Makapuku Forum

Siku nyingi sana aisee
 
7. Sheffield United Vs Sheffield Wednesday ( Steel City Derby )

Inajulikana pia kama Sheffield Derby inazikutanisha timu hizi zinazotoka sehemu ya Sheffield. Mechi hii inajulikana pia kama mechi ya ukarimu, mechi ya marafiki kwani kuna idadi kubwa sana ya wachezaji na makocha waliowahi kufanya kazi katika timu zote mbili. Japo kuna muda mechi huwa na utata na rabsha za hapa na pale.


 
Mashabiki pekee ndio hawashangilii pande mbili. Undava undava tu
 
6. Southampton Vs Portsmouth ( South Coast Derby )

Mechi huzikutanisha timu mbili hasimu kutoka Pwani ya Kusini ya Uingereza. Mechi hii imepoteza mvuto kutokana na timu hizi kwa muda kucheza katika madaraja tofauti na kufanya kukutana mara chache sana katika miaka ya karibuni.

Kocha Harry Redknapp aliwahi kuingia kwenye mgogoro baada ya kuhama Portsmouth na kwenda Southampton na kisha kurudi Portsmouth huku akiwaacha Saints ( Southampton ) wakishuka daraja.


 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…