Makinda ampinga Zitto hoja ya Kumuondoa Waziri Mkuu

January Makamba msaliti wa vijana wa Tanzania. Hafai na hatusaidia vijana. Analinda maslai ya baba yake.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida spika makinda ameilinda serikali ya magamba kwa kutupilia mbali hoja ya Zito Kabwe na amesema haina mashiko na imepitwa na wakati kikanuni kwani bunge linatarajiwa kuvunjwa kabla ya siku Kumi na nne.
 
wana jf spika makinda amekataa hoja ya kumpiga chini pm. sababu hapa imekuwa ni siku zinatakiwa ziwe si chini ya 14, sasa leo wameshapata sahii zote lakini siku 14 hawawez kufikisha bunge linaisha j3 na hvyo tutakuwa na siku 4 tu.
nawasilisha
 
Spika:
Katiba Ibara ya 51(2) Waziri Mkuu anateuliwa na Raisi na kuthibitishwa na Wabunge walio wengi, atakuwa kiongozi mkuu wa Serekali Bungeni, Mawaziri watawajibika kwa Waziriku Mkuu,

53a(3) Hoja ya kutokuwa na Imani na waziri Mkuu haitapitishwa kama,

a. haitaungwa mkono na 20% ya Wabunge.
b. Sikuhike abla ya siku inayotakiwa kuwakilishwa Bungeni.
c. Spika aridhike,
d. .... (ona thread nyingine)

Hitimisho:

SPIKA:

1. Msingi ni kwamba sahihi zipelekwe siku 14 (within)
2. Sijapata hoja rasmi,
3. Siku zilizobaki hazitoshi,
4. Labda bunge lijalo na zile siku 14
5. Kinachoendelea ni batili,

Utaratibu alioutangaza Mh. Zitto Hauwezekani.
 
Ni spika anaasema kwa mujibu wa katiba.hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inatakiwa imfikie spika siku 14 kabla.
Sasa sijui....nawakilisha.
 
Ina maana Mh. Zitto hakulijua hili??

Makamba is a bit like his father. Wabunge wote wanajua kuwa bunge limebakiza siku 3 kufunga kikao hiki, lkn mwezi wa 7 bunge lina kikao kingine na jambo hili litajadiliwa, tatizo ni nini?

Hon. Mnyika MP., alikaa na hoja yake mpk kikao cha bunge kilichofuata kwani ilikufa? Kwanza kwa maoni yangu huu ndio wakati mzuri kwa Pinda kujitetea kwa kuwawajibisha wanaotuhumiwa kabla ya kikao cha bunge cha bajeti mwezi wa 7.
 
duuh hoja ya zitto ishapigwa chini duuh

haijapigwa chini per se coz mpaka bunge lijalo kigezo cha siku 14 kitakuwa kimetimia, swala liliopigwa chini ni kuwasilisha hoja iyo jumatatu kwani zitakuwa zimetimia siku 4 tu, hivyo basi nafasi ya hoja hii bado ipo hai.
 
alichofanya spika kiko nje ya katiba na kanuni za bunge? naomba kujuzwa.ila kama kanuni na katiba zinasema hivyo basi basi sidhani kama ametetea serikali ila kafanya kazi yake.
 
Huyu spika ni Bogus kabisa. Anachokifanya Zitto ni kukusanya sahihi ili apate sahihi za 20% ya wabunge za kuandika taarifa ya maandishi kwa spika. Sasa analolifanya Zitto ni mwanzo wa mchakato na Spika hana haki ya kusema kama mchakato huo ni batili mpaka pale atakapoletewa taarifa ya maandishi na kujiridhisha kuwa haijakamilisha matakwa ya katiba kama yalivyoainishwa.

Spika hahitajiki kujua kinachoendelea alichotakiwa kusema ni kuwa yeye hajapata taarifa ya maandishi na hayupo katika nafasi ya kutamka kuhusu mchakato ila kama kuna mtu anafanya hivyo anafanya kwa mujibu wa katiba na yeye atakuwa katika nafasi ya kutoa uamuzi wake pale tu atakapoletewa taarifa ya maandishi na kujiridhisha kama inakidhi matakwa ya katiba.
 
Sasa nimeamini ccm ni genge la wanyang'anyi, njia ya muongo ni fupi sana leo nimedhibitisha kwa macho yangu

kumbe jazba zote zile zilikuwa geresha, puuuuuuuumbavu zao.

Hawa ccm walijihami kwakuonyesha wanahasira ili cdm wasiwafunike, kumbe wanazidi kufunikwa.

Usitishie kuj.... Kama unaugonjwa wa kuhara
 
Back
Top Bottom