MAKASA: Bi Mkubwa (Mama mkwe)

MAKASA: Bi Mkubwa (Mama mkwe)

BI MKUBWA
( sehemu ya 8 )

Endeleaa..................

“Nenda chumbani kampake dawa ya kumzindua yule baba mwenye nyumba, aliamuru kiongozi wa wachawi. Haraka sana nilifumba macho huku nikiyafunua
kidogo, kwa kuwa kulikuwa na giza hakuweza kuona kuwa naona.
Nilimuona yule mchawi akifungua kibuyu kidogo akanywa ile dawa na kututemea,

Baada ya kututemea ile dawa akatoka na kuwafuata wenzake balazani wakapanda ndege yao na kuondoka mama mkwe aliingia chumbani kwake na kujipumzisha akitafakari yajayo.

Hatimaye kulikucha niiamshwa na kelele ya vijana watoto pamoja na wazee walikuwa Nyumba ya jirani wakishuhudia mchawi aliye nasa .

Asubuhi nyumba ya jirani ilikuwa imejaa watu ambao walikuwa wakipiga kelele.
“Mchawi, mchawi kanasa ndani.
"Mtoeni tumwone huyooo
"Na lazima apigwe aseme ukeweli

Umati ulikuwa mkubwa sana na kelele zikawa nyingi, mume wangu naye aliamshwa na zile kelele,

"Mke wangu vipi?
"Safi, umeamaje wewe?
“Mhhhh… johari, mwili unauma sana,
“Pole sana, kwani ulifanya kazi gani?”
“Hakuna, vipi mbona kuna kelele huko nje?
“Nasikia kuna mchawi kanasa katika nyumba ya huyo shoga yangu.
“Shoga yako yupi?
“Yule aliyekuja hapa nyumbani na kusema atatupeleka kwa baba yake akatufanyie zindiko.”
“Acha utani,
"Kweli tena
"kwake ameshikwa mchawi?”
“Siyo ameshikwa. Amenasa!”
“Unatania?
“Husikii kelele huko nje?
"Ndio nasikia.
"Njoo hapa dirishani uone.
“Kwani hapo dirishani huyo mchawi aliyenasa anaonekana?”
“Hapana …uje uone watu walivyojazana nje ya madirisha.

Mume wangu alifika dirishani ili na yeye aweze kuchungulia Nyumba ya jirani
“Kwa kuwa yule mama mwenye nyumba ni rafiki yako nenda kamuone,
"Ila naogopa sana mume wangu
"Unaogopa nini?
"Kuona wachawi unazani mchezo.
"Si kuna watu kibao kule?
"Ndio
"Nenda basi kashuhudie uje unipe habari
"Sawa basi ngoja niende.

Nilijitanda kitenge changu na kwenda kujionea japokuwa picha nzima nilikuwa naijua kutokana na kusikia waliyokuwa wakiyafanya wachawi usiku hapa nyumbani kwangu.

Nilifika pale na yule shoga yangu aliponiona aliniita pembeni akaanza kunisumulia:
“Unajua nini Johari?
"Niambie shoga yangu.
" kama nilivyokuambia jana kuwa mtaa huu Luna wachawi na nyumbani kwako kuna wachawi wanakuja kila siku usiku huku wengine wakitumia ungo.
"Kumbe ni kweli yaani nilikuwa sikuamini
"Umeamini sasa?
"Asilimia mia moja.
"Lakini nilikuambia?
“Nakumbuka uliniambia hivyo tena mbele ya mume wangu,
"Leo wameingia cha kike sasa.
"Chakike haswaa
"Sasa huyo aliyenaswa ni nani?
“Shoga namjua basi?
"Si umemwona au?
"Ndio, Labda wewe ukimuona unaweza kumfahamu.

Jirani yangu huyo alinipenyeza licha ya kuwepo watu wengi, walimpisha kwa kuwa walikuwa wanajua kuwa yeye ndiye mama mwenye nyumba, huku nami nikijitahidi kumfuata.

Tulifika ndani ya nyumba na kumkuta mchawi akiwa bado ameganda katikati ya sebule huku watu wakiwa wamejazana kwenye madirisha ili
waweze kumuona, alikuwa amevaa kaniki kiunoni.

Niliingiwa na hofu kubwa hasa niliposikia watu wengine wakisema mchawi yule achomwe moto.
Lakini hata mume wa rafiki yangu niliona ana wasiwasi baada ya kusikia maneno hayo kwani alianza kuhangaika kupigia simu kwa watu ambao mimi sikuwajua.

"Hellow
"Hellow
"Shikamoo mzee,,
"Marahaba, mnaendeleaje huko?
"Salama , ila kuna tatizo.
"Tatizo gani teni?
"Kuna mchawi kanasa hapa nyumbani
"Sawa basis nafika sasa hivi.
“Mzee naomba uje haraka wasije kumdhuru huyu mchawi,

Baada ya kumwona yule mchawi ilibidi nitoke niende nyumbani, nikachomoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwangu, njiani nikakutana na mume wangu ambaye alikuwa amevaa bukta, fulana na
makubazi miguuni.

"Mume wangu wapi tena?
"Naenda Kwann Hugo mchawi.
"Si ulisema Mimi niende nine kukupa habari?
"Nimegundua habari nzuri uisome mwenyewe.
"Makubwa!!!!
"Nenda basis nyumbani mke wangu?
"Sawa, ila uyo mchaei ni nona mme wangu
"Kwanini?
"Ukimwangalua tu anakutemea mate, na mate yake yanaruka kama nyoka.
"Basi siendi, twende nyumbani mke wangu.
"Hahaà kumbe mwoga nakutania bwana hatemi mate.
"Acha masihara wewe mchawi si mchezo.
"Sawa unaogoa wakati pale nyumbani unaishi nae.
"Nani mchawi palenyumvani naenda kumfanya bucha sasa hivi,
"Kwani wewe humjui ?
"Nitajie nani?
"Si wewe mme wangu.
"Acha masihara wewe mambo hayo sio ya masihara,
"Sawa yaishe mume wangu!!
“Ehee, huyo aliyenaswa unamfahamu?” "simjui,
"Yupo sehemu gani?
"Yupo tu pale sebuleni anang’aang’aa macho.
“Sasa wenye nyumba wanasemaje?”
“Baba mwenye nyumba nimemuona akihangaika kupiga simu kwa watu ambao siwajui,
“Amepiga simu polisi?”
“Sijui.”
“Lakini akishafika huyo mtu akamnasua, huyo mchawi atapita wapi?
"Kwanini?
" Ni wazi atauawa palepale nje ya nyumba yake ni vema akaita kwanza polisi.
“Hilo naona hajakumbuka, amepaniki, ni vema ukawahi kumpa ushauri huo.”
“Hapana turudi sote tukatoe ushauri kwa pamoja.

Nilikubaliana na mume wangu hivyo nikageuza njia na kuanza kuelekea tena kwa jirani yetu. Tulipofika watu ndiyo walizidi, bahati nzuri tulikuta kuna waandishi wa habari wa Gazeti la Uwazi
ambao baada ya kutuona walitukabili.

“Mama samahani, mimi ni dulla?
"Kwahiyo
"huyu ni bosi wangu anaitwa chid ni mwaandishi wa gazeti la Uwazi, tumeambiwa wewe ulikuwa
ndani, unamfahamu huyo mchawi aliyenaswa?”
“Kaka mimi huyo aliyenaswa kweli nimemuona lakini simfahamu kwa jina wala sijawahi kumuona hapa mtaani.”
“Lakini watu wanasema wewe na mama mwenye nyumba ni marafiki,
"Kwahiyo kama marafiki?
"je, umeonana naye na mmeshauriana nini?
"Nimeonana nae lakini mini sio msemaji wa Nyumba za watu mtafuteni mwenye nyumba,
"Sawa, basi Nina swali La mwisho Dada angu.
"Uliza,
"Tunaomba basi hata jina tu LA huyo mchawi?
"simfahamu kwa jina wala kwa sura,
"Ina maana ni mgeni?
"sijawahi kumuona hapa mtaani.
"Na kinachoendelea hapa Kwa sasa ni nini?
"Tumeshauriana kwamba waitwe polisi."
"Polisi wataweza kumnasua mchawi?
"Polisi ni Kwaajili ya ulizi tu si unaona watu walivyojaa hapa wanaweza wakampiga.
"Sawa asante sana dada,
"Sawa kwaherini
"Samahani tena kidogo Dada ,
"Vipi tena?
"Sijui unaitwa nani ?
"Siwezi kutaja jina, samahani kwa hilo.

Niliwaacha waandishi hao na kwenda kwa mama mwenye nyumba ambaye alikuwa na mumewe nami na mume wangu.

Mume wangu alipewa jukumu la kuita polisi naye akapiga namba 112 na polisi wakaitikia.
"Umepiga simu polisi station, naongea na nani?
"Mervin charz
" tukusaidie nini?
"Hapa Mtaa wa Pwiriri, kuna mchawi amenaswa.
"Polisi hatuhusiki na mambo ya kishirikina.
"Ndio, lakini sasa kanasa hapa?
"Sawa, sasa mnataka msaada gani kwa sababu sisi polisi hatuwezi kumnasua!"
"Sio kumnasua
"Ila nini sasa kama kanasa?
"Hapana msaada wetu ni kwamba tunataka mje kulinda usalama wake na wa mali pia kwa kuwa watu wanatishia kumlipua kwa mafuta ya taa.
"Kwahiyo akilipuliwa ?
" Sasa wakifanya hivyo akiwa ndani ni wazi kwamba vitu vingi pamoja na nyumba vitatekelea, tafadhalini njooni,
"Nimekuelewa, tunakuja,

Nje ya nyumba fujo zilizidi na wakati tunatafakari nini cha kufanya, aliingia mtu mmoja ambaye alikuwa ni mzee wa makamo.
"Baba karibu sana.
"Asante sana,
"Shikamoo mzee,
"Marahaba vipi hapa salama?
"Salama sio sana , kama unavyo ona
"Sawa, haina shida.
"Baba Umekuja na teksi?
"Ndiyo," alijibu mzee huyo.
"Sawa. Shilingi ngapi anataka?"
"Nimeshamlipa," alijibu mzee.

