MAKASA: Bi Mkubwa (Mama mkwe)

MAKASA: Bi Mkubwa (Mama mkwe)

BI MKUBWA
( sehemu ya 17 )

Endeleaa..............

Wakati nambeba mume wangu nimtoe kwenye kile chumba nikashangaa mlango unafungwa, nikapigwa na butwaa baada ya kumuona bimkubwa akiwa amesimama mbele ya mlango wa kutokea chumbani.....

"Kilichowaleta huku ni nini?
"Mama tusamehe.
"Niwasamehe nini?
"Hatuta ingia tena mama
"Sawa, lakini lazima nitoe adhabu
"Mama tusamehe
"Nishawasamehe, yaan Leo ilibidi muishie humu humu ila nitawapa adhabu ndogo tu.
"Mama usifanye hivyo, kumbuka sisi ni wanao
"Sina watoto ambao hawanisikilizi
"Mama.......
"Sikiliza wewe mwanamke chagua kimoja, kati yako wewe na mume wako mmoja awe bubu na mwingine awe kipofu,
"Mamaa hiyo adhabu in kubwa sana
"Sikiliza nyinyi usiku huu mtalala humu ndani na hawa wasichana nitakapo ludi alfajiri nataka unipe jibu kamili, sawa?
"Mama mbona utatupa mateso
"Kama hutaki nitawaweka humu ndani kama hawa wasichana
"Mama basi.

Bimkubwa akachukua usinga wake akamchapa nao mume wangu usoni, mume wangu nikamwona anaamka na kwenda kukaa pamoja na wale wasichana, akanichapa na mimi nikajikuta naamka na kwenda kujiunga na wale wasichana na mume wangu.

Bimkubwa na yule kijana wakavua nguo mbele yetu na kuvaa nguo zao nyeusi wakajifunga viremba vyeupe kichwani na kujivesha matunguli shingoni,

Wakatoka nje kupitia kona moja ya kile chumba, tulibaki mle ndani tukiwa watu ambao kama hatujitambui japokuwa mlango ulikuwepo hatukuwa na uwezo wa kufungua kutokana na kuwa na hakili zisizokuwa na uwezo wa kutambua nini cha kufanya.

Bimkubwa na yule kijana walimpitia mchungaji na kumfuta yule afande, walipofika Kwa afande walijadili ni adhabu gani ya kumpatia yule afande...

"Mchungaji hawa tuwape adhabu gani?
"Chagua wewe mama maana wewe ndio muhusika mkuu
"Wewe in MTU wangu wa kalibu unaweza kuchagua adhabu ya kuwapa.
"Alafu nimekumbuka kitu mama.
"Nini hicho mchungaji?
"Natarajia kupanua kanisa langu
"Kwahiyo?
"Hawa nataka niwaweke Kule mbele ya madhabau kuniongezea nguvu wakati wa kufanya maombi
"Lakini ilibidi wawe ndugu zako
"Ni ndugu zangu hawa
"Kivipi?
"Waumini wangu pale kanisani
"Sawa, lakini hiyo kazi mpaka utakapo anza kujenga hilo kanisa
"Ndio
"Ina maana Leo wasipate adhabu yoyote
"Lazima wapate?
"Adhabu gani tuwape?
"Leo tusiludi Kwa ndege,
"Una maanisha nini?
"Hawa leo tuwafanye farasi watuludishe hadi nyumbani
"Sawa haina shida
"Alafu nimekumbuka kitu?
"Kipi hicho?
"Leo najisikia hamu sana ya kufanya mapenz
"Sawa mchungaji na mimi Leo nafanya na huyo huyo afande wewe fanya na mke wake
"Na huyu kijana uliyekuja nae
"Akamchukue house girl wao.

Baada ya kukubaliana wakamchukua afande na mke wake na kuwatoa sebuleni, yule kijana nae akamchukua house girl wa afande na kumtoa sebuleni wote watatu waliwekwa sebuleni.

Mchungaji akachukua kitambaa chekundu na kuchovyo kwenye dawa akawapaka wote watatu sehemu zao za siri ( afande, mke wa afande na house girl wao ),

baada ya kumaliza kuwapaka dawa mchunga akanza kuvua nguo zake zote akabaki kama alivyozaliwa bimkubwa nae akafanya hivyo mwisho kijana nae akafanya hivyo,

Mchungaji akaanza kufanya mambo na mke wa afande bimkubwa na yule kijana nayo wakafuata, wote wakawa wanafanya shughuli hiyo wakiwa wanaimba imba nyimbo zao za kichawi,

Yule kijana akawa wa kwanza kumaliza shughuli bimkubwa nae akafuata mchungaji akawa wa mwisho kumaliza shughuli, baada ya kumaliza shughuli bimkubwa akasema.....

