Makapuku Forum


Habari njema kwa Afrika mashariki
Habari njema kwa Tanzania
Na pia ni habari njema kwa mkoa wa Tanga
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Mobhare Holmes Matinyi kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria.

Matinyi amewahi kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kisha baadaye kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Jabiri Kuwe Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Dkt. Bakari anachukua nafasi ya Salim Ramadhani Msangi ambaye atapangiwa majukumu mengine, kabla ya uteuzi huu Dkt. Jabir alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA .
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Peter Phillip Mwasalyanda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Mwasalyanda alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na anachukua nafasi ya Dkt. Jabiri Kuwe Bakari ambaye amemaliza muda wake.
 
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza mabadiliko ya Uwanja wa Mchezo namba 169 wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 utakaowakutanisha Simba SC na Young Africans SC (Yanga), maarufu kama Dabi ya Kariakoo ambapo sasa hautafanyika tena katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kama ilivyopangwa awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 24, 2026 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya TPLB, mchezo huo sasa utafanyika katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Jijini Dar es salaam, na unatarajiwa kuchezwa Mei 3, 2026 kuanzia saa 12:00 jioni.

Sababu ya mabadiliko hayo ni kuendelea kwa matengenezo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, hali iliyolazimu Bodi hiyo kubadili eneo la mchezo huo muhimu ili kuhakikisha Ratiba ya Ligi inaendelea kama ilivyopangwa bila usumbufu wowote.

TPLB imesema tayari klabu za Simba na Yanga pamoja na Wadau wengine wa Ligi Kuu ya NBC wamepatiwa taarifa rasmi kuhusu mabadiliko hayo, huku maandalizi ya kuelekea mchezo huo yakianza mara moja ili kuhakikisha unachezwa katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya ligi hiyo Barani Afrika.
 
Serikali ya Norway imetangaza mpango wa kuwasilisha muswada bungeni utakaopiga marufuku watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii, hatua inayolenga kulinda ustawi wa watoto katika ulimwengu wa kidijitali.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya ABC News hatua hiyo itakayowasilishwa bungeni kabla ya mwisho wa mwaka 2026, inaifanya Norway kuungana na mataifa kadhaa yaliyoanza kuchukua hatua kali kudhibiti matumizi ya teknolojia kwa watoto.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Jonas Gahr Støre akizungumza na vyombo vya habari leo Aprili 24, 2026 amesema lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha watoto wanapata malezi yanayozingatia ukuaji wao wa kawaida bila kuathiriwa na matumizi makubwa ya mitandao.

“Tunalenga kurejesha utoto wa watoto wetu. Michezo, urafiki na maisha ya kawaida ya kila siku ya watoto.”

Mpango huo unafuatia hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Australia, ambayo mwaka jana ilipiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16.

Wakati huo huo, bunge la Uturuki limepitisha sheria inayokataza watoto chini ya miaka 15 kutumia mitandao hiyo, huku pia likizihusisha kampuni za michezo ya kidijitali.

 
Swali la mwanaume anatakiwa kufanya tendo la ndoa mara ngapi kwa wiki limekuwa likijadiliwa kwa muda mrefu, huku wengi wakilitafsiri kama kipimo cha “nguvu za kiume”.

Hata hivyo, daktari bingwa bobezi wa magonjwa ya mfumo wa mkojo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Remigius Rugakingira, amesema hakuna idadi maalumu inayomfanya mwanaume aitwe ana nguvu au hana.

Akizungumza na Mwananchi, Aprili 22, 2026 Dk Rugakingira amesema kiafya mwanaume anaweza kufanya tendo hilo mara tatu hadi tano kwa wiki bila madhara, lakini idadi hiyo inategemea hali ya mwili, aina ya kazi anazofanya na makubaliano na mwenza wake.

“Kuna wanaofanya kazi ngumu, hawa hata mara moja kwa wiki si tatizo. Muhimu ni kuridhishana na kuzingatia afya,” amesema.

Amesisitiza kuwa uanaume haupimwi kwa idadi ya kufanya mapenzi, bali ni mchanganyiko wa mambo mengi ikiwemo afya ya akili, lishe bora, mazoezi na hali ya homoni mwilini.

“Kuna dhana potofu kwamba mwanaume mwenye nguvu lazima awe anafanya mara nyingi, lakini hilo si sahihi. Hata mtu anayejizuia anaweza kuwa na uwezo mkubwa,” amefafanua.

Dk Rugakingira amesema uwezo wa mwanaume unahusisha mfumo mzima wa mwili kuanzia ubongo, mishipa ya damu na homoni ambavyo vinahitaji kuwa katika hali nzuri.

Anabainisha kuwa mawazo, msongo wa akili na uchovu vinaweza kuathiri uwezo wa kusimamisha uume na kufanya tendo kwa ufanisi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…