Jirani zangu huyu ni baba yangu mzazi na ndiye aliyenitengenezea nyumba hii ili wachawi wasiingie, akatutambulisha.

"Shikamoo baba, tulijishitukia mimi na mume wangu tukimuamkia kwa pamoja kama vile kuna mtu alituamuru kufanya hivyo.
"Marahaba, marahaba
"Mzee hawa ni jirani zangu, tunaishi nao vizuri. Ilikuwa tuwalete kwako Jumapili ijayo ili kuwazindikia nyumba yao," alisema baba mwenye nyumba.
"Bado hamjachelewa, walete tu. Tumalize kwanza hili lililonileta," akasema.
"Hapana baba tusubiri kwanza polisi.
"Polisi wanini?
"Si unaona jinsi fujo zilivyotanda hapo nje?

Kabla hajajibu lolote tulisikia ving'ora vikilia nikajua kwamba hao ni polisi wanakuja. Hata hivyo, nilishanga kusikia ving'ora vya magari mawili nikajiuliza kwa nini wamekuja na magari mawili kana kwamba kuna fujo tayari zimefumuka.

Nilichungulia dirishani nikaona kumbe walikuwa wameongozana na gari la Kikosi cha Zima Moto. Watu waliokuwa wamejazana mlangoni akiwemo mama mkwe wangu walipisha na kuweka njia bila hata kuamrishwa baada ya kumuona mkaguzi wa polisi yaani Inspekta Kijo akija ndani pamoja na maofisa wengine wa polisi.

Aliingia akiwa na askari sita wote wakiwa na silaha za kivita, Semi Machine Gun (SMG).
"Nani mhusika mkuu hapa,
"Muhusika wa nini inspekta?
"Namaanisha mwenye nyumba?
"Ni mimi hapa, hawa ni jirani zangu na huyu ni mke wangu na huyu ni baba mkwe wangu.
"Na huyu handsome ndio.....
"Huyu ndiye mchawi aliyenasa hapa?"
"Ndiyo, anaonekana tu
"Sisi sijui tungetoka nje tuwapishe muongee, alisema johari
"Jirani bakini tu haina shida
"Ina maana hawezi kujisogeza kabisa?" aliuliza swali yule inspekta wa polisi, swali ambalo halikuwa na jibu kwa sababu alimuona na kama angeweza kujisogeza tusingesema alinasa.
"Ndio Inspekta
"Sasa mtamnasuaje?
"Yupo mtu wa kumnasua,
"Nani huyo mtaalamu?
"huyu baba mkwe wangu,
"Kumbe mtaalamu yupa hapahapa?
"Ndio, tulikuwa tunawangoja nyinyi mje kwa usalama wa huyu mchawi.
"Mmefanya vizuri sana
" Tulifikiri kama tungemnasua bila nyinyi kuwepo, watu wenye hasira wangeweza kumuua."
"Kwani anaitwa nani huyu?

Swali hilo LA Inspekta lilianzisha mada mpywa na ngumu kuliko tulivyofikilia nikajua sasa hapa mama mkwe anaenda kuumbuka.
"Kwa kweli hatumjui inspekta
"Hata jina kumbe hamlijui?
"Ndio inspekta
"Kwani sio mwenyeji wa hapa
"Ndio, sio mwenyeji

Baba mkwe akadakia
"Basi kama sio mwenyeji wa hapa wanangu kuoni makini atakuwa ana MTU wake nyuma huyu,
"Kweli kabisa baba angu, alijibu mama kibela
"Basi Mimi simtoi hapa mpaka amtaje huyo mwenyeji wake
"Baba bora tu umtoe atakaa mpaka saa ngapi?
"Mwanangu kumnasa huyu ujue umeanzisha vita mpywa na wachawi
"Ni kweli kabisa mama kibela, niliongeza chumvi
"Sawa wewe kijana naomba utoe majibu nitakayokuliza, kwanza uniambie unaitwa nani unatoka wapi na mwenyeji wako nani, ili nikunasue.

Itaendelea..............
 
Jamaaaa badoooo, si umesema ziko nyingi au unasubirii mtunzi atungeeee?
 
BI MKUBWA
( sehemu ya 7 )

Endeleaa................

"Hii hali inatisha sana, unasikia majogoo wanawika, hiyo inaashiria kuwa kunakucha na watu wataanza kutoka mitaani hasa wale wanaenda kuchukua bidhaa sokoni," alisikika mama mkwe akizungumza.

"Sasa tufanye nini?
"Inatakiwa akili ya ziada kuamua cha kufanya,
"Au hapa tulipo kuna mtu ambaye ana dawa ya kumfanya mtu asionekane?" alikuwa ni mama mkwe akiwatupia swali wenzake.

"Hilo ungelikumbuka wakati mkuu anaenda nyumbani kwake kwa sababu kama hiyo dawa ipo, tungeitumia kama tutashindwa kumng'atua kwa leo pale aliponasa mwenzetu," alidakia mwanamke mwingine ambaye pia sikumfahamu kwa jina wala kumtambua kwa sauti yake.

Wakati wakiwaza hayo yule kiongozi mkuu wa wachawi akawa ameingia na tunguri zake nne zenye shanga. Kiongozi alipofika tu hakushangaa akaanza kuwapanga vijana wake.
"Vipi hapa?
"Safi tu kiongozi.
"Naomba mjiandae tuanze kazi.
"sawa mkuu
"Akafu kuna jambo la muhimu kingine
"Jambo gani hilo tena
"Naomba mwanaume mmoja akamvue yule jogari zile nguo tubaweza kujisahau akaamka ikawa kasheshe nyingine.
"Sawa,ngoja mimi niende,
"Ngoja wewe anaend Huyu, unataka kukimbia kazi sio
"Hapana kiongozi
"Sawa kazi ianze Mara moja

Baada ya maagizo ya mkuu wao yule kijana akaja kunivua zile nguo wakati wengine wanajiandaa kurusha makombora kumnasua mwenzao

Yule kijana akanivua nguo na kunifuta Yale madawa waliyonipaka Kwa kutumia kitambaa cha rangi nyeupe na dawa amvayo alikuwa anachovya ili kutoa Yale mafuta.

Walijitahidi kufanya shughuli zao za kishirikina kwa kurusha ‘makombora’ yao ya kichawi huku wakisema kwamba likitua kwenye nyumba ile ya jirani litasambaratisha dawa zilizomfanya
mwenzao anase.

Wakaanza kurusha makomba, radi ambazo zilikuwa zinasikika huko nje ni hatari, kama ingekuwa radi ya mvua basi mvua hiyo ingekuwa ya kiama, baada ya mda kidogo wote wakaingia tena ndani.

"Jamani hii shughuli imekuwa pevu
"Sijawahi kuona kwakweli.
"Sasa kama kiongozi unasema ujawahi kuona na sisi tusemeji?
"Shika adabu yako wewe mkuu mkuu nini?

Nilisikia wakibishana wengine wakidai yule mkuu wao kakosea kuchanganya unga wa dawa walizotumia kutengeneza makombora hayo.

Kwa kuwa kikao chao walikuwa wakifanyia kwenye sebule yetu, nilisikia wakisema dawa walizotia kwenye pembe ya nyati hazikutimia. Sikujua ni dawa gani walizotia kwenye ile pembe
lakini nilisikia mtu akiambiwa apulize kuelekea kwenye ile nyumba ya jirani.

“Nimepuliza tayari na kombora limekwenda lakini sasa itabidi watu
waende kumalizia kule kule kwenye nyumba, ”alisema yule mtu aliyekuwa akionekana kama kiongozi wao.

Baadaye alitumwa mama mkwe na kijana mwingine kwenda kwenye ile nyumba ya jirani ili kumalizia
dawa nyingine za kumnasua.
Wachawi wengine wote walikaa kwenye kochi pale sebuleni kana kwamba walikuwa ni wageni wetu
rasmi ambao walisubiri chakula au hotuba ya kukaribishwa na mwenye nyumba.

Walikuwa wakinong’ona maneno ambayo mimi nilikuwa siyasikii lakini nahisi walikuwa wakijadili ugumu au kazi waliyonayo ya kumnasua mwenzao
ambaye alinasa kwenye nyumba ya jirani.

Nilijitahidi kumtingisha mume wangu ili kuona kama ataamka lakini ilishindikana kwani alikuwa akiendelea kukoroma kutokana na dawa walizomnusisha, Wakati naendelea kumtingisha
mume wangu huku nikiwaza nini cha kufanya ili kumzindua nilisikia kishindo cha mlango wa barazani kufunguliwa.

Nilijikusanya pale kitandani na nikaenda
kuchungulia nikashuhudia mama mkwe akiwa na yule kijana wakiwa wamesimama mbele ya wachawi wenzao.

