawala ccm zikitolewa na viongozi wa ngazi za juu mfano kwa sasa mkoani kigoma kuwa wana ccm wawawajibishe viongozi wa ngazi tofauti ili kuweza kutekeleza ilani ya chama chao

Wakati hayo yakiendelea.Bunge lime limejifunga kibwebwe na kusema hii ndio kazi yetu ss huku jana likikataa kutambua kinachondelea mtwara na kuunda tume ili kujiridhisha na majibu ya serkal
Wanaharakati na na asasi za kiraia wanasema ni kazi yao kuisimamia na kuikosoa serkal

Wahisani nao wanadai lazima wajue na watalamu wamambo ya kisiasa wanadai kuwa wahisani ni watu muhimu kwa hili.
Viongozi wa dini na wakimila wanaonekana kama wananguvu kubwa .tumeona tarime na mtwara
JE NINANI HASA ANA NGUVU KWA HILI.
Nawasilisha tujuzane .
 
Spika Anna Makinda kwa mara nyingine tena amewafunga midomo wabunge kwa kukataa hoja yoyote binafsi ambayo ilikuwa inataka kujadili swala la gesi ya Mtwara eti kwa kisingizio kwamba kuwa ni zito na nyeti, linalopaswa kujadiliwa kwa hekima kubwa na busara ya kutosha ili kupata muafaka wa kweli.

Swali ni kwamba wabunge waliochaguliwa na watanzania hawana busara za kutosha kujadili maswala la kitaifa???? na nina anapaswa ajadili maswala yetu??

Huu ni muendelezo mwengine wa kubananga demokrasia.
 
Halafu hawajui ni kwanini tunawachukia wabunge wa ccm.
 
Teh teh teh kwa hiyo wabunge hawana busara na hawawezi kujadili mambo nyeti ila ya "HOVYO HOVYO"..kaazi kweli kweli....
 
always huyu mama ananichefua kuliko maelezo... natamani angejua
 
Back
Top Bottom