[3/20, 09:20] Dah kama ni movie basi ndo imefika pale mahali hutamani hata kwenda kujisaidia ama pale wanaposema *WATCH* *OUT* *PART* *TWO*

♀
[3/20, 09:24] : Ukicheza na mbwa atakufuata mskitini cloud's walizidi kumsafisha makonda
[3/20, 11:42] "Baada ya hapo nilishuka chini nikakuta Mkuu wa Mkoa yupo na vijana wa 'Shilawadu' walikuwa kama wanakitu wanazungumza" @MutahabaRuge
[3/20, 11:43] : Nikiwa kwenye Gari alinifata mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kuniambia kuhusu mwanamke aliyezaa na mchungaji @MutahabaRuge
[3/20, 11:54] "Alhamis tulikuwa na kikao na kamati ya maudhui na TCRA katikati ya kikao tukapata ugeni wa Mkuu wa Mkoa na baadae akaondoka" @MutahabaRuge
[3/20, 11:56] Wakati natoka ofisini nje nilikutana na Makonda na Vijana wa Shilawadu nikauliza kwema hapa nikajibiwa ni Story za kawaida tu. @MutahabaRuge
[3/20, 12:11] Baadaye nilipata Simu kutoka kwa Mkurugenzi @JosephKusaga kwamba anatupiwa lawama na mkuu wa mkoa amezuia kipindi chake. @MutahabaRuge
[3/20, 12:13] Nilitoa maelezo kwa boss wa vipindi Clouds TV kuhusu hiyo Story isiyokuwa na maana sababu haina balance kuwa kisiruke hewani. @MutahabaRuge
[3/20, 12:14] : Nilimueleza Boss Kerry awasiliane na Makonda kwamba video yake haitoruka hewani sababu haina balance @MutahabaRuge
[3/20, 12:15] Mida ya Saa 10 Alhamisi nilipata Simu ya Gwajima kunieleza kuhusu kuwepo kwa habari inayonihusu nikamueleza hiyo Story haitoruka. #Ruge#
[3/20, 12:17] : Nikawauliza hiyo Story mna uhakika nayo kwenye balance mtapata Mchungaji Gwajima? @Rugemutahaba nilimpigia Kerry kumuuliza hii story!
[3/20, 12:18] Ukweli sisi kama chombo cha Habari lazima tujenge heshima ya kutoa habari zenye uwiano lazima tuiheshimu taasisi yetu. @MutahabaRuge
[3/20, 12:18] : Siku ya Ijumaa Saa tano kasoro nilipokea Simu kutoka kwa HR wetu mkuu wa mkoa ameingia ofisini akiwa na Askari sita wenye silaha. #Ruge#
[3/20, 12:19] Naomba nieleweke wazi hatuwezi kumuacha mtu akatupanda kichwani hii ni dharau kwangu nasimamia watu 200 asinidharau. @MutahabaRuge
[3/20, 12:19] Mimi sitaki kuona bunduki mtaani kwa maslahi ya Vizazi vya kesho bunduki ziwepo wanapolinda benki sio kwenye media. @MutahabaRuge
[3/20, 12:20] Kwa Mara ya kwanza Makonda anatuvunjia heshima sisi kama Rafiki zake tulifanya kazi naye Uzuri tangu akiwa Mkuu wa wilaya. @MutahabaRuge
[3/20, 12:20] Hofu yangu ni kwamba kama mimi nipo na mkurugenzi yupo kwanini asingetengeneza mazingira ya kuonana na sisi kwanza. @MutahabaRuge
[3/20, 12:21] Baadaye nikampigia Simu Makonda nikamuuliza kwanini hakunipigia Simu mimi kwanza kabla ya kufanya lile jambo. @MutahabaRuge
[3/20, 12:21] Panapotokea misingi ya hofu lazima tuweke wazi kabisa bila kificho panopohitaji ukweli lazima tuweke wazi ukweli usemwe. @MutahabaRuge
[3/20, 12:22] Mfano wangu ni kwa Simba na Yanga ni mahasama lakini chombo kinachowasimamia kikiingilia maslahi yao wanaungana. @MutahabaRuge
[3/20, 12:22] Vijana wa SHILAWADU wapo kwenye hofu wametishwa wamepoteza morali na kazi yao hawana Amani tena wameomba likizo. @MutahabaRuge
[3/20, 12:23] Kauli yangu ya mwisho ilikuwa habari ya Askofu Gwajima isiruke. Ijumaa nimekaa nyumbani usiku nashangaa kupokea simu ya Meneja wetu wa masuala ya Uajiri , akaniambia ofisini kuna 'Crisis'. Nikauliza kuna nini? Nikaambiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda amekuja ofisini na ameingia na watu karibia Sita wamebeba bunduki " -# RugeMutahaba .
[3/20, 12:23] Sisi tunampenda Makonda hatulipi chochote tunaipenda Dar es Salaam tulifanya kampeni ya Dar Mpya kwa Mapenzi yetu wenyewe. @MutahabaRuge
[3/20, 12:24] Paul, ambaye ni rafiki yetu AMETUKOSEA. Huwezi kuja Ofisini kwetu ukiwa na mabunduki tena usiku. Kama kuna tatizo, Paul ana namba yangu ya simu. Paul ni alikuwa rafiki yetu kweli tangu akiwa mkuu wa Wilaya na mimi siwezi kukataa urafiki. " # RugeMutahaba .