“Imeshindikana?
"Ndio kiongozi, alisema mama mkwe.
“Inamaana ile dawa haikufanya kazi?”
“Ndiyo maana yake.
"Au mmekosea mashart?
"Hapana, Tumejitahidi kupuliza ile
pembe nyingine kwa kupitia dirishani, ameshindwakunasuka.
"Kumbe anaoneka hata ukiw nje?
"Ndio taa hawaja zima
"Wewe mwenyewe anafanya jitaha gani?
"Atafanya nini mkuu, yani pale nikama vile miguu imepakwa supagluu.
"Duuu sijawahi kuona hii

Wakati wanazungumza hayo muda nao ulikuwa siyo rafiki yao kwani majogoo yalianza kuwika kuashiria kuwa kunakucha iikuwa in saa kumi na moja kasoro.

“Sasa jamani tumeshaumbuka, tufanye nini? ”alihoji mama mkwe.
“Hakuna cha kufanya, tungoje jua lichomoze tuone mwenye nyumba atafanya nini,” alisema kiongozi
"Mkuu mda umeenda sana ungewaruhusu watu waende makwao sasa?
“Sawa Cha kufanya kila mmoja arudi
nyumbani lakini ni muhimu kuwahi eneo la tukio ili kuhakikisha tunamlinda mwenzetu.
“Tutamlindaje wakati amenasa na tumejaribu kumnasua tumeshindwa?
“Kumnasua kweli tumeshindwa lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa tupo pale kwa sababu siku hizi kuna mtindo mbaya sana wa kuua watu.
“Umesema kweli, wote tuwe pale,
“Unajua tukiwa wote pale tutazuia watu wasimpige au kumchoma moto.
"Kweli kabisa Mkuu upo sahihi
"Ni hatari sana kama tutamuacha peke yake.
“Lakini mimi sitaweza kwenda pale, nitakuwa nimeumbuka sana,” ilikuwa ni sauti ya mama mkwe.
"Kwani majirani wanajua wewe ni mchawi?
"Hapana, ila Kwa dawa za hawa nikienda watawez kunigundua bure.
“Sawa, wewe usiende lakini hutaeleweka vibaya?
“Hapana, Nikiamka tu nitajifanya nina malaria.

Wote walikubaliana kwamba asubuhi wawe eneo la tukio na watu wakijazana basi nao wawe kama mashuhuda lengo kuu ni kuzuia mauaji kwa
mwenzao.

“Nenda chumbani kampake dawa ya kumzindua yule baba mwenye nyumba, aliamuru kiongozi wa wachawi. Haraka sana nilifumba macho huku nikiyafunua
kidogo, kwa kuwa kulikuwa na giza hakuweza kuona kuwa naona.
Nilimuona yule mchawi akifungua kibuyu kidogo akanywa ile dawa na kututemea,

Itaendelea.......
Kiongozi tuma zote aseeee
 
BI MKUBWA
( sehemu ya 9 )

Endeleaa...................

Baba mkwe akadakia
"Basi kama sio mwenyeji wa hapa wanangu kuoni makini atakuwa ana MTU wake nyuma huyu,
"Kweli kabisa baba angu, alijibu mama kibela
"Basi Mimi simtoi hapa mpaka amtaje huyo mwenyeji wake
"Baba bora tu umtoe atakaa mpaka saa ngapi?
"Mwanangu kumnasa huyu ujue umeanzisha vita mpywa na wachawi
"Ni kweli kabisa mama kibela, niliongeza chumvi
"Sawa wewe kijana naomba utoe majibu nitakayokuliza, kwanza uniambie unaitwa nani unatoka wapi na mwenyeji wako nani, ili nikunasu
"Baba Mimi naona kama hayo maswali tungemuuliza wakati umemnasua.
"Kwanini mwanangu
" Ameteseka sana, kuanzia usiku hadi SAA NNE hii hajatoa hata mguu toka alivyosimama.
"Lakini mwanangu kumbuka kuwa nayeye alikuwa na nia hiyo hiyo ya kuwatesa.
" Sawa baba lakini tutumie utu hata kidogo tu ni binadamu Huyu.
"Sawa mwanangu sababu nyumba ni yenu na tatizo ni lenu nitafanya hivyo.

Basi baba mkwe wa baba mwenye nyumba alichukuwa dawa
nyeusi na kuichanganya kwenye maji kisha akamnywesha akachukua dawa nyingine kwenye koti lake na kumwambia atafune baada yakutafuna ile dawa akachua ile aliyompa anywe na kummwagia yule mchawi aliyenasa miguuni
mara tatu, akamsukuma na akapepesuka, ikawa tayari amemnasua.

Baada ya kumnasua wale watu waliokuwa wanachungulia madilishani walianzisha Fujo yakutaka kumpiga yule mchawi
‘Ua mchawi huyoooo, chinja, piga maweee,”
zilikuwa ni kelele za wananchi waliokuwa wamejazana nje ya nyumba.

Polisi wanne wenye silaha ilibidi watoke nje na kuwatawanya watu wenye hasira. Hata hivyo, bado watu walikuwa wabishi kuondoka ndipo askari mmoja akalipua bomu la machozi.

Moshi ulifumuka na kujaa nje lakini mwingine uliingia ndani na kutufanya nasi kububujikwa na machozi kutokana na muwasho wa moshi huo ulipoingia machoni.

Wakati watu wanakimbia huku na huko kutokanaa na woga wa kishindo cha mlio wa bunduki na moshi wenye pilipili, polisi walitumia mwanya huo kumtoa ndani mchawi na kumuingiza katika gari lao, ‘Difenda’.

Walimchukuwa na baba mkwe wa jirani yetu na mmiliki wa nyumba na mkewe. Mimi nilishauriwa na mume wangu nimsindikize jirani yangu kwa kuwa ni shoga yangu.

Tulifika polisi na kukuta makamanda na askari wengine wa vyeo vya chini wakitusubiri kwa kuwa habari ile ilisambaa kwa kasi kubwa mji mzima. Wote tuliingizwa katika chumba kimoja pale polisi na tukaketi kwenye viti. Yule mchawi aliambiwa asimame , akaanza kuhojiwa.

“Wewe mchawi unaitwa nani?.
“Naitwa fred Libaya ,”
“Unaishi wapi?”
“ mahande.”
“Dini yako?”
“Mpagani.”
“Hebu eleza ulifikafikaje katika nyumba uliyokutwa na ilikuwaje ukakutwa ndani katika nyumba ya watu?
“Mimi nilialikwa na wachawi wenzangu pale Kijiji cha mahande na wakaniambia kuwa tuna safari ya mbali.
"Eheee...endelea
" Tuliambiwa tutasafiri kwa ungo. Wakasema mwenyeji wetu huko ni bibi wa Ajigale.
"Bibi ajigile mnamfahamu jamani
" wote tukaitikia "" ndio""
"Sawa..endeleaaaa
“Mimi sikumjua huyo bibi na hakika nilikuwa kama
bendera fuata upepo…

Yule askari polisi alitugeukia sisi.
“Jamani ile nyumba ndio anayoishi bibi wa Ajigale?”
“Hapana, ile in nyumba ni yangu Mimi
“Sasa wewe fredi mbona unataka kunichanganya? Nakuuliza uliingiaje pale uliponasa, unasema mambo ya nyumba nyingine, ohoo, usinichezee,” alifoka.
“Hapana afande, nakuja hukohuko. Nimeanza mwanzo ili unielewe.
“sawa Endelea.”
“Lengo la safari ilikuwa kwenda kufanya uchawi
katika nyumba ya akina bibi Ajigale. Sasa tuliondoka kwa ungo kutoka mahande na baada ya kufika kwa bibi wa Ajigale, Lengo letu lilikuwa ni kumsafisha mkwe wake,
" Kumsafisha una maanisha nini?
"Kumuunganisha yaani na yeyey awe mchawi.
" Jamani huyo mkwe wake mnamjua?
"Ndio, ndio huyu hapa ni jirani yetu.
" Sawa endeleeea,
"Sasa wakati tunataka kuanzasafari ya kuekekea makaburi bibi ajigile alitoa mashitaka kuwa mama wa nyumba niliyoingia alitangaza kuwa huwa anatuona kila tunapofika pale usiku.”
“Kwani huwa mnafika mara kwa mara?”
“Ndiyo, huwa tunafika mara nyingi.”
“Mkifika huwa mnafanya nini?”
“Hakuna cha maana tunachokifanya. Mara nyingi inakuwa kwa ajili ya kufanya nao mapenzi, na huwa tunamchukuwa mwenye nyumba na kwenda naye makaburini.”
“Makaburini kufanya nini?”
“Si ndiyo uchawi wenyewe?
" Ndio, mnaenda naye kufanya nini?
"Tunaenda kumchezea maana kwa kufanya hivyo mama yake
yaani bibi wa Ajigale hufurahi sana.
“Anafurahia kitendo hicho cha kumchukuwa mwanaye?”
“Ndiyo na anasema anataka amfundishe uchawi ili akifa arithi
mkoba wake wa kichawi.
" Sasa ikaweje mkataka kumuunganisha na mkwe wake.
"Huyo tulitaka kumuunganisha sababu alishawahi kumwona bibi ajigile akiwa anawanga.
" Na kwanini huwa mnafanya nao mapenzi?
"Sababu bibi ajigile anataka mwanae asifanikiwe kupata mtoto.
" Kwahiyo mchawi ukifanya naye mapenzi tu huzai tena?
"Hapana kama unataka MTU asizae, baada ya kumaliza kufanya nae mapenzi tunachukua zile mbegu zake tunaenda kuzika kwenye kaburi LA mtoto Mdogo ambaye alifariji kabla ya kutimiza week moja.
" Sawa, sasa mlitaka pia kumuunganisha mtoto wa bibi ajigile?
"Ndio,
“Angekataa je mngefanyaje?”
“Hawezi kukataa,
" kwanini ?
"Anapumbazwa kwanza kwa dawa za kichawi kabla ya kuambiwa uamuzi wa mama yake, angezidi kukataa, hakungekuwa na namna nyingine zaidi ya kumfanya kitoweo.
“Sawa sasa tuludi kwenye hoja ya msingi,, wewe kwenye nyumba ya huyu mama ulienda kufanya mini?
“Ilikuwa tunaenda kumnyamazisha,
" kwanini mkamyamazishe?
" kwa sababu Bibi wa Ajigale, alisema kuwa Huyo mama jirani alikuja nyumbani kwa watoto wake na kuwa ambia kuwa atawapeleka kwa mtaalamu wake ambaye in baba yake ili awazindike sasa angewazindija INA maana sisi tusingeweza kumkarisha mtoto wake kuwa mchawi.
"Sasa nyinyi mlitaka kumnyamazisha kivipi?
" kwanza tulitaka tumpandikize uzezete?
"Baada ya hapo?
" Baada ya hapo tulitaka tumuue?
"Mngewezaje kumuua wakati sio ndugu yenu huwa mnaua bila mpangilio sio?
" Hapana kila MTU anamuua ndugu yake?
"Sasa nyie huyu ndugu yenu?
" Hapana , huyu tungemuua kwasababu ametoa siri yetu.
"Kwahiyo wewe ndio MTU wa kuwatia watu uzezeta?
" Ndio , hata hapa nikiachiwa nikitumwa kwako nije kukutia uzezeta nafika, sababu hiyo nj amri kama wewe unavyotii amri ya mkubwa wako wa kazi,
"Sawa bwana ila naomba usifanye ikawa kweli namimi hapa nakuhoji nimeagizwa tu na wakubwa wangu.
" Si ndio maana nimesema na Mimi naagizwa na wakubwa.
"Saw a tuishie hapo hapo.

