Makinda ampinga Zitto hoja ya Kumuondoa Waziri Mkuu

mtoto wa mkulima wacha yamkute ni mgumu kufanya maamuzi kila kitu ameguswa chukua hatua basi hawezi
 
Hivi inamaana Mjanja Zitto wa Kabwe halijui hili au? Kaazi kweli kweli. Tuanakurupuka sana kutaka umaarufu

Lkn wewe ndio umekurupuka kutoa maamuzi, saini 70 zikipatikana ni aibu/stress tosha kwa Pinda na Serikali ya CCM. Ok, sorry CCM hawana AIBU/carefree hivyo hawatakosa usingizi kwa hilo.
 
Bandugu! inabidi tuwe na upembuzi wa haraka kuhusiana na lengo la Mh, Zitto na tafsiri zilizotolewa na Mh, Makamba.
Kwanza ieleweke wazi kuwa Wote walitambua uwepo wa Kanuni husika ila kinachoendelea kwa sasa ni mkakati wa CCM kuwapumbaza wananchi kwani hatua ya kuitisha kikao cha wabunge wa CCM kililenga kwanza kuwadhibiti ili wasisaini karatasi husika kwa lengo la kuhakikisha idadi inayotakiwa haifikii kwa kuamini CUF wengi wao wangesuasua.

Baada ya kubaini uwezekano wa kupatikana hizo sahihi 70 ni Mkubwa ndipo wameibuka na mkakati huo wa eti kupata #Sahihi70 unahitaji kutoa notice ya siku 14 ili hoja ijadiliwe. Bunge ends in 3 days. #PublicityStunt? Sasa tujiulize kama suala hilo la kikanuni lilieleweka kwa nini CCM waliweweseka kiasi cha hadi Katibu Mkuu Kiongozi kufika Dodoma? Si wangeacha tu halafu baadaye wakaja na maelezo kuwa hilo ni batili?

Tumshukuru Zitto na washirika wao kwa hatua waliyoichukua ya kutoyumbishwa na kuendelea na harakati za kukusanya na kupatikana saini zinazohitajika kwani ni dhahiri sasa Bomu analo mkononi ni muda tu unasubiriwa wa Mawaziri husika Wajiuzuru au alilipue kwa Kuwasilisha hoja hiyo ya Kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu.

Kiuongozi hatua ya kupatikana kwa sahihi hizo za kutishiwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye ndiyo uliopelekea CCM kukomaliana ili Mawaziri husika wawajibike kumuepusha Waziri Mkuu na aibu, Hata hivyo binafsi ninaona pamoja na Mawaziri husika kujiuzuru ni kama Waziri Mkuu ameshachafuka vile! Hivyo ni busara zake kupima badala ya kusubilia kupimwa kama kweli anauwezo wa kufanya watanzania tumuamini katika kuwasimamia hao mawaziri wa Serikali.

Hiyo ndiyo adha ya kufanya Kazi na mtu (JK) anayetaka kila kitu aonekane yeye ndiyo mzuri, anabusara, anawapenda watu nk. ilhali hatua hiyo mara nyingi inadhoofisha utendaji wa watu wengine hasa wanaotegemea maamuzi kutoka kwake.
 
Sltn watanzania tuandamane nchi nzima hadi bungeni kama wasipowajibika,Makinda si Mungu na sheria c wazazi,hatma yao sasa
 
Matatizo yangu ni kipengele 133 (3) (b) kwamba kama spika ATARIDHIKA kuwa masharti ya katiba kwa ajili ya kuleta hoja hiyo yametimizwa.
Hivi hapa kigezo ni nini, maana spika anaweza kusema tu masharti hayakitimizwa hiyo hoja inakufa.
Mtoa hoja akitaka kukata rufaan juu ya mabavu ya spika kanuni ipi itumke.
 
Back
Top Bottom