ANDREA PIRLO, THE PROFESSOR, THE BRAIN OF MILAN.
Imeandikwa na @jr_xavihernandez.
Kuna mtu mmoja aliyeitwa Mircea Lucescu alitabiri Andrea Pirlo atakuja kupata mafanikio makubwa sana kwenye soka ni muda ambao Pirlo hajafika miaka hata 19 lakini mtu yule alimtazama Pirlo kwa jicho la tatu.
Andrea Pirlo alikuwa zake akicheza pale Brescia akiwa na miaka 16. Baba yake alikuwa mmiliki wa viwanda vya kusindika chuma, Pirlo alipita njia yake akaamua kuchagua soka, Nini kilifuata?
Mwaka 2001 kocha Carlo Ancelotti anamtambulisha Andrea Pirlo kwenye timu ya Ac Milan, Waitaliano walimuona ni mwendawazimu unatuleteaje mchezaji ambaye hana hata nguvu tena kwenye eneo la ulinzi?
Waitaliano walizoea viungo wa shoka kwenye eneo la ulinzi viungo wababe wanaoweza kupambana kwa namna zote kucheza rough,tackling na roho mbaya kina Demetrio Albertini lakini Pirlo hakuwa hivyo.
Waitaliano walishindwa kubakiza maneno Ancelotti hakujali alimtumia Pirlo kama Deep-Lying Playmaker yani kiungo mkabaji anaehusika na ushambuliaji.
Ghafla waitaliano wakaanza kuimba wimbo mmoja wakaanza kumuita Professor wa mpira kila alipocheza majukwaa ya San Siro yaliwehuka na burudani alizokuwa anazitoa Andrea Pirlo.
Bado Wafaransa hawajasahau ile fainali ya kombe la Dunia 2006 kwa jinsi Pirlo alivyokuwa anawatawanya aliitoa timu kutoka kwa Gattuso akaipeleka kwa Luca Toni na Totti, Miguu ya Pirlo ilikuwa na rula,penseli,ufutio na bikari.
Alimeza dimba lenye mapafu wawili yani Vieira na Makelele, Waitaliano wakamuita tena The Brain of Milan, Achana na Pirlo kabisa, Joe Hart mpaka kesho anaiota ile Panenka kwenye Euro 2012.
Pirlo alikuwa mchawi wa Dimba, Waitaliano walikili hawakuwahi kuwa na kipaji kama yeye ndani ya miaka 25. Ni mwanadamu ambaye alipiga pasi za aina zote kwa usahihi sana(fupi,ndefu). Alitumia akili kuliko mabavu.
2011 Pirlo anamwambia Buffon kwamba nakuja Juventus, Buffon alisema maneno machache alisema Asante Mungu, Pirlo anakuja Juventus, San Siro hakukuwa na mtu fundi kama Pirlo.
Kwenye Ac Milan tishio pale ulaya ile Milan yenye Kaka,Gattuso na Seedorf, Juu inao Crespo na Shevchenko. Katikati yao alikuwepo Pirlo. Unaweza kumuita Proffesor au Brain of Milan.