Hatimaye polisi na mchawi wakamalizana.
Mahojiano hayo yalimtia hasira mume wa shoga yangu na nilikuwa namuon alikuwa akitetemeka kwa hasira pale alipokuwa ameketi. Naamini ingekuwa pale siyo kituo cha polisi, angemrukia na makubwa yangetokea.

Baada ya polisi kumaliza kumuhoji baba mkwe akashika kasi na yeye akaanza na maswali aliyonayo :
“Nilikusikia ukisema kwamba baada ya kumtia uzezeta mwanangu mlitaka pia kumuua?
" Ndio mzeee
"Nani kakwambia Mimi mzee
" Samahani
"Samahani ya nini yakutaka kumuua mwanangu?
" Baba punguza hasira,,alisema mama kibela
"Sawa , mlitaka kumuua kwa kutumia silaha gani?”
“Tulikuwa na mabomu ya kichawi,
" Hayo mabomu ya kichawi mlinunua wapi?
"Bibi ajigile huwa anauwezo mkubwa tu na anatenge mwenyewe
" kwahiyo mlitaka kumtupia hilo bomu?”
“Hapana,
"Ila...?
"huwa ni la kutegea mlango wa chumbani.
" Kwahiyo Leo mngemtia uzezeta na mngeludi tena kuja kutega bomu?
"Ndio hivyo hivyo tulivyokuwa tunafikilia.
" Baada ya kutega Bomu nini kingetokea?
"Kwanza angeanza kuvimba miguu, baada ya siku tatu angeanza kuoza ndani ya mweZi mmoja angekuwa marehemu
" Sasa kama angeoza hiyo nyama mngekulaje?
"Akioza huwa nyama yake hatuli,
" ila mnafanya nini?
"MTU akianza kuoza au akiwa tayari kaoza huwa nyama yake inakamuliwa mafuta yote na yeye anakuwa chakula cha misukule.
" Hayo mafuta mnayokamua nyie yanini?
"Yana kazi nyingi sana .
"Kama IPI ?
" kwanza kwa ajili ya ndege zetu ( ungo ) pia kama mtu tumemuua Hana mafuta ya kutosha tunaongeza hayo
Na kazi kubwa ni kwamba mtu anapotaka kujiungana uchawi huwa yanatumika kumkamilishia taratibu zote za kujiunga na uchawi
" Sawa Mimi nishamaliza , kama kuna LA nyongeza jamani?

Wote tukatikisa kichwa kuashiria hakuna swali lolote, baada ya hapo, Yule afande aliyekuwa akimhoji alimpa karatasi alizo andika maelezo asome kisha kama maelezo yaliyo andikwa amekubaliaba nayo atie sahihi yake.

Baada ya hatua ya kutia sahihi kukamilika, Polisi aligeuka na kutuangalia kwa mara nyingine. Alisimama na kujinyoosha kisha alimuita askari mmoja ambaye hakuwa na cheo chochote, wenyewe huwaita praiveti akamuamuru amchukue
yule mchawi fred libaya akamfungie mahabusu.

Sasa mzee njoo nawe nipate maelezo yako, (akimaanisha baba mwenye nyumba )
"Jamani huyo bibi anayetajwa mnamjua?.
“Ndio nii mama mkwe wake huyu mama,” yule baba
mwenye nyumba jirani yangu akajibu huku akinyoosha kidole kuelekeza kwangu.
“Duh, mama mpo salama hapo kwenu kweli?”
Niliona aibu sikujibu swali hilo kwa sababu ukweli ni kwamba mimi pia nazozana mara kwa mara na mama mkwe wangu kutokana na tabia yake ya kishirikina na hasa alipogundua kuwa kuna mpango wa kwenda kwa mzee wa jirani yangu akatupe dawa ya zindiko ili tuizindike nyumba yetu baada
ya wao kugundua kuwa wachawi walikuwa na kawaida ya kuja usiku kutuwangia.

Baba mwenye nyumba baada ya kuhojiwa jina lake
na kabila pamoja na dini yake, mahojiano na polisi
yalikuwa hivi:
“Mzee uliamua uwapeleke jirani zako kwa baba yako akafanye zindiko kwenye nyumba yao, kwa nini ulivutika kufanya hivyo?”
“Nilivutika kwa sababu niliona jirani zangu wanateswa na wachawi kila siku usiku.”
“Wewe ulikuwa ukiwaona hao wachawi?
"Ndio, Nilikuwa nawaona na mara nyingi tulikuwa tunaamshana na mke wangu na kushuhudia vituko
vyao bila wao kutuona. Tulipoona wamezidisha vituko tukawa tunaacha taa zetu bila kuzima ili waingiwe na woga, lakini wakawa hawajali.”
“Ukafanyaje?”
“Nilimtuma mke wangu huyu akawaambie na alipowaambia mama mkwe wake huyu mama alikuwepo ndipo usiku wa leo walipoamua kutufata kama mchawi fred alivyokueleza. Hawakujua kuwa nyumba yetu imezindikwa na siyo
rahisi mchawi kuingia na kuleta madhara. Hayo
ndiyo maelezo yangu.”

Mzee mwenye nyumba huyo alisainishwa na polisi maelezo hayo. Yule askari alisema tusubiri kidogo kwani anaenda kwa mkuu wa kituo kumpa taarifa na kupata maelekezo yatakayofuata.

Hakuchelewa alirudi akasema:
“Tumekubaliana kwamba bibi naye akakamatwe, ahojiwe, kwasababu fred libaya amemhusisha na kumtaja bibi ajigile Mara kadhaa, kwamba ametamka kuwa aliingia ndani kwenu kwa ajili ya kuandaa kifo cha mtu Hivyo, mzee kaingie kwenye gari ‘difenda’ la polisi ukatuoneshe nyumba ya bibi ajigile tukamtie mbaroni.”

Itaendeleaaa......
 
BI MKUBWA
( sehemu ya 10 )

Endeleaa......................

Hakuchelewa alirudi akasema:
“Tumekubaliana kwamba bibi naye akakamatwe, ahojiwe, kwasababu fred libaya amemhusisha na kumtaja bibi ajigile Mara kadhaa, kwamba ametamka kuwa aliingia ndani kwenu kwa ajili ya kuandaa kifo cha mtu Hivyo, mzee kaingie kwenye gari ‘difenda’ la polisi ukatuoneshe nyumba ya bibi ajigile tukamtie mbaroni.

Baada ya polisi kumwamuli Mzee mwenye nyumba aingia kwenye gari aliingia, lakini mimi pia kwa kuwa majirani walisema ndiye ninayeishi naye niliambiwa niwemo kwenye msafara.

"Mama na wewe ingia tafadhali?
"Hapana Mimi nitafika na huyu jirani yangu.
"Wewe si ndio unaishi nae ?
"Ndio.
"Lazima uingia ukatusaidie kumpata.
"Lakini mume wangu ambaye ndiye mama yake yupo nyumbani,
"Kwahiyo kama yupo nyumbani?
"Nendeni tu mtamkuta, atawasaidia kumpata.

Nilijitetea kukwepa kwenda kumkamata mama mkwe wangu maana nilijua akiachiwa lazima gogo litaangukia kwangu , kwasababu alishajua kuwa na Mimi najua siri yake.

Lakini polisi walizidi kunisisitiza ili twende wote nyumbani,
"Hapana mama, mambo ya wanaume huyajui,
"Mambo gani?
"Tunaweza tukakuta huyo mumeo hayupo.
"Sawa basi twende.
"Mama twende tu, tutarudi wote, wewe usiwe na wasiwasi
"Basi kama ni hivyo tuondoke na mkewe?
"Sawa, twendeni kwani gari hili lina nafasi kubwa.

