Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama uliangalia bunge jana utakuwa ulimsikiliza vizuri Zitto na kuelewa mchakato anaotaka kuufanya.
Katika kuwasilisha hoja ya kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, mwenye hoja anatakiwa kwanza awe na sahihi sabinni za wabunge, na ndicho alichosisitiza Zitto jana kwamba wabunge wote wenye uchungu na nchi hii kuanzia leo wajitokeze kusaini ili sasa kuanzia hapo hoja hiyo ipate kufikishwa kwa spika kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji.
Nadhani kuna watu wanajaribu kuipotosha hoja hii as if Zitto akishapata saini sabini tu, basi waziri mkuu ana step down. Tujitahidi kujiepusha na upotoshaji unaofanywa hapa, bila shaka kwa malengo maalum.
Hata alichoandika january makamba kwenye twitter yake ni katika kujipapatua tu, iko wazi kabisa kwamba Zitto ni mtu maarufu sana, hawezi kuhitaji public stunt katika hili, bali amewatega waosha vinywa wote wa ccm ili watanzania wajue ni mbunge yupi mzalendo na ni yupi domokaya.