Makinda ampinga Zitto hoja ya Kumuondoa Waziri Mkuu

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
531
225
Wadau naomba ufafanuzi kwa mwenye kujua sheria za VOTE OF NO CONFIDENCE! Sheria inahitaji asilimia ngapi ya wabunge ili kuleta hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu! Kura pia inahitaji asilimia ngapi ya Wabunge ili PM apigwe chini? Kura 70 ni asilimia ngapi ya wabunge?

Kanuni zinasema baada ya kupata #Sahihi70 unahitaji kutoa notice ya siku 14 ili hoja ijadiliwe. Bunge ends in 3 days. #PublicityStunt? - By January Makamba @JMakamba

Wana JF
Tafadhali, someni kwa makini na muelewe kanuni za bunge zinasemaje kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu na taratibu zake

SEHEMU YA KUMI NA TATU (ya kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007)
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU

133.-(1) Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa
Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
kwa mujibu wa Ibara ya 53A ya Katiba.

(2) Hoja yoyote ya kutaka kupitisha Azimio la kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu haitatolewa Bungeni endapo:-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya
Waziri Mkuu yaliyoainishwa katika Ibara ya 52 ya
Katiba;

(b) hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(c) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa; au

(d) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa
kuipitisha.

(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa
na Bunge isipokuwa tu kama:-

(a) taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na
kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua
asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa
kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne
kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;

(b) Spika ataridhika kuwa masharti ya Katiba kwa
ajili ya kuleta hoja hiyo yametimizwa.

(4) Hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya
Katiba, itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na
itaamuliwa kwa kura za siri.

(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo
inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

(6) Endapo hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa
na Bunge kwa kupigiwa kura na Wabunge walio wengi, Spika
atawasilisha Azimio hilo kwa Rais na mapema iwezekanavyo na
kwa vyovyote vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha
Azimio hilo, Waziri mkuu atajiuzulu na Rais atamteua mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu


Spika:
Katiba Ibara ya 51(2) Waziri Mkuu anateuliwa na Raisi na kuthibitishwa na Wabunge walio wengi, atakuwa kiongozi mkuu wa Serekali Bungeni, Mawaziri watawajibika kwa Waziriku Mkuu,

53a(3) Hoja ya kutokuwa na Imani na waziri Mkuu haitapitishwa kama,

a. haitaungwa mkono na 20% ya Wabunge.
b. Sikuhike abla ya siku inayotakiwa kuwakilishwa Bungeni.
c. Spika aridhike,
d. .... (ona thread nyingine)

Hitimisho:

SPIKA:

1. Msingi ni kwamba sahihi zipelekwe siku 14 (within)
2. Sijapata hoja rasmi,
3. Siku zilizobaki hazitoshi,
4. Labda bunge lijalo na zile siku 14
5. Kinachoendelea ni batili,

Utaratibu alioutangaza Mh. Zitto Hauwezekani.

 
Saini za watu 70 ni kwa ajili ya kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na pm, wabunge wakijadili na kupitisha hoja kwa 50% na kura 1 ya zaidi, then pm anapigwa chini.
 
Mh jamani mtoto wa mkulima anahali ngumu kiongozi wangu!
 
Mbunge anatakiwa kuwasilisha hoja ya kudhamiria kutoa hoja ya kutokuwa na imani na PM akiwa ameambatanisha na saini za asilimia 20 ya wabunge wote. Iwapo mjadala ukifika bungeni utaamriwa kwa kura za siri na inabidi ipatikane zaidi ya asilimia 50 ya kura za wabunge wote ili kumwondoa PM
 
hivi hizo kura 70 bado mpaka sasa?

mambo ya % tutayajadili baadaye
 
Mi namshangaa Pinda kwa kweli. Ya nini fedheha????

Mzee kamalizie palizi maindi yameshachanua. Sijui unataka nini mpaka sasa. Au wataka kulia kama ulivyolia eti biashara yenu ya Albino? hapa Kamanda Zitto kakamata korodani Waziri mkuu macho yanamtoka tu hapa.

Go home bwoy.
 
Wanajf,

Kwa muda siku mbili tumeshuhudia wabunge wakiongea kwa uchungu na wengine kufikia hata kuwanyooshea vidole mawaziri na kuwaita wezi na ndio wanaolitafuna taifa. Mwananchi yeyote mzalendo atakuwa ameguswa vilivyo kwa jinsi wawasilisha hoja walivyokuwa wakiwasilisha hoja zao.

Wakati wa kufunga mjada wa majadiliano wa kamati za kudumu za mahesabu, Mhe Zitto Kabwe alisema kama mawaziri waliotajwa kutokuwawajibisha walio chini yao hawajawajibika basi wabunge wazalendo wenye uchungu na maslahi ya taifa hili watie saini na zikifika 70 plus 1 watapeleka hoja mbele ya meza ya spika ili kiongozi wa serikali bungeni awajibishwe kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae.

Nimeona hii hoja ya Mhe January Makamba nimeishiwa na nguvu na kuona yote ninayoyaona ni ndoto.
 

Attachments

  • January.jpg
    January.jpg
    46.9 KB · Views: 423
yafaa nini basi kugonga meza kwa hasira na kuongea mpaka mate yatoke kwa hawa CCM MP's. Huyu ni MakambaKanuni zinasema baada ya kupata #Sahihi70 unahitaji kutoa notice ya siku 14 ili hoja ijadiliwe. Bunge ends in 3 days. #PublicityStunt?
 
Wanajf,

Kwa muda siku mbili tumeshuhudia wabunge wakiongea kwa uchungu na wengine kufikia hata kuwanyooshea vidole mawaziri na kuwaita wezi na ndio wanaolitafuna taifa. Mwananchi yeyote mzalendo atakuwa ameguswa vilivyo kwa jinsi wawasilisha hoja walivyokuwa wakiwasilisha hoja zao.

Wakati wa kufunga mjada wa majadiliano wa kamati za kudumu za mahesabu, Mhe Zitto Kabwe alisema kama mawaziri waliotajwa kutokuwawajibisha walio chini yao hawajawajibika basi wabunge wazalendo wenye uchungu na maslahi ya taifa hili watie saini na zikifika 70 plus 1 watapeleka hoja mbele ya meza ya spika ili kiongozi wa serikali bungeni awajibishwe kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae.

Nimeona hii hoja ya Mhe January Makamba nimeishiwa na nguvu na kuona yote ninayoyaona ni ndoto.

Unajua mkuu mimi nilivyoelewa ni kwamba hoja itapelekwa kwa spika lakini si lazima ijadiliwe kikao hiki, na ishu kubwa sidhani kama Pinda atadondoshwa maana wana CCM watamlinda, kwa hiyo hapa kinachotafutwa ni kwamba Hoja ya kutokumuhitaji Waziri mkuu ilishawahi kufika mikononi mwa Spika hii ni pia ni aibu kubwa kwa Waziri Mkuu
 
kwa wale wataalamu wa mambo ya sheria na kanuni za bunge, naomba kuelimishwa,
Hivi zito anaweza kuwasilisha hoja j3, then baada ya wiki 2 (siku 14) spika akitisha kikao cha bunge kwa ajili ya kupiga kura za siri? inawezekana?
 
Back
Top Bottom