Mwendo wa gari haukuwa mrefu kwa sababu dereva aliwasha king'ora, hivyo magari barabarani yakawa yanatupisha.

Tulifika nyumbani tukamkuta mume wangu akiwa ameketi nje ya nyumba na mama mkwe alikuwa ndani. Mume wangu macho yalimtoka kutokana na kusikia king'ora cha gari la polisi likiwa na askari wawili likisimama mbele ya nyumba yetu.

"Mzee habari za hapa? askari kiongozi wa msafara alimsalimia mume wangu.
"Nzuri jamani,
"Sijui nyinyi hari zenu?
"Sisi tupo salama kabisa.
"Bibi ajigile tumemkuta?
"kuna nini?
"Tumekuja kumchukuwa mama yako.
"Mama?
"Ndiyo, mama ako?
"Mnampeleka wapi?
"Bila shaka unaona hii ni difender?
"Ndio.
"Defender huwa inapaki wapi?
"Kituo cha polisi?
"Basi itakapo paki ndio anatakiwa ashuke?
"Kwani kuna shida gani?
"Shida ataijua polisi.
"Ni vyema mkanitarifu mimi ndio mwanae.
"Kama wewe ni mwanae uje kituo cha polisi kusikiliza shitaka lake.
"Basi mniambia hata kichwa cha habari tu nijue ndugu zangu.
"Sawa tutakuambia, mama ako anahusika tuhuma za kutaka kuua?
"Kuua tena mzee kama huyu?
"Ndio.
"Anataka kumuua nani?
"Ni tuhuma za kishirikina?
"Mama angu mbona sio mchawi?
"Kuna tukio la leo mtu kunaswa ndani ya nyumba ya mtu.
"Ndio kweli kabisa lakini hajanasa mama angu.
"Ndio hajanaswa yeye lakini amehusika,
"Kivipi afande, na wakati tukio linatokea alikuwa hapa nyumbani?
"Hapana. Ametajwa na yule mchawi aliyenasa ambaye tunamshikilia kituoni.
"Lakini sijaafiki mama awe Mchawi?
"Kwani mzee huna habari kwamba hapo kwa jirani yako kuna mchawi leo usiku amenaswa?
"Najua na mke wangu nimemuagiza amsindikize shoga yake.
"Sasa huyo mke wakoYupo kwenye gari ile na shoga yake.
"Haiwezekani afande?
"Ndio hivyo, mke wako alijaribu kukataa tusije naye lakini nimemlazimisha na tunaye kwenye gari pamoja na majirani zako.
"Basi. Mwiteni kwanza Huyo mke wang?
"Sawa subili nikuitia.

Polisi akaja kuniita kwenye gari ili nikaongee na Mme wangu ila kutokana na kuona aibu Kwa jirani zangu nikakataa kutoka ndani ya gari, mume wangu akaamua kunifuata.

"Ahaa, kumbe ni kweli?
"Kweni sisi uliona tunatania pale au?
"Hapana.
"Kumbe nini?
'"Tutaongea subilini kwanza niongee na mke wangu.
"Sawa ongea nae
"Mke wangu shuka basi tujadili kabla mama hajachukuliwa,
"Mzee huo sio utaratibu, fanyeni haraka mda sio rafiki.

Baada yamume wangu kunibembeleza sana nikashuka kwenye gari ili niweze kumpa taarifa kidogo zilizotokea huko polisi.

"Ehee huko polisi mambo yalikuwa vipi?
"Yule mchawi kamtaja mama.
"Kamtaja kuhusu nini sasa?
"Kasema walikuwa na mama mkwe lakini yeye ndiye aliyeingia ndani na mama akabaki nje,
"Sawa mke wangu tusiongee sana, tunamsaidiaje saizi huyu mama?
"Hakuna njia,
"Jamani mke wangu mama angu huyu nifanyeje?
"Inabidi tu tumsindikize.
"Mke wangu wewe wakuongea maneno haya?
""Sasa mme wangu MTU yupo hapa ndani ninamfichaje?
"Ni kweli mke wangu basi tuhonga hela?
"Tukishahonga?
"Baadae mama tumpeleke kijijini unajua nitapata aibu sana.
"Unahongaje na majira wapo palepale?
"Tuwape hata ishara.
"Mme wangu mambo ambayo amekufanyia Huyu mama ako ukijua hutatamani hata kumuona.
"Kwanini?
"Ndio nakwambia hivyo, wewe mtoe nje akapate na yeye aibu yake labda ataacha huo ujinga.
"Yaani Johari Leo unamwita manma angu mjinga?
"Usilo lijua ni kama usiku wa giza.

Baada ya malumbano Mimi na mume wangu kumaliza ilitulazimu kumwita mama na kumwambia ukweli japokuwa alikuwa anatusikia tukiwa tuongea kuhusu swala hilo, Tulitoka nje tukiwa na mama, kama ilivyo ada, watu wakajaa tele nje ya nyumba yetu wakitaka kujua kwa nini polisi wamefika tena kwa king'ora.

Watu walizungumza mengi, wengine wakisema mama mkwe ndiye aliyesababisha yule mchawi anase, wengine wakawa wanasema naye aliingia ndani lakini kwa kuwa ni mzima kishirikina, alichomoka na kumuacha yule mchawi kijana akiwa ameng'ang'ana sakafuni.

Lakini wapo waliopatia na kusema kwamba mama mkwe wangu alimsindikiza yule mchawi kuwamaliza wale majirani huku wengine wakimtoa kabisa na kuona kuwa yeye alikwenda kuwaonesha nyumba tu ili mchawi amalize kazi kwa wale jirani.

Mazungumzo hayo watu walikuwa wakiyasema kwa sauti na sisi wote tulikuwa tukiyasikia waziwazi na kumuongezea hofu mama mkwe wangu ambaye alikuwa hajui hasa atakachofanywa polisi.

Nilimuangalia nikamuona anatetemeka kama vile alikuwa anaumwa malaria kali kwani hata kanga ilikuwa inamshinda kuifunga ikawa inaanguka, uzuri ni kwamba ndani alikuwa na sketi refu.

Ilibidi kila wakati nimfuate na kumfunga vizuri kanga yake iliyokuwa ikianguka wakati tunakwenda kupanda gari la polisi.

Mama mkwe aliingizwa kwenye gari nami nikamfuata lakini mume wangu alikuwa akitufuata kwa nyuma akiwa kwenye gari lake. Kama tulivyokuja nyumbani, safari ya kurejea polisi ilikuwa fupi tulifika na kukuta watu kibao wakiwa wanangoja ili wajue kitakachoendelea.

Itaendelea...........
 
BI MKUBWA
( sehemu ya 11 )

Endeleaa................

Mama mkwe aliingizwa kwenye gari nami nikamfuata lakini mume wangu alikuwa akitufuata kwa nyuma akiwa kwenye gari lake. Kama tulivyokuja nyumbani, safari ya kurejea polisi ilikuwa fupi tulifika na kukuta watu kibao wakiwa wanangoja ili wajue kitakachoendelea..

Nje ya kituo cha polisi walikuwepo watu wengi mno kuliko wale tuliowaacha wakati tunaondoka kuelekea nyumbani kumchukua mama.

Habari zilishazagaa kwamba kuna mchawi amenasa kwenye nyumba
moja na amepelekwa polisi. Habili hizo zilisambaa kwa kasi kutokana na wananchi kushangazwa na tukio hilo la kunaswa mchawi

Wakati hayo yanaendelea mkuu wa wachawi nae aliwapa kazi vijana wake wafutilie kila hatua ya tukio hilo linavyoendelea ikiwezekana waweze kuwasaidia wachawi wenzeke wasiweze kuzirika, na kuwaokoa pia.

Mara baada ya gari la polisi kuingia kituoni, watu walilisogelea ili kumuona mchawi, hawakujua kuwa alikwisha ingizwa selo.

“Yupo wapi Huyo mchawi?
"Atakuwa huyu mama.
"Hapana bhana aliyenaswa ni mwanaume.
"Basi atakuwa yue pale wakimwonesha baba mwenye nyumba, zilikuwa ni kelele za watu waliotaka kushuhudia.

Basi sisi moja kwa moja tulingia kituoni na kwenda kukaa kwenye kile chumba cha mahojiano, afande akaingia na kuanza kazi yake.

"Shikamoo mama.
"Ma..ra....haba
"Mama acha wasiwasi Mimi ni polisi na hapa ni kituo cha polisi kwahiyo usiogope kabisa upo sehemu salama.
"Sawa vaba angu!!
"Unaitwa nani?
"Sikujua kimpambe!
"Una umri gani?
"Nina miaka 78!
"Dini yako ?
"Sina Dini ( mpagani )
"Umezaliwa mkoa gani?
"Simiyu
"Sawa, mama unajua kilichokuleta hapa?
"Hapana!!
"Unauhakika?
".......( kimywa )
"Sawa, sasa mama tumekuleta hapa Kwa ajili ya usalama wako tu.
"Usalama wa nini na hapa polisi mwanangu?
"Kuna tuhuma zimeletwa hapa kuwa wewe unanjama ya kutaka kuua?
"Sio kweli, Mimi sina njama yoyote ya kutaka kuua!
"Mama inabidi uongee ukweli ili tujue namna ya kukusaidia.
"Sawa na huo mimi ni ukweli wangu sina njama hiyo.
"Sawa, sasa mama bila shaka hawa mbele yako ni jirani zako na hawa ni wanao?
"Ndio.
"Sasa Leo hii kuna tukio LA kunaswa Kwa mchawi kwa hawa jirani zako?
"Ndio
"Unajua chochote kuhusiana na tukio hili?
"......( kimywa )
"Mama kiufupi ni kwamba mchawi aliye naswa Leo Kwa hawa jirani zako amekutaja wewe kuwa ni mmoja wao katika hili tukio na ndio mwenyeji wake wewe, ni kweli?
"Eheeee
"Eheeee nini, sema kweli au sio kweli?
"Ni kweli
"Vizuri sana, sasa elezea ilikuaje?
“Ni kweli huyu mchawi alikuja nyumbani na wenzake na akataka afanye dawa kwenye nyumba ya huyu jirani, (akinyoosha kidole kuelekea kwa
mwenye nyumba.)

