KERRY AWAPA MBINU SIMBA
.
Kocha wa Moroka Swallows, Dylan Kerr ambaye aliwahi kuifundisha Simba, amewapa madini Wekundu wa Msimbazi mbinu za kuwamaliza Orlando Pirates katika mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Jumapili hii.
.
Kerry akiwa na Swallows katika mechi TANO zilizopita dhidi ya Orlando ameshinda moja, sare tatu na kapoteza mechi moja.
.
“Nakumbuka mara mwisho kucheza dhidi ya Orlando nilitumia mfumo wa 4-3-3, tulitengeneza vizuizi vitatu kila pembe, haikuwa rahisi kufika eneo letu, tulifunga njia, kila mpira ambao tulikuwa tukiupata tulihakikisha unakuwa na madhara kwao,” alisema na kuongeza.
.
“Haikuwa rahisi kupata pointi dhidi yao lakini kasi ilitubeba. Mkishambulia kwa kasi mnawavuruga,” alisema.