Farhan Jr
Kabla ya kulala nadhani Mwenyekiti wetu Mangungu tuna vitu vichache vya kukubaliana nawe kuelekea 2023/24 ili tusiwe na changamoto nyingi kama msimu huu unaomalizika.
Mwenyekiti suala la jezi rasmi za msimu mpya litazamwe kwa mapana sana, jezi zipatikane mapema kabla ya msimu kuanza, jezi zipatikane maeneo yote nchini ama tuwe na maduka ya kikanda, hili ni muhimu zaidi.
Kutangaza na kutoa jezi zetu mapema ni kuweka mazingira sahihi ya Mashabiki kujiandaa kiuchumi, ili waichangie klabu yao pale jezi zitakapotoka, hii itasaidia sana.
Mwenyekiti tuboreshe pia kwenye idadi ya jezi, tuna FA CUP, NBC PL na Champions League ni michuano Mama ambayo ni afya sana jezi zake zote zitoke pamoja mapema ili Mashabiki waenjoy na mitoko mapema.
Hii pia itatupa taswira nzuri kama timu, kuelekea SIMBA DAY mandhari yake yawe jezi mpya na kama kuna Wadhamini wapya basi wapate mileage yao vizuri sana, hili linawezekana.
Mwenyekiti pia nina ushauri huenda usiwe na maana sana ila tuone namna ya hii timu kucheza mechi angalau tatu kwenye mikoa ambayo soka halichezwi sana ili kuiuza hii timu na kuisogeza zaidi kwa watu.
Simba ni taasisi kubwa lakini marketing lazima iendelee, leo hii United, Madrid na timu kubwa zinazunguka duniani kucheza na kutambulisha wachezaji wao! Sisi tunaweza angalau mikoa mitatu nchini kabla ya kilele watu waione timu yao, hii sio ya Dar Es Salaam pekee.
La mwisho Mzee wangu Mangungu tupiganie hili suala la Wanachama wapya kama mchakato bado umekwama hapo FCC, ipo haja ya timu kuzalisha zaidi na kuingiza zaidi mapato kwakuwa lengo muscles basi hata mia mia zina nguvu yake.
Ni sahihi kufeli ila hatupaswi kufeli kwenye kila kitu! Muda tunao tena mwingi sana, em tujibane bane basi hapo tufurahi!
Ni hayo tu kwa leo!