Makapuku Forum

NYOTA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Abeid Mziba ‘Tekero’ amekiangalia kikosi cha sasa cha Yanga kinachoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na kuwaambia mabosi wa klabu hiyo, “ongezeni watu wa maana ili mmalize kazi.”
Mziba aliliambia Mwanaspoti kuwa, mabosi wa Yanga wanatakiwa kuongeza mabeki wawili wa kazi ili kusaidiana na waliopo kujiweka mguu sawa kwa ajili ya mechi za kimataifa msimu ujao.

Pia alisema mbali na kuongeza mabeki wawili, lakini mabosi wa Yanga wanatakiwa kusajili watu wa maana katika maeneo mengine ili kuwasaidia mastaa waliopo sasa kikosini hasa eneo la ushambuliaji ili kufanya vyema kwenye mechi hizo za kimataifa kwa msimu ujao.

“Yanga ya sasa inahitaji beki wa kushoto mwenye uwezo wa kukaba, beki wa kati wa kusaidiana na Dickson Job na Bakari Mwamnyeto sio kwamba waliopo ni wabaya, ila ni lazima kuwe na mbadala kwani anaweza mmoja wao au wote kuumia,” alisema.
 
Arudi nyumbani sasa khaaah!! Waziri ana kazi gani sasa[emoji2297]
 
LICHA ya Simba kuwa na mastaa kibao wenye uwezo mkubwa, lakini jina la beki Shomary Kapombe limekuwa gumzo Afrika Kusini wakati timu hiyo ikijiandaa kucheza Orlando Pirates katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Utamu zaidi ni kwamba mashabiki wa Kaizer Chiefs wamewahakikishia Watanzania watakuwa nao bega kwa bega katika mechi hiyo itakayopigwa Jumapili, mjini Soweto na kama Simba itapata sare tu, itatinga nusu fainali. Mwanaspoti lilizungumza na baadhi ya Watanzania wanaoishi Afrika Kusini, akiwamo shabiki wa Simba, Abdallah Mabange waliosema kwa sasa nchini humo Kapombe amekuwa akitajwa zaidi.

Mabange alisema katika mchezo uliopita kuna video ya beki huyo ilisambaa mitandaoni kwao ikionyesha kocha wa Orlando Mandla Ncikazi alivyokuwa akimshangaa kutokana na kazi nzuri aliyoifanya uwanjani.
 
Safi sana.
 
Bingwa mara 23 wa Grand Slam na bingwa mara saba wa dunia wa Formula One Lewis Hamilton wameungana na mwenyekiti wa zamani wa Liverpool FC Sir Martin Broughton kuinunua klabu ya Chelsea.
Vyanzo vya karibu na Serena na Lewis vinasema kuwa kila mmoja atatoa kiasi cha pauni 10millioni kununua shea kutoka kwa Broughton amabaye ataweka kiasi cha Euro 2.5billioni kuinunua timu hiyo kutoka kwa Roman Abramovic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…