Makapuku Forum

Ingependeza zaidi uwe unatuandikia kwa Kiswahili
Wengine tumeishia darasa la 5 tunapata shida kutafuta translation mkuu
.......
 


Ha hahahaha, hii sethali imenifurahisha sana na kiukweli hili hutokea sana yaani kuna wakati unakuwa kama greda, unatengeneza njia nzuri ukidhani nawe utapita lakini ikikamilika huruhusiwi kupita labda kwa kubebwa na unajua kubebwa unakuwa huna cha kuamua.
Kipengele kizuri mjomba.
 
FurahiDei is Old: Muziki Unatuchekesha

Habari Makapuku, nina imani siku imekwenda vizuri na tunauanza mwanzo wa weekend. Hivi leo ndo siku ya kuvunja jungu eeh au bado?

Maana tunajiandaa na mengi mfungo huu, aidha kwa kukosa au kupata. Yote iwavyo, leo ni ijumaa, furahiday na inabidi tufurahi.

Kwa wapenzi wa muziki na hasa band ambapo unaliskia gitaa kwa uzuri kabisa basi leo tuangalie muziki mchangamfu. Muziki wa kukatika, yaani kunyongorosha kiuno na mapega feni lisingiziwe.

hapa gitaa zinacharazwa kwa umakini utafikiri mwalimu wa nidhamu kashika wiki

naongelea bendi iliyokuwa na fujo miaka ya 90s hapa Africa Mashariki. Nawaongelea Katitu Boys, wana micharazo

Hebu waangalie kwenye clip hii ya YouTube.

Ukimaliza kuwaangalia mimi nitakuwa hapa hapa naangusha moja moja bila kujali nitasema nini baadaye

 
RIP Kevin
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…