Makapuku Forum

Azam imetangaza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha wao mpya Denis Lavagne.

Lavagne ambaye amewasili jana amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' ambapo ataanza kazi yake kuanzia mchezo ujao wa ligi dhidi ya Mbeya City ugenini Septemba 13,2022.

Mkataba huo wa Lavagne amepewa malengo ya kutakiwa kuifikisha angalau hatua ya makundi timu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Miaka Miwili ya CEO.
.
Barbara Gonzalez aliteuliwa kuwa CEO wa klabu ya Simba Mnamo Tarehe 05.09.2020. Ni miaka miwili sasa akiwa ofisini na mengi hametokea Toka ujio wake. Naichambua miaka yake miwili kama kiongozi wa Mradi.
.
MAFANIKIO

🩸Kutoka mwaka 2020 klabu ya Simba imefanikiwa kuvuka mara mbili hatua ya makundi, hii ilionesha namna Baranara Gonzalez anataka Simba ifanye vizuri barani Afrika na kwa msimu ule amefanikiwa kushinda makombe yote ya Ndani.
.
🩸Timu ya Wanawake kuendelea kutawala Soka la Tanzania na Kuuza wachezaji nje, lakini pia kushiriki michuano ya Afrika na ubingwa wa CECAFA.
.
MABADILIKO

🩸Katika kipindi cha miaka miwili ya CEO mabadiliko mengi yamefanyika ya watu mbalimbali katika utumishi wa klabu kuondoka. Idara ya Habari Aliondoka "Bingwa la Kufeli", Ezekiel Kamwaga kisha Ahmed Ally na inavyoonesha safari bado inaendelea.
.
🩸CEO wakati anaingia alimkuta kocha Sven Vandenbroeck kisha Didier Gomes, Akafuta Pablo Franco Martinez, Thierry Hittimana, Zoran Maki na bado anafuata mwingine. Simuongelei Matola sababu yeye yupo tu.
.
BIASHARA.

🩸Simba wamefanikiwa kufanya biashara nzuri ya Nembo yao, kwanza ni kupata Bilioni Moja kwa Msimu kutoka #VunjaBei na kisha kuitenganisha Simba Queens na timu ya wakubwa kibiashara.
.
🩸Katika kipindi cha miaka miwili wamesaini Dili za kutosha za wadhamini kwa timu ya wanaume na sasa wadhamini kwa timu ya wanawake. Wamefanikiwa kusaini mkataba Ghali zaidi katika hitoria ya soka Tanzania.
.
PONGEZI

🩸Nidhamu ya Taasisi Imeimarika kuanzia wachezaji hadi watumishi, Simba hakuna mtu mkubwa zaidi ya Klabu. Kwa hilo nampongeza sana haswa kuondoka kwa "BINGWA LA KUFELI"
.
MAPUNGUFU

🩸CEO hana uvumilivu na haamini watu, kwa Taasisi hii ni hatari kwani watumishi wanakua wakiishi KICHINA CHINA na CEO.
.
🩸CEO hajaweka mkazo hivyo Simba inahangaika kusajili kuliko kuweleza kwa vijana watakaofia klabu kama kina Mkude.
.
🩸Anakwenda kuizamisha Simba, mfumo wake wa kutaka MAFANIKIO ndani ya Usiku mmoja imeifanya Simba kukosa muendelezo katika siku za karibuni.
.
Che Guevara

.
NB:
Ukiitwa na CEO usibebe Mabegi makubwa.
 
Mwamuzi AHMED ARAGIJA ameteuliwa na CAF Kuchezesha mechi ya CAF Champions League huko nchini Djibouti
.

Aragija atasaidiwa na FRANK KOMBA kama msaidizi namba 1 na MOHAMED MKONO msaidizi namba 2 huku SIYAH SALUM akiwa mezani.

Kila la kheir waamuzi wetu kwenye majukumu yenu ya kimataifa, nendeni mkapambanie nchi.
 
Huku simba ...kule chelsea mbona huu mwaka changamoto...

Sema uzurii babe wangu ananipenda sana
 
Ndio ndioooo
 
Simba kama inataka kumshinda
 
Kweli Mungu ni zaidi ya fundi.

Mtu unafikiria kumkomoa DEJAN wa watu kumbe ndio unamsaidia ili kuepuka lawama za Wa-CUBA.

DEJAN ana Mungu sana kwakweli maana angebebeshwa lawama zote yeye maskini ya Mungu.
:
ila kweliiii mashabiki wa simba tumeshavurugwa na hii team
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…