[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Kupitia mtandao wa Instagram nilipata connection flani ya Jamaa yupo Atalanta, Georgia huko Marekani tukawa tunapiga stori mbili tatu kuhusu football akaniuliza kwanini Neymar Jr ndie mchezaji wako bora wa muda wote?
Alitaka kufahamu sababu, kwanza kabisa nikamkumbusha kwanza kuhusu De Toekomst, ndio hiyo shule maarufu ya soka inaitwa Ajax Youth Academy, iliyoanzishwa rasmi Machi 18, 1900 kisha nikamwambia dhumuni kubwa la academy hiyo na watu wa Ulaya.
Wenyewe wanakiits kiwanda ambacho Binadamu wanatengenezwa, baada ya ile kauli ya Mungu aliumba dunia kisha Mdachi aliitengeneza Uholanzi, hapa kuna elimu kidogo kuhusu Land Reclamation, tuiache kidogo.
Wazungu baada ya kuzunguka sana dunia kuanzia bahari ya Hindi mpaka Atlantic wakapata ripoti za kichunguzi kuhusu talents halisi zinazopatikana eneo hilo, walihitaji kuwahi mbele ya muda kuhakikisha mpira unachezwa na kuhusudiwa zaidi barani Ulaya lakini bado ilishindikana.
Baada ya tafiti mbalimbali za kisayansi wakaja na TIPS MODEL mfumo ambao binadamu mdogo anatengenezwa kuwa venye Ajax wanataka, wakiamini Uholanzi ni majaribio mazuri kisha isambae Ulaya nzima, hata uwanja wa ndege mkubwa Ulaya ni Schipol upo Amsterdam, kifupi Uholanzi ina maana kubwa sana.
Walishachungulia mbele ya muda na kuona kuwa baada ya Millitary Supremacy basi mpira utakuwa sababu moja wapo ya ukubwa wa mataifa duniani, walihofu Brazil na Afrika zitasogea kupunguza gap la umaskni kutokana na pesa za mpira.
Ilibidi isukwe plan ambapo hii ya academy na mifumo mikubwa ya kisayansi bado haikufua dafu mbele ya miguu ya Roger Milla, Jay Jay Okocha, Ronaldinho, De Lima, Maradona na mafundi wengine kutoka bahari ya Hindi na Pacific.
Bado maswali yakawa mengi kwenye maabara ya soka kuwa soka linahamiaje Ulaya? Afrika na Amerika Kusini watadondoka vipi? Hapo ndipo kilipo kisa changu na kwanini NEYMAR JR ndie Mchezaji wangu bora wa muda wote.
Leo usiku nikimaliza kuchat nae, nitarudi kuwasimulia hoja zangu na dunia iliyofichwa.