"Bimkubwa: Kijana mludishe huyu house girl chumbani kwake na uje uwachukue hwa uwaludishe chumbani kwao.
"Mchungaji: Hapana hawa Leo tuwaache hivi hivi wapate adabu
"Bimkubwa: sawa haina shida aibu yao hiyo kesho
"Mchungaji: Basi sisi tuondoke tukapumzike
"Bimkubwa: sawa, alafu mchungaji lile swala la kuwafanya wawe farasi vipi?
"Mchungaji: Kweli kabisa nilitaka kusahau

Baada ya kukumbuka swala hilo mchungaji akachukua dawa kwenye kichupa akaanza kuwanywesha afande , mke wake pamoja na house girl wao,

Baada ya kuwanyweshe ile dawa dakika kama moja wote wakawa kama farasi wakawapanda na kutoka nao, walipofika kwa mchungaji wakashuka mchungaji akawashauli wapande ungo waondoke yeye atawabadili wawe katika hali yao ya kawaida.

Bimkubwa na yule kijana wakapanda ungo na kuondoka, baada ya bimkubwa na yule kijana kuondoka mchungaji akawachukua ( afande, mke wa afande na house girl wao ) na kuwasogeza sehemu ya mbali na nyumbani kwake akawanyweshwa ile dawa baada ya dakika moja wote wakawa katika hali zao za kawaida ila wakiwa watupu, aliwalaza pembezoni mwa barabara na yeye akaondoka.

Bimkubwa na yule kijana walipofika nyumbani Kwa mwanae waliingia na kuwakuta kama walivyowaacha....

"Mama sasa hawa tuwafanyeje maana wamejua siri kubwa sana
"Kama nilivyosema mmoja awe kipofu mwingine bubu
"Hapana mimi naona hili swala tungewashilikisha na wezetu
"Wenzetu wakina nani?
"Kule mahande wakina mzee kipesani
"Sawa hill swala tutawashilikisha na hawa itabidi wakae humu hadi kesho tutakapomaliza kikao na mzee kipesani.

Hatimaye mda ulisonga mbele na kukakucha, asubuhi kulipo pambazuka watu waliokuwa wanapita maeneo ya karibu na kanisa waliwashuudia afande mke wake na house girl wao wakiwa wamelala kandokando ya barabara wakiwa uchi.

Watu walizidi kuongezeka kadri mda ulivyokuwa unazidi kwenda, walijalibu kuwaamsha lakini hawakuweza kufanikiwa kuamka

ITAENDELEA......
Mkuu mbona huleti mwendelezo wa hii simulizi?...Umetukatili sana
 
BI MKUBWA
( sehemu ya 14 )

Endeleaa.................

Majira ya SAA tano bimkubwa akakata lile paja na kumpa yule kijana apeleke kwa yule afande, kijana aliwasili Kwa yule afande akamkuta mke wa yule afande akampa lle nyama.
"Shikamo
"Marahaba, hujambo
"Sijambo
"Vipi kaka unasemaje
"Afande kanituma nilete hii nyama
"Sawa kaka, Asante
"Sawa kwahery

Baada ya kukabizi nyama akaludi Kwa bimkubwa, kile chumba ambacho bimkubwa alimwambia mwanae asifungue ndio kikawa chumba cha kulala bimkubwa na yule kijana, na walikuwa wanatumia chumba hicho kwa siri bila mwanae kujua.

Baada ya yule kijana kuwasili kwa bimkubwa baada ya maongezi kidogo bimkubwa akakumbuka kuwa ile nyama haipikwi na ili ipikwe na iive lazima uweke dawa.

Basi bimkubwa na yule kijana wakajiandaa kwa ajili ya kwenda kwa afande kama walivyomuhaidi usiku.

Mke wa afande baada ya kupewa ile nyama akakata na kuanza kuipika , chakushangza toka alivyo anza kupika majira ya SAA sita kasoro hadi inatimia SAA saba kasoro haikuweza kuiva.

Bimkubwa na yule kijana walimaliza kujiandaa majira ya SAA saba na dakika kumi waliwasili Kwa afande. Baadaya kufika kwa afande, mke wa afande akawakaribisha wakaingia hadi ndani,

Baada ya kusalimiana akawauliza maswali kidogo kutaka kuwatambua bimkibwa akajieleza yeye nishangazi take afande, basi akaangalia kinywaji kwenye friji akakosa ikabidi awaage wageni wake kidogo kwenda dukani kununua vinywaji.

Wakati mke wa afande anaenda kununua kinywaji bimkubwa akawa amepata mda wa kwenda jikoni kuweka ile dawa kwenye nyama ili iive.

