Makapuku Forum

Sawa mkuu
 
...ni kweli binamu ila jua lilipozamia ndipo litakapoibukia, dunia inajizungusha kwenye muhimili wake. Hali nimekubaliana nayo ila mazingira yananiambia nikomae tu, nisubiri kipindi cha pili naweza kusaidiwa na upepo
Hahaha chochote kinaweza tokea dakika za lala salama binamu,unaweza pindua meza
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limemkamata Abulaziz Abdallah maarufu Hunter mwenye umri wa miaka 19, Mkazi wa Chanika Tungini, akiwa na wenzake tisa wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21 wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya kujeruhi Watu kwa mapanga, kuvunja nyumba usiku na kuiba katika maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo Chanika.

"Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni kali dhidi ya vikundi mbalimbali vya kihalifu katika jijji la Dar es salaam na watakaokamatwa watafikishwa katika vyombo vya sheria"
 
Rais Samia ametangaza siku mbili za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki.

Maombolezo yataanza April 29,2022 hadi April 30,2022, katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye Balozi pia.

Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na Wakenya katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Kibaki.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imemuhukumu Fadhili Ngoho (25) mkazi wa Ulembwe, Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa miaka 8.

Fadhili amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka Mtoto wa miaka 8 ambaye ni Mtoto wake wa kambo aliyekuwa akisoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo katika kata ya Ulembwe

Inaelezwa kuwa siku hiyo Mshtakiwa alimbaka Mtoto huyo na kumwambia asipige kelele "Tarehe 23/2/2020 Mama wa Mtoto huyo alimuona Mwanae hatembei vizuri ndipo alipomuuliza ana tatizo gani na kisha Binti huyo akamwambia Mama yake kuwa Baba yake wa kambo alimbaka.
 
Vyombo vya Habari nchini Afrika Kusini vimeripoti kuwa Mzungu mmoja nchini Afrika Kusini aitwaye Paul Hendrik van Zyl (77), amefikishwa Mahakamani kwa kumpiga risasi na kumjeruhi Mwanamke mweusi anayedai kuwa alimdhania ni kiboko.

Mzungu huyo alikamatwa siku ya Jumanne baada ya kupiga risasi kuelekea kwa Mwanamke huyo, Ramokone Linah, ambaye alikuwa akivua samaki na mpenzi wake mtoni katika mji wa Lephalale, kaskazini mwa jimbo la Limpopo, Van Zyl anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua, kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka lakini yeye anajitetea kwamba alikuwa akiwapiga risasi wanyama.

Linah (38) alipata majeraha ya risasi kwenye mkono wake, wakati mpenzi wake aliyekuwa nae pamoja alifanikiwa kujificha kabla ya kutoa taarifa kwa polisi na huduma za dharura.

Mshtakiwa ndiye mmiliki wa shamba ambalo tukio hilo lilitokea na Polisi wamesema walipata bunduki kadhaa wakati wa kumkamata mshukiwa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…