Makapuku Forum

Eid Mubarak wanajukwaa. Yeah, sikukuu ya kuchenja, mkesha umeanza jana na leo tunamaliza. Ndiyo sikukuu pekee ambayo si Bakwata wala Chimumuna wa hapa Mtwara tunakubaliana bila kuangaliana kwa jicho la tenge.

Binafsi, sijachinja ila najua kwa aliyechinja atanikaribisha maana nyama lazima igawiwe mara tatu, kwa familia na ndugu, pili kwa marafiki na majirani na tatu kwa masikini unaowajua hawana uwezo.
Toa sadaka na tii amri za Mungu.
makaveli10 fanya urushe kuku mmoja wa kienyeji pande hizi, naelekea Mjimwema nikaoshe macho
 
Idd inaendaje Obe maana ustadh moudgulf kazima cm hapatikani huenda ningeambulia hata kilo 1 ya ngamia.
 
Mkuu, we njoo kesho asubuhi..
Sheria ya dini inataka mnyama mwenye miguu mi4..
Mie nimechukua kuku wawili nimewabananisha na kuchinja πŸ˜‚πŸ€£

Karibu sana tupate upepo wa bahari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…