Mke wa afande alipoludi kutoka dukani akawapa vinywaji wageni wake na kwenda jikoni kuangalia mboga yake, alipofunua mfuniko aliona mboga sasa ipo tayari imeiva, akaiunga alipomaliza akapika ugalia akawawekea wageni wake na yeye akachukua ugali wake akakaa pembeni wakaanza kula.

Mda huo wakati wanaanza kula mlango uliogwa akaingia afande akastaajabu kuwaona wale wachawi walio mhaidi kuwa wageni wake wapo ndani. Kutokana na kujua kilichotokea usiku ilibidi avunge kama anawajua.

Akawasalimia baada ya salamu mke wake akamwandalia chakula basi wote wakawa wanakula, mke wa afande wakati anakula alishangaa sana kila akimega nyama kipande cha nyama kilikuwa hakiishi, lakini hakusema kwa mtu kutokana na kuogopa wale wageni

Afande nae alishanga kuona ile nyama ikiwa na mafuta mengi kuliko kawaida na kila alipokuwa akikata nyama ilikuwa haiishi ikabidi amuulize mke wake.

"Mke wangu
"Abee
"Hii nyama wakati unanunua hukuona mafuta in mengi, kwanini hukuchagua nyingine?
"Hii nyama ni ile uliyomtuma Huyu kijana alete asubuhi.
"Lini?
"Leo asubuhi, au umesahau?
"Mbona sikumbuki.

Yule kijana akadakia mada mzee hii nyama in ile ya asubuhi uliyonipa Mimi nilete, bimkubwa nae hakuwa mzembe akamfinyia jicho afande, ndipo afande akaelewa somo kuwa hii nyama sio kabisa.

Baada ya kuona hivyo afande akaacha kula na kutoka pale na kwenda chumbani kwake, akamtumia SMS mke wake ""usile hiyo nyama"" mke wake akashangaa akatoka pale na kumfuta mme wake chumbani alipofika alikumkuta Mme wake kajiinamia.

"Mme wangu vipi?
"Matatizo mke wangu
"Matatizo gani mme wangu
"Hii nyama tunayokula
"Imefanyaje ?
"Sijui hata nianzie wapi
"Mme wangu mbona unanitisha
"Hii nyama hujahisi chochote mke wangu?
"Mme wangu hilonimeliona nakula nyama ila haiishi
"Ni tatizo kubwa mke wangu
"Hebu niambia ni nini?
"Hii nyama nahisi ni nyama ya binadamu
"Mme wangu ebu niambie kinachoendelea

Afande ilibid ampe story Kwa ufupi kuhusu wale wageni kuanzia mwanzo hadi mwisho, baada ya afande kumpa mke wake story ya wale wageni mke wa afande akachukua bastola ya mme wake na kutoka kule chumbani na kuwafuta wale wageni sebuleni.

Alipofika sebuleni hakufanijiwa kuwaona wale wageni, alipo angalia chakula walichokuwa wanakula kipo ila hakuna mboga alipo angalia chakula chake aligundua kuwa chakula kipo ila mboga haipo.

Akaenda moja kwa moja jikoni pia hakuikuita mboga aliyokuwa kapika akaludi kwa mme wake.....
"Mme wangu wageni hawapo
"Kama nilivyokuambia mke wangu
"Kama ulivyoniambia nini?
"Hawa wageni ni waajabu
"Kwanini hukuniambia wakati unafika , wakati ulijua wageni sio wa kawaida
"Ningeanzaje mke wangu?
"Ungeanza kama ulivyoanza saizi.
"Mke wangu sio laisi hivyo kama unavyofikilia.
"Alafu sasa ile nyama walioleta wameondoka nayo.
"Bora hata wameondoka nayo
"Siamini kama leo ninekula nyama ya binadamu mwenzangu.
"Mke wangu naomba hili lililotokea hapa leo liwe siri yetu
"Kwanini?
"Itakuwa aibu sana,
"Aibu ya nini?
"Watu wakijua tumekula nyama ya mtu
"Mme wangu tusiposema wataendelea na Kwa wengine bora tuseme wengine wasalimiki
"Mke wangu tunaanzaje kusema kwa watu tumekula nyama ya binadamu,
"Mme wangu hiyo siri yako leo imetufanya kula hii nyama, unadhani ungesema mapema kilichokukuta usiku Mimi ningeweza kuwapokea hawa wageni, ningejihami kupokea hawa wageni
"Sawa mke wangu, ila hiyo kazi ya kuanza kusema umekula nyama ya binadamu sio laisi kama unavyofikilia.

Kumbe wakati wanazungumza hayo bimkubwa na yule kijana walikuwa hawajaondoka walikuwa pale ndani lakini walikuwa katika hali ya uchawi ambayo wao walikuwa hawajawaona.

ITAENDELEA......
Utamu umekata.....naona huku umejaziajazia tu vistori ili iwe ndefu labda!
 
Back
Top Bottom