Maombi ya Ofisa Habari wa timu ya Geita Gold, Hemed Kivuyo kutamani wakutanishwa na Yanga katika robo fainali Kombe la Azam Shirikisho yametimia baada ya droo hiyo kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kivuyo alisema anatamani wakutane na Yanga kwasasbu mara nyingi wamekuwa wakiwaponyoka.
"Kama ikitokea hiyo bahati Yanga wameangukia kwenye mdomo wetu tena tunachezea kwetu tutashukuru sana," alinukuliwa Kivuyo.
Droo hiyo imefanyika leo na Geita Gold imepangiwa kucheza na Yanga katika robo fainali itakayochezwa jijini Dar.
Mechi mbili walizokutana katika Ligi Kuu msimu huu Geita imefungwa zotr (1-0 CCM Kirumba, Mwanza) na 3-1 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar
View attachment 2553221