Makato ya ushuru wa kuweka au kutoa fedha benki na kutuma na kupokea fedha kielektroniki waanza

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Serikali imekata tozo kwenye miamala yote kuanzia tarehe moja July mwaka huu... Kama akaunti yako haina salio kwa sasa tozo litakatwa punde akaunti ikiwekewa fedha.
IMG-20220818-WA0041.jpg
 
Serikali imekata tozo kwenye miamala yote kuanzia tarehe moja July mwaka huu... Kama akaunti yako haina salio kwa sasa tozo litakatwa punde akaunti ikiwekewa fedha. View attachment 2327409
Ni shetani pekee au mwendawazimu anaeweza kutetea huu upunguani wa phd isiyotumia busara na hekima.

Hatuwezi kuendelea kwa kutumia elimu ya darasani pekee, busara na hekima inatakiwa katika 75% ya maamuzi yoyote hasa yanayogusa jamii, huyu waziri mpuuzi anayeamka ns tozo bila kujali kunakotozwa tayari kushakatwa kodi nyingine ni sawa na kichaa, mtu kama huyu mwenye phd ambayo haina busara na hekima bora aende akafundishe vyuoni
 
Zilipenda baraza la Mawaziri mkuu
 
Kwani hayo maamuzi ya kuanzisha hizo tozo anayatunga na kuridhia peke yake ?
 
Wala. Wananchi wamelala kama makondoo wanabishana kuhusu Simba na Yanga. Wangekuwa wakali unadhani wangethubutu kufanya huu ujinga? Mama haharibikiwi wala hatishiki, acha makondoo yakatwe fedha ili kina Kinana wapate fedha za kutumbua!
Haya yote chanzo Ni magufuli, fedha zote aliingiza kwenye mamiradi yake, wenzie wamekuta Nchi haina akiba ya fedha
 
Serikali imekata tozo kwenye miamala yote kuanzia tarehe moja July mwaka huu... Kama akaunti yako haina salio kwa sasa tozo litakatwa punde akaunti ikiwekewa fedha. View attachment 2327409
Ndo maana Bp, visukari , havikai nao mbali nao , KWa kweli to be honest SSH hastahili hata kufika 2025, nchi imemshinda Sana na inazidi kumshinda, waziri wake fedha ndo hakuna kitu hivi ni uchumi GANI, unatoa KWa mkono wa kushoto na unaiba KWa mkono wa kulia?

Mtumishi aliongezewa elfu 20, huku mshahara wake nje codi anayokatwa, ikikumbana na tozo kwenye miamala, Luku, Sasa tena kwenye bank,huku mafuta juu, na KILA kitu juu,

Umepunguza ruzuku ya mbolea, huku mafuta na KILA kitu kiko juu, jumlisha tozo, maushuru ya kijinga huko mawilayani, unaongeza na tozo kwenye benk

Nawbia Sasa watu wameishafika kwenye peak mnacho kutaka KWa Sasa ni maandamano yasiyo kuwa na kikomo ,binafsi nayaona YAKO karibu na hamtahamini
 
Haya yote chanzo Ni magufuli, fedha zote aliingiza kwenye mamiradi yake, wenzie wamekuta Nchi haina akiba ya fedha
Panua ubongo wako kidogo. Tanzania tatizo kubwa siyo fedha ila ni matumizi. Matumizi yasiyo ya lazima na ufisadi ndiyo tanuru linalochoma fedha zetu.

Kabla hawajaingia kwenye kumtoza mwananchi kodi mara mbili au hata tatu kwa kitu kile kile ingebidi kwanza wapunguze utitiri wa viongozi wasio na umuhimu wowote na malipo ya anasa.

1. Wabunge wapunguzwe kabisa kwani wengi hawana kazi yoyote. Watu kama ma-DC, maafisa mipango etc waondolewe na ngazi za wilaya na mikoa wabaki viongozi wachache. Mawaziri na makatibu wapunguzwe kabisa.

Ununuzi wa magari ufanywe kulingana na hali halisi na siyo kununua magari ya kifahari. Viongozi wasafiri kwenye madaraja ya kawaida na kulala kwenye hotel za kawaida isipokuwa wale viongozi wakuu.

Vikao vya kupiga fedha ambavyo Magufuli alikuwa amevipunguza kabisa vimerudi kwa kasi na ufisadi kwa ujumla na pia ukwepaji kodi. Njia za kupata fedha ziko nyingi na siyo kukimbilia kuwakamua wananchi.
 
Back
Top Bottom