Polisi aliandika na baada ya kuona yupo kimya anasita kuendelea akamhoji:
“Ehee, ikawaje bibi?
“Baadaye tulipofika kwenye nyumba, nilimwambia aingie yeye kwa sababu ndiye aliyekuwa na dawa za kutia ndani ya nyumba ile.
“Kwani dawa zile zilikuwa za nini?
“Dawa za kudhuru.
“Kudhuru nini au nani?
“Dawa za kudhuru watu.
“Kwa nini mlitaka mdhuru watu ambao
hawajawakosea?
“Ilikuwa ni amri ya mkuu wa wachawi.”
“Mkuu wa wachawi?
"Ndio
"Ni nani huyo?
“Anaitwa mzee kipesani.
“Mzee kipesani anaishi wapi?
“Anaishi Kijiji cha mahande.
“Unajua sbabu ya kutaka kuwazuru?
"Ndio
“Tueleze basi.”
“Ni kwamba huyu bwana (alinyoosha mkono kumuelekeza askari aliyekuwa akihoji kwa baba mwenye nyumba ya jirani), mke wake alikuja pale nyumbani, akawakuta mwanangu na mkwe wangu, akasema kuna wachawi wanakuja pale nyumban kila siku.
“Ehee, baada ya kusema hivyo?
“Huyu mama akasema baba yake anajua dawa ya. kinga au zindiko la nyumba, hivyo alimuahidi kwamba angewapeleka.
“Kwa hiyo mzee kipesani alijuaje hayo?
“Ni mimi nilimuambia.
“Na aliposikia hilo akasemaje?
“Ndipo akaamuru kuwa wakawekewe dawa ili wamalizwe wasiweze kuwapeleka hawa kwa baba yao.
"Kwahiyo hiyo ndio sababu kutaka kuwadhNdio
"Ilikuaje mpaka ukaanza kuwahaadithia kwamba hawa jirani wanawaona?
"Nikwamba siku hiyo tulikuwa na kazi ya kumsafisha huyu mke wa mwanangu naye ajiunge na kikundi chetu cha wachawi sasa walikawia kutoka pale Nyumba walikuwa wapo nje kwa mda mrefu kwahiyo nikawatahadhalisha kuwa jirani yetu huwa anaona tunachokifanya ndio mkuu wetu akasema tusitishe kwanza zoezi hili tumshughulikie Huyo jirani Yetu anayetuona.
"Sawa, Huyu mwenzako aliyenasa alisema kwamba mlikuwa wote Kwa Huyu jirani yako ni kweli?
"Ndio
“Wewe mbona hujanasa, uliingia ndani ukatoka salama?
“Hapana, mimi sikuingia, niliishia nje aliingia yule kijana tu,
"Kwanini hukuingia ?
"kazi yangu ilikuwa kuonesha nyumba ya
hawa jirani tu.
“Baada ya hapo ikawaje?”
“Alipoingia ndani tu,
"Ndio..
"akaniambia kuwa hawezi kunyanyua mguu kwenda mbele wala kurudi
nyuma,
"Kwahiyo ulichukua hatua Gani?
"Nilipoona hivyo nilirudi nyumbani kumwambia mzee kipesani.”
“Mzee kipesani baada ya kupata taarifa hizo alifanya nini?”
“Alitoa dawa akasema tukammwagie yule aliyenasa, tulienda lakini hakunasuka.
“Ehee, ikawaje?”
“Zilifanywa kila mbinu kwa kutumia dawa
mbalimbali ili kumnasua lakini zote ziligonga mwamba ndipo wakaamua kuwa aachwe tu maana ilishindikana kumtoa.
“Asubuhi mambo yakawaje?”
“Nilimsikia mkwe wangu huyo hapo akimuamsha mwanangu na kumfahamisha kuwa kuna mchawi kanaswa, kachungulia dirishani na
nikawa nasikia kelele nyingi za watu nikajua mambo yameharibika.

"Sawa, Lakini mama kuna kitu ujatuweka wazi?
"Kitu gani mwanangu?
"Huyu aliyenaswa alisema kwamba alikuwa anakuja kwenu na wenzake kila siku, INA maana kila siku walikuwa wanafika Kwa ajili ya kumsafisha Huyu mkwe wako?
"Hapana
"Sasa ni nini walikuwa wanafuta?
"Kuna Nazi ambayo tulikuwa tunafanya.
"Kazi gani hiyo?
"Nikwamba...........!!
"Mama edelea ni kazi gani hiyo?
"Nikwamba tulikuwa tunamalizia kazi ya msochwaa.
"Msochwaa ni kazi gani?
"Ni kazi ya kumfunga MTU kizazi.
"Sasa ni nani mlikuwa mnamfunga kizazi?
"Huyu mwanangu wa kiume.
"Haaaas mama nilikuwa nimekukosea mini mpaka ukafikia hatua hiyo ( mme wangu aliongea kwa hasira sana.
"Kijana naomba utulie nimalizana nae nyinyi mtayaongea yenu baada ( afande)
"Mama naomba tuendele, sasa kizazi nyinyi mnamfungaje mtu?
"Ni kwamba kama ni mtoto wa kiume lazima alale na mama yake mzazi na kama wa kike lazima alale na baba yake mzazi,
"Kwahiyo ni kwamba ukilala tu na mwanao basi azai tena?
"Hapana
"Sasa inakuaje?
"Ni kwamba lazima ufanye nae mapenzi na ukimaliza kufanya nae mapenzi unachukua ile mbegu yake unaenda kuzika katika kaburi la mtoto mdogo aliyefariki kabla ya kutimiza week moja.
"Kwahiyo mama ushalala na Mimi?
"Kijana naomba uache kuuliza hayo maswali vinginevyo wote nitawatoa nje.

Nilimshuudia mume wangu akimwaga machozi kama mtoto mdogo Siku hiyo baada ya kujua ukweli kwamba ashalala na mama yake mzazi bila yeye mwenyewe kujua.

Polisi aliendelea kumhoji mama mkwe..
"Mama kwanini ulitaka mwanao asizae?
“Sikuwa na lengo lingine isipokuwa nilitaka afundishwe uchawi ili nikifa aweze kurithi mikoba yangu,
"Kwani ukizaa huwezi kuwa mchawi?
"Inawezekana,
"Sawa kwanini wewe mwanao asizae?
"Nilitaka awe na cheo kikubwa. Kwaababu ukiwa na watoto ili uweze kuwa na cheo lazima uue wanao wote ili upandishwe cheo, na kama huna watoto basis usizae ndio maana nikaamua nimtoe kizazi ili asiweze kupata watoto na baadae akawaua.

Baada ya mama mkwe kusema maneno hayo mime wangu aliishiwa kabisa nguvu.
“Mama ina maana ulikuwa unataka unifundishe uchawi mama? alidakia mune wangu.
“Usiingilie mahojiano mzee. Elewa kwamba hapa ni polisi au niwatoe nje ya kituo? Hii ni Mara ya mwisho sasa ukiongea tena nawatoa wote nje.
“Hapana. Nimeshangaa kumsikia mama anasema hayo aliyoyasema wakati mimi sijui chochote kuhusu hilo. Kama hivyo ndivyo mbona hakuniambia lolote baada ya tukio na kabla?
“Mzee tuliza mori,” alisisitiza polisi.
“Au niwatimue wote?

Nilitamani nimnyamazishe mume wangu
kuona kuwa tukitimuliwa, hatutajua mengi zaidi kuhusu kundi lile la wachawi.

“Sasa kwa nini mwanao hujamjulisha kuhusu ujuzi wa uchawi uliotaka arithi?
“Ndiyo maana walikuwa wakija nyumbani wachawi wenzangu ili kumchukuwa na kujaribu
kumpumbaza akili ili baadaye nikimwambia asipinge.
“Kwa hiyo ulijua kuwa ukimuambia angengataa?
“Najua kabisa kuwa kama ningemwaambia akiwa na
akili zake timamu angekataa. Mara nyingi tuna uzoefu ni watu wachache sana ambao wakiambiwa watapewa uchawi wanakubali. Hawa wasomi huwa
hawakubali na zaidi huwa wakali. Hawataki kabisa kusikia habari hiyo.

“Kwani mnapofanya uchawi, mnapata faida gani?
"Swali hilo mama mkwe hakujibu, alimuangalia yule polisi kisha akainamisha kichwa chini.
“Sasa itabidi tuwapeleke mahakamani, mama unasemaje?
“Unataka nifungwe?
"Si ulitaka kuua wewe.
"Mwanangu nikifungwa Utapata faida gani?
“Achana na faida, kwani wewe ulipokuwa ukifanya mambo haya ya ulozi ulikuwa unapata faida gani?

Yule polisi aliyekuwa akimhoji mama mkwe aliandika mambo fulani kwenye jadala ambalo alikuwa analitumia kunakili mahojiano. Alimuangalia mama mkwe kisha mwanaye na akanyanyua mkono wa simu ya mezani.

