Makapuku Forum

1990 - Kiongozi wa Soviet, Mikhail Gorbachev anazawadiwa tuzo ya Nobel kwa mchango wake mkubwa katika kumaliza Vita Baridi iliyokuwepo kwa miaka takribani 30 kati ya Urusi na Marekani.

Gorbachev anachukuliwa kama pandakizi aliyekulia na kusomea Marekani na ambaye baadae CIA ilikuja kumuingiza kwenye siasa za Urusi na kushinda Urais na baadae kuvunja Umoja wa Kisoviet wa Kirusi ( USSR ).
 
 
1968 - Didier Deschamps anazaliwa.

Kiungo mkabaji wa zamani na nahodha wa Timubya taifa ya Ufaransa.

Alikuwepo kikosini wakati Ufaransa inatwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 katika ardhi ya nyumbani akiwa kama kepteni.

Pia Ufaransa ilivyobeba kombe la ulaya mwaka 2000.

Aliwahi kugombana na Eric Cantona kwenye timu ya taifa, baada ya Cantona kumuita Deschamps mbeba maji " Water Carrier " kwakuwa alikuwa anacheza namba 6 kazi yake kuu ni kupora mipira na kumpa Cantona achezeshe timu hivyo hakuwa na ufundi.

Kauli hiyi ilimfanya Cantona kutoitwa tena kwenye Timu ya Taifa.
 
Didier akiwa uwanjani huwa hakati tamaa, anajua kupigana akiwa uwanjani
 
1977 - David Trezeguet anazaliwa.

Ni mshambuliaji wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa.

Anakumbukwa kwa kupiga penati ya ushindi iliyowapa Ufaransa taji la Euro 2000 dhidi ya Italy.

Miaka sita baadae katika fainali ya Kombe la Dunia, anakumbukwa kwa kukosa penati muhimu iliyiwapa Italy ubingwa huo wa Dunia.
 
1979 - Paul Robinson anazaliwa.

Ni golikipa wa zamani wa England.

Anakumbukwa zaidi wakati wake akiwa na Vilabu vya Leeds United, Tottenham na Blackburn Rovers.

Waingereza hawawezi kumsahau, mara baada ya kurudishiwa mpira na Gary Neville badala ya kupiga mpira uende mbele yeye akaukosa na mpira kujaa wavuni. Hii ilikuwa ni moja ya sababu ya England kushindwa kufuzu fainali za Euro 2008.
 

Kile kikosi noma
.....
 
Dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…