Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG_20161008_203443.jpeg
 
Hii Bitoz ifungulie Uzi wake kule habari mchanganyiko, na kichwa chake kiwe hichohicho hujafa hujaumbika halafu tuje kuushambulia Uzi, nadhani Uzi utakwenda mbali sana
Ungeenda ww mbona unanisakizia....mi sinaga mpango wa kuanzisha thread labda km kuna jambo nataka kueleweshwa tu (kuuliza)
..............
 
Mji wa New York uko masaa 3 mbele ya mji wa California lakini haimaanishi kuwa California ni mji ambao uko slow...wala New York sio kwamba uko fast ... miji yote inaishi kwa kutegemea TIME ZONE...
Kuna mtu mpaka sasa yuko single...na mwingine alioa mapema tuu na kusubiri miaka 10 kupata mtoto...na yupo mwingine ambaye alipata mtoto ndani ya mwaka mmoja tuu baada ya kuoa.
Kuna ambaye aligraduate akiwa na miaka 22 na akasubiri miaka 5 kupata kazi nzuri...na kuna ambaye aligraduate akiwa na miaka 27 na akapata kazi mara moja!!
Kuna ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni akiwa na miaka 25 tuu na akafariki akiwa na miaka 50 wakati huohuo yupo aliyeweza kuwa mkurugenzi akiwa na miaka 50 na akaishi hadi miaka 90...
So mwisho wa siku unagundua kuwa kila mmoja wetu ana TIME ZONE yake... Ndugu zako au rafiki zako wanaweza kuwa mbele yako au wanaweza kuwa nyuma yako lakini kamwe USIWAONEE WIVU WAWAPO MBELE YAKO na pia USIWAKEBEHI UWAPO MBELE YAO maana kila mtu yupo kwe TIME ZONE yake..
Hold on, be strong, and stay true to yourself...maana all things shall work together for your good...Hujachelewa na wala Hujawahi...upo ON TIME... STAY BLESSED.

JUMAPILI NJEMA
.............................
 
Maneno murua kabisa haya, Yanafariji kwa waliokata tamaa
 
Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguoza kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.

Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.

Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”

Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?!

Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana.

Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: “Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu”

“Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto.

Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.

“ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.

Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:
“Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.”

HEKIMA:
1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI
KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.

2. “TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILAYA KUJALI HALI ULIYONAYO.
Ahsante kwa ujumbe murua kabisa...
 
Mji wa New York uko masaa 3 mbele ya mji wa California lakini haimaanishi kuwa California ni mji ambao uko slow...wala New York sio kwamba uko fast ... miji yote inaishi kwa kutegemea TIME ZONE...
Kuna mtu mpaka sasa yuko single...na mwingine alioa mapema tuu na kusubiri miaka 10 kupata mtoto...na yupo mwingine ambaye alipata mtoto ndani ya mwaka mmoja tuu baada ya kuoa.
Kuna ambaye aligraduate akiwa na miaka 22 na akasubiri miaka 5 kupata kazi nzuri...na kuna ambaye aligraduate akiwa na miaka 27 na akapata kazi mara moja!!
Kuna ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni akiwa na miaka 25 tuu na akafariki akiwa na miaka 50 wakati huohuo yupo aliyeweza kuwa mkurugenzi akiwa na miaka 50 na akaishi hadi miaka 90...
So mwisho wa siku unagundua kuwa kila mmoja wetu ana TIME ZONE yake... Ndugu zako au rafiki zako wanaweza kuwa mbele yako au wanaweza kuwa nyuma yako lakini kamwe USIWAONEE WIVU WAWAPO MBELE YAKO na pia USIWAKEBEHI UWAPO MBELE YAO maana kila mtu yupo kwe TIME ZONE yake..
Hold on, be strong, and stay true to yourself...maana all things shall work together for your good...Hujachelewa na wala Hujawahi...upo ON TIME... STAY BLESSED.

JUMAPILI NJEMA
.............................
Aksante kwa ujumbe maridhawa.
 
Back
Top Bottom