Nilikuwa karibu naye nikaona anabonyeza namba moja, mbili nne kisha akaiweka sehemu ya kusikilizia
sikioni.
“Mwambie Koplo komba aje ofisini kwangu. Jibu la upande wa pili sikulisikia lakini yeye akajibu.
“Ndiyo, aje amchukue huyu bibi, mwambie achukue ufunguo wa mahabusu.

Nilijua kuwa huyo Koplo komba alikuwa anakuja kwa ajili ya kazi moja, kumchukua mama mkwe na
kwenda kumtupa mahabusu. Mama ni mama, nilimuona mume wangu akitetemeka baada ya yeye kujua kuwa mama yake anakuja kuchukuliwa
na kwenda kufungiwa mahabusu.

Moyoni nilikuwa na furaha sana kuona sheria inaanza kufuata mkondo wake. Nilikuwa nawaza kama wangefanikiwa kumfanya mume wangu mchawi na kumrithisha mikoba ya kichawi mambo
yangekuwaje.

Niliamini kuwa kuwekwa mahabusu lile litakuwa fundisho kwake na wote ambao watasikia habari ile kupitia vyombo
vya habari.

Wakati nawaza hayo, yule Koplo Beti akawa ameshafika.
“Jambo afande?” akasalimia huku akipiga guu chini na kutoa saluti kwa mkuu wake wa kazi.
“Mchukue huyu bibi, kamfungie lokapu mpaka nitakapotoa maelekezo mengine.
“Haya bibi inuka, songa mbele,” aliamuru yule askari wa kike.

Mama mkwe kwanza alionekana dhahiri kwamba alikuwa akishindwa kuinuka bila shaka kutokana na wasiwasi wa kwenda kufungiwa selo.

Mama mkwe na yule mchawi aliyenasa kwenye nyumba ya jirani wakawa wameshafungiwa lokapu.

Mume wangu alijitahidi kuomba kwa kamanda wa polisi ili mama yake asiwekwe ndani na badala
yake amuwekee dhamana alishindwa.
“Unajua mzee, hatumuweki ndani huyu bibi ili kumkomoa, tunamuweka tukiwa na maana yetu,
“Nakuomba sana kamanda, kwa nini asiende kulala nyumbani na kesho nikamleta?
“Sisi jeshi la polisi hatufanyi kazi kwa kubabaisha, Ni kwamba, kutokana na tukio analohusishwa nalo kuna taarifa za kintelejensia watu wenye hasira kali
wanamsubiri ili wampige. Wanaweza kuchoma moto nyumba yako na ukapata hasara mara mbili. Pia Kuuawa kwa mama yako na kupoteza mali kwa
kuchomwa nyumba na vitu vyako. Hatuwezi kujua, Wanaweza kujichukulia sheria mkononi usiku mkiwa mmelala.
“Sasa ina maana nimuache hapa polisi siyo?
“Ndiyo maana yake.
"Lakini afande naamini nyumbani kungekuwa salama kabisa
"Elewa tukimuachia na balaa likazuka huko kwako, wakubwa wetu watatuona
hatukutumia ujuzi wetu wa miaka mingi katika kazi hii, naomba sana usituponze na usijiponze pia.
“Ukimpa dhamana sitampeleka nyumbani,
"Utampeleka wapi sasa?
"Nitamhamishia kwa mtu mwingine,
“Mzee unasema tu, huko nje umechungulia?
"Ndio
"Kuna watu kibao wanasubiri kuwaona hawa wachawi. Wapo wenye magari na waendesha bodaboda. Watakufuatilia
kwa nyuma kwa hiyo usitake kuhamishia tatizo hili katika nyumba ya mtu mwingine,
"Sawa afande.
"Afande alifunika jalada la kesi hiyo, akainuka na kuliweka kabatini.

Tuliangaliana na mume wangu baada ya jibu la kamanda, akilini mwangu nilijisemea kwamba anachosema kiongozi huyo ni kweli kabisa, kwani
nje ya kituo cha polisi kulikuwa na umati wa watu waliokuwa wakiimba;

{ Tunataka watolewe }
{ Tuwaone, wauliwe. }
{ Tunataka watolewe }
{ Tuwaone, wauliwe. }

Yule kamanda aliondoka ofisini kwake baada ya kulifungia jadala la maelezo ya mama mkwe na yule mchawi mwenzake na alituacha tukiwa mle ndani.

“mume wangu unasikia huko nje?
"Nasikia mke wangu
"tutafakari sana kuhusu huyu mama, wanaweza kumuua hawa, (nilimshauri mume wangu ).
“Ni kweli mke wangu, nadhani tukubaliane na haya wanayosema polisi,
tusing’ang’anie kumtoa.

Hakukuwa na njia nyingine isipokuwa kumsubiri kamanda ili tumuage na tuondoke. Wakati nawaza hili na lile yule kamanda aliingia akiwa na karatasi
ambayo nilikuwa sijajua ilikuwa ya nini.

“Mzee, na nyinyi mlioingiliwa ndani na wachawi, mnaweza kwenda na RB ya kesi yenu hii hapa,
“Tafadhali tueleze utaratibu wa kesho,
( mume wangu alitaka ufafanuzi. )
“Kesho tunatarajia kulipeleka jalada ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka na kama litarudi tutaona watafunguliwa mashitaka gani. Cha muhimu ni
kwamba jioni mleteeni chakula bimkubwa,

alishauri yule askari kamanda wa polisi.
Tuliondoka wote wanne, yaani mimi na mume wangu na jirani na mkewe hadi nyumbani.

Tulijisikia aibu kutokana na kitendo cha mkwe wetu kwenda kwa jirani na kutaka kuwaangamiza.

Jioni ilipofika niliandaa chakula na kuwapelekea mama mkwe na yule mchawi mwenzake, mama mkwe nilimshuudia akila kile chakula bila wasiwasi, walipomaliza nikachukua vyombo na kulidi zangu nyumbani.

Usiku wa saa nane mambo yakawa mambo kituo cha polisi, mzee kipesani na wachawi wenzake baada kufanya upelezi wao na kukamilika wakatinga kituo cha polisi wakiwa na ndege yao.

Baada ya kufika hapo walizi waliokuwa zamu wote wakashangaa wapo kwenye lumande moja pamoja na wale wachawi wakuwa bado wanashangaa imekuaje wakashaa mama mkwe wangu kajitoa kopy, ina maana wapo wawili lakini nguo za rangi tofauti.

Walijitahidi kutaka kutoka lakini hawakujua hata mlango upo wapi, wakiwa bado wanahaha mle ndani nafsi moja ya mama mkwe wangu ikaanguka na kufa na nafsi moja ikatoweka pamoja na yule mchawi.

Sekunde chache tu baada ya mama mkwe kutoweka walishuhudia upepo mkali sana baada ya ule upepo kupita wote wakajikut wapo nje ya selo.

Walikuwa kama wanaota vile walipo angalia ndani ya selo aliyofungwa mama mkwe wangu walishuhudia akiwa amedondoka na ile selo ya yule mchawi mwingine hayupo baada yakuingia na kumwangalia mama mkwe wangu waligundua kuwa kafariki.

Walifanya mawasiiano na kamanda mkuu wa zamu na kutoa taarifa ya kifo cha mama mkwe wngu na hawakujua wajibu nini kuhusu yule kijana aliyetoweka.

Baada ya mda kidogo kupita kamanda mkuu akawasili na kushuhudia mama mkwe wangu akiwa amefariki, walichuku mwili wake na kupelea hospital kwa uchunguzi zaidi..

Itaendelea.........
 
BI MKUBWA
( sehemu ya 12 )

Endeleaa.................

Baada ya mda kidogo kupita kamanda mkuu akawasili na kushuhudia mama mkwe wangu akiwa amefariki, walichuku mwili wake na kupelea hospital kwa uchunguzi zaidi.

Baada ya kumfikisha hospital madaktari wakaanza kufanya uchunguzi was maiti ya mama mkwe, walipo maliza uchunguzi waliwasilisha majibu Kwa kamanda,

"Kamanda majibu yapo tayari.
"Amefariki Kwa tatizo gani?
"Hadi saizi tumefanya vipimo vyote hatujaona ugonjwa wowote.
"Sawa imekuaje amefariki,
"Hats sisi madakitari hatujajua ni tatizo gani, hata hivyo mwili wake una maajabu kidogo
"Maajabu gani tena?
"Moyo wake umesimama ila cha kushangaza damu bado inazunguka mwilini,
"Ina maana hajafa?
"Hilo ni swali gumu sana kwangu.
"Kwanini doctor?
"Kwa sababu moyo umesimama na damu bado inafanya kazi.
"Doctor cha msingi moyo umesimama andika tu taarifa ya kifo.
"Sasa afande tutaandika kafariki na ugonjwa gani?
"Andika pressure tutafanyaje sasa.
"Sawa afande,
"Doctor Fanya mpango peleka mwili mochwari baadae ndugu zake watafika kuuchukua.
"Haina shida afande.

Basi Kulipopambazuka tulijiandaa kumpelekea mama mkwe chai. Nilichemsha chai na maandazi na kuweka kapuni.

Tulipofika polisi tulikuta mkusanyiko mkubwa wa askari, walipotuona wote waligeuza shingo zao kutuangalia.

"Shikamo afande
"Marahaba, mnaendeleaje.
"Tunaenfelea vizuri
“Mmekuja, jamani njooni ofisini kwangu,

Tulipoenda akatuambia kuwa asubuhi
alipoenda kuwaangalia watuhumiwa waliokuwa lokapu, alikuta mama mkwe amefariki dunia.

