Kipa wa Simba SC Aishi Manula @28_manula amesema ni kweli Watanzania wengi wanatamani aende kucheza soka nje ya Tanzania lakini changamoto ni kwamba hajapata Club anazozitaka.
"Wengi hawafahamu, wengi wanakwambia tu wanatamani kuona umeenda nje lakini bila kujali umeenda nje ya wapi, sisi Makipa tuna mipaka, zile Nchi za Kiarabu hasa wale Waarabu weupe hawawezi kuchukua Kipa kutoka nje ya Nchi kwahiyo ili utoke Tanzania kuna Nchi kadhaa tu ambazo umewekewa Congo, South Africa, Angola na kwengine ambayo leo hii Ligi yetu ya Tanzania ni kubwa, wote wanatamani kucheza Tanzania"
"Muda mwingine napata ofa, napata Timu wakati mwingine napata timu ambayo ni kubwa, ya average ambayo haishiriki michuano ya kimataifa lakini mimi lengo langu ni kushiriki michuano ya kimataifa ili nipate platfoarm zaidi.... muda mwingine natamani kwenda nje lakini kulingana na nikiangalia nataka kucheza Champions league, Confederation cup kwahiyo kuna mambo mengi ambayo yananikabili ambayo Watanzania hawayaangalii wao wananitaka tu niende nje" ——— amesema Aishi Manula.