Makapuku Forum

Hakika ushauri murwaaaa
 
NUKUU NO 1#

Taifa letu ni kubwa,ni zuri na mahari pa kuishi na kuendelea kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka na wanajitambua haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa Jamii.

Na ukweli ni kuwa ni walimu, kuliko kundi lolote jingine, ndio wanaoamua mtazamo huu,na kubadili mawazo na matumaini ya Taifa.

Haya yalisemwa na Rais wa kwanza wa Tanzania na baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika chuo cha walimu Morogoro, mwaka 1996. Mwalimu alifariki Oct 14,1999 kwa ugonjwa wa kansa ya damu
 
NUKUU NO 2#

Jukumu la Elimu ni kumfundisha mtu kufikiri kwa kina nakwa udadisi.
Kiwango cha ufahamu ukijumlisha na wasifu wa mtu, hilo ndio lengo la Elimu.

Haya yalisemwa na mwanaharakati na mpigania haki za binadamu na kiongozi wa vuguvugu la kudai haki na usawa wa Waafrica wenye asili ya Marekani,
Martin Luther King Jr. Alizaliwa Jun 15,1929 na alifariki Dunia April 4,1969
 
NUKUU NO 3#

Elimu ni silaha yenye nguvu kubwa kuliko zote ambayo mtu anaweza kuitumia kubadilisha ulimwengu.

Haya yalisemwa na Rais wa kwanza mweusi wa Africa kusini Nelson Mandela.
Mpigania uhuru huyo alifungwa jela na serikali ya makaburu kwa miaka 27,mpaka mwaka 1990 alipofunguliwa na kuashilia mwanzo na mwisho wa ubaguzi wa rangi nchini Africa ya kusini,
Aliiongoza nchi hiyo Kati ya mwaka 1994 mpaka 1999.
Alizaliwa Julai 18,1918 na kufariki Dunia Dec 5,2013
 
NUKUU NO4#

Elimu sio maandalizi anayo fanya mtu kwa ajili ya baadaye. Elimu ndio maisha yenyewe.

Haya yalisemwa na mwanafalsafa wa kimarekani John Dewey, ambaye pia alikuwa mwanaharakati wa mageuzi ya elimu na mwanasaikolojia.

Alizaliwa Oct 01,1859 na kufariki Dunia Juni 01,1952
 
Huu ni ukweli kabisa, tujifunze kutosheka na pia tusipende kulalamika kana kwamba sisi ndio pekee wenye shida ulimwenguni
Asante werrason
 
Apumzike kwa amani mwalimu
 
R I P Martin Luther King
 
R I P Tata Madiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…