Tulipigwa na butwaa na kuuliza maiti yake ipo wapi, kamanda alituambia kuwa tayari wameipeleka mochwari kuhifadhiwa. Binafs sikuhuzunika sana nilijua kuwa hiyo yote ni mipango ya Mungu na niliamini kuwa ameniepushia
na mambo mazito ambayo nilihisi yangeweza kutokea mbele ya safari.
Wakati nikitafakari hayo,

"Afande mama angu kafa na homa gani?
“Daktari amempima amesema alikuwa na presha,
"Pressure hiyo imemuanza lini toka utotoni hadI Leo sijawahi kumwona mama angu akisema ana pressure.
"Mzee sisi hatujui hayo kama hauamini inabidi ukaongee na doctor akupe maelezo zaidi na sisi polisi tunapokea majibu kutoka hospital,
"Afande lakini kumbuka Jana nilikwambia nimchukue mama nikalale nae nyumbani asubuhi nimlete ukakataa,
"Sasa kwa maana hiyo Mimi ndio nimemuua.?
"Hujamuua ila unipe maelezo yakutosha ya kifo cha mama angu.
"Sawa Mimi nitamuomba doctor aje akupe maelezo maana Mimi sijui chochote kuhusu kifo hicho.
"Sawa basi naomba kuongea na hule mchawi aliyenaswa?
“Samahani sana, Cha kushangaza ni kwamba yule mchawi aliyekuwa amenasa kwenye nyumba ya
jirani yenu hatukumkuta mahabusu!
"Afande hapo ndio nitawafikilia vibaya sasa katoroka vipi kituoni?
"Tunamtafuta tutampata, usitufikilie hivyo.
"Amevunja mlango au dilisha?
"Hapana
“Ina maana askari aliyekuwa zamu
kamtorosha?
“Sisi tumeshangazwa, askari wote waliokuwa zamu usiku tumewaweka ndani baada ya kuwahoji lakini
wote wanasema, hawakula njama za kumtorosha na sisi tunaamini kwamba ametoka kishirikina,
“Sasa itakuwaje?
“Itabidi asakwe na akamatwe, kwa sababu ni dhahiri kwamba ametoka mahabusu kishirikina,

Alinyamaza kidogo, akachukuwa kiwiko cha simu kisha kubonyeza vitufe.
“Haloo, hebu nipe kiongozi wa hapo kaunta,
"Sawa, huyu hapa,
“Niletee lile jalada lenye maelezo ya yule kijana aliyetoweka selo.

Baada ya kutoa amri hiyo alifika askari mmoja ambaye alionekana ni sajenti kwa kuwa alikuwa na V tatu kwenye mkono wake kwa juu karibu na bega.

Askari huyo alishindilia guu chini, akapiga saluti,
“Jambo afande?
“Jambo,
akapokea jalada na kugeuza kutoka
alikotoka. Kamanda alituangalia huku akipekua makaratasi yaliyoambatanishwa ndani ya jalada
hilo.

“Humu ndani yule mchawi haijaelezwa anakaa wapi, kati yenu kuna mtu anajua anakaa wapi?”
Mimi na mume wangu tuliangaliana, tulitikisa kichwa kuashiria kuwa hakuna kati yetu anayejua nyumbani kwa mchawi yule, mume wangu akajibu:
“Hatujui anakaa wapi, lakini katika maelezo yake aliyoyatoa kwenu hakutaja anakokaa?
“Alaaa, hilo sikulitambua lilinipita, ngoja tuone.

Alifungua jadala lile alilopewa na yule askari na kusoma. Alikuwa kila akisoma anatikisa kichwa kama vile kaambiwa jambo na kulikubali.
“Kumbe ameandikisha hapa kuwa anakaa mahande, itabidi nitume askari kule wakafuatilie,

Sisi kuhusu huyo mchawi tuliona ni jambo ambalo halituhusu. Tulimuaga yule kamanda na kutoka nje ya ofisi yake. Habari zilizagaa mjini kwamba mama mkwe amefariki dunia.

Kulikuwa na maelezo ya kutofautiana kati ya kundi moja lililokuwa likijadili
tukio hilo na lingine. Kuna waliokuwa wakisema aliteswa sana na askari na ndiyo maana akaaga dunia na wapo waliosema kwamba hakufa, ametoka selo na watu kuona kama amefariki dunia.

Hata hivyo, hoja hiyo ilikuwa inapingwa na baadhi ya watu ambao walisema kama ni kutoka angetoka akiwa hai kama alivyotoweka mchawi mwenzake.

Hoja hizo tulikuwa tunazisikia njiani
wakati tunarudi nyumbani, tulikuwa tunakuta makundi ya watu wanajadili, bahati nzuri ni kwamba hakuna hata mtu aliyekuwa akijua sisi tulikuwa wahusika wakuu.

Naamini kama wangejua waliyekuwa wanamjadili alikuwa mama mkwe wangu, naamini safari yetu ya
kurudi nyumbani ingekuwa ngumu kwani
tungesumbuliwa ili tuwape ufafanuzi.

Tulifika nyumbani na kukuta tayari ndugu na majirani wamefurika.
Moja kwa moja kikao cha wanandugu kilianza na mume wangu aliwapa taarifa rasmi ya nini kimetokea kule kituo cha polisi.

Japo kuwa alikuwa kafariki lakini watu walionge sana Kwa vitendo vyake vya kishirIkina nilishuhudia kikundi kimoja cha kinamama wakiongea hivi:

"Wewe wachawi unawajua?
"Kuwajua kivipi.
"Huyo kajibadili tu mwenyewe atakuwa katoweka na utasikia yupo sehemu fulani,
"Kumbe inawezenana heee?
"Washidwe nini wewe unacheza na wachawi nini.
"Basi hiyo itakuwa balaa,
"Si umesikia yaliyotokea huko polisi?
"Sijasikia,
"Hujasikia kuwa yule mwanaume aliyenasa ile nyumba ya jirani polisi hawakumkuta mahabusu asubuhi?
"Acha wewe!!!
"Inasemekena alifungiwa lokapu lakini asubuhi wakakuta hakuna mtu. Waliangalia mlango wao wa chuma, ulikuwa umefungwa na nondo kwenye madirisha zilikuwa nzimaaa.
"Duh, ikawaje?
"Ikawaje? Unauliza sharubu kwa Osama, polisi wote waliokuwa zamu usiku wamewekwa ndani.
"Hee! Kwa nini?
"Eti wakubwa wao wanadhani wamemtorosha.
"Hawana akili hao wakubwa.?
"Wanajua wamemtorosha.
" Wamtoroshe kisha wapoteze kazi, kisa?
"Hawajiulizi kwa nini alikutwa ndani kwenye nyumba ya watu wakati hakuna mlango wala dirisha lililobomolewa?
"Unajua wakubwa serikalini wanajifanya hawaamini uchawi lakini wao ndiyo waumini wa uchawi kwelikweli, kila siku wanakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta kupandishwa vyeo.
"Una uhakika?
"Wewe endelea kusubili uhakika.
"Sasa huyo mchawi aliyetorka wanaweza kumpata kweli?
"Itakuwa kazi kubwa. Baada ya kutoka rumande atakuwa amehama mji huyo, lakini serikali ina mikono mirefu, wanaweza kumtia mbaroni.
"Lakini huyo mchawi nae kiboko. Hiyo dawa wakiipata majambazi tutakwisha wote. Maana wanaweza kuingia benki wakazoa fedha zote wakakimbia nazo.
'"Kweli, lakini nilisikia mtu mmoja akisimulia kwamba masharti yao ni magumu wakiingia ndani ya nyumba kimiuji, sharti lao ni kwamba, kwa kuwa wanaingia kupitia ukutani, si ruhusa kutoka ndani hata na sindano, ndiyo maana hawaibi benki.
"Kwa sharti hilo hata mimi naamini kuwa ndiyo maana wachawi hawaibi benki.

Mazungumzo ya wanawake wale yalikatizwa na tangazo la MC aliyesema kwamba mwili wa marehemu mama mkwe umeshafika pale nyumbani.

Wanaume walibeba jeneza lenye mwili na kuliweka ndani. Kusema kweli waombolezaji walikuwa wachache. Walimlaani mama mkwe kutokana na mpango wake wa kutaka kumroga mume wangu yaani mwanaye.

Hakukuwa na ucheleweshaji, marehemu alipelekwa makaburini na alizikwa na watu wachache sana, wengi walichukizwa kwa tabia yake ya uchawi.

Baada ya kumaliza kuzika ndugu nao waliondoka mda si mrefu baada ya kula chakula, hatimaye Giza likaingia, Mimi na mume wangu tukaingia chumbani kulala ilipofika SAA saba usiku mlango wa chumbani kwetu uligongwa,

Tulijiuliza maswali mengi sana ni nani anayegonga mlango wakati hii Nyumba saizi tupo wawili tu, mume wangu akafungua mlango alipofika sebuleni alikuta paka wawili wamekaa sebuleni, cha ajabu paka mmoja akaanza kulia kama mtu na kusema mwanangu nisamehe.

Mume wangu akatoka mbio kuja chumbani kwetu akanishika mkono na kuniambia njoo uone maajabu, tulipofika sebuleni cha ajabu tukamkuta mama mkwe na yule mchaWi aliyekuwa amenasa Nyumba ya jirani, wakiwa wamevaa nguo zao nyeusi na viremba vyeupe kichwani wakiwa wameshika zana zao za kichawi

"Mwanangu usiogope njoo ukae tuonge.

Itaendelea ...............
 
Back
Top Bottom