Makapuku Forum

UNAAMBIWA
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 Tanzania, Mke pia anao wajibu wa kumuuudumia Mume wake ikiwa Mume huyo atakuwa anapitia changamoto za kiuchumi kwa sababu za kiafya/akili ikiwa anacho kipato cha kuwezesha kufanya hivyo na sio kumkimbia/kumtelekeza.
 
Balozi wa Mazingira anayewakilisha Bunge, Joseph Kasheku (Musukuma) leo Jumanne Aprili 5, 2022 amejiuzulu nafasi hiyo akisema ni aibu kuwa mwakilishi wakati aliyemteua ameunda ripoti ya hovyo.

Musukuma mbunge wa Geita Vijijini amefikia hatua hiyo muda mfupi baada ya tume iliyoundwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Seleman Jafo kuwasilisha kwa wabunge ripoti ya uchunguzi wa chanzo cha kuchafuka kwa maji ya Mto Mara
 
Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijamii wa U turn Collection, Allen Mhina (31) na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka matatu yakiwemo ya kuchapisha maudhui yanayokiuka haki na uhuru wa mtu mwingine na kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying).

Mbali na Mhina, ambaye ni mkazi wa Temeke, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 57/2022 ni Mtandao wa U turn Collection na Mange Kimambi App.

Mhina na wenzake wamesomewa mashtaka yao, Ijumaa ya wiki iliyopita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mchinga Salma Kikwete aliyehoji ni lini Serikali itajenga vituo vya polisi katika

Kata mbili zilizopo jimboni kwake
‘’ Mahitaji ya vituo vya polisi kwakweli ni makubwa kwa mfano vituo vya daraja B, vilivyo ni 93 wakati mahitaji ni 563 mataona tofauti ilivyopana kwa hiyo changmoto hii ipo kwenye maeneo mengi kama Serikali tunaitambua changamoto hiyo na niombe tupewe muda ili tuweze kutatua changamoto hii kwa mapana yake''

 
Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi leo Aprili 5, 2022 amemteua Dk Zuhura Mohamed Abdallah kuwa Kamishna wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini katika Tume ya Mipango Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo Dk Zuhura alikuwa Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU)
 
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei awahimiza bodaboda mkoani humo kufanya malipo ya tozo za ushuru wa maegesho ili kuwa chachu ya maendeleo kwa taifa.

Mkoa wa Mbeya wameanza kulipa ada za maegesho ya magari katika barabara zinazomilikiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kwa njia ya mtandao badala ya fedha taslimu Aprili mosi 2022.

RPC Matei amewahamasisha bodaboda kuwa chachu ya maendeleo kwa kulipa ushuru wa maegesho kwa njia ya mtandao ili kuiwezesha Serikali kupata mapato.
 
“Tulichagua kuingia mfumo huu wa vyama vingi tukijua kwamba ndani ya mfumo huu tutakwenda kupata maendelo ya haraka kwa sababu vyama viko vingi, macho yako mengi, maono yapo mengi wanavyoona chama kimoja ambacho kipo ndani ya serikali pengine hawatokuwa na macho makubwa ya kuona kama wengine walio nje ya Serikali, na ndio maana tukasema vyama vingi hivi kazi yake ni kuangalia yanayoendelea ndani ya Serikali na kutoa maoni yao, jamani hivi tunakwenda hivi, lakini mbona mmh, mbona tunaona hivi, mbona sheria hii ingebadilishwa hivi, mbona sera hii tungekaa tukazungumza hivi.

“Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania. Tukikubaliana, tunakwenda kutekeleza wote kama Watanzania” Rais Samia Suluhu Hassan
 
“Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania. Tukikubaliana, tunakwenda kutekeleza wote kama Watanzania. Atakayekiuka hapo ni mkosaji, awe ametoka kokote kule kwa sababu tulijadiliana na kukubaliana tunaiweka hivi na hiyo ndio itakayokwenda kutuongoza katika utendaji wetu na maisha yetu kwanza ushirikishwaji kutoka serikalini ni uhakika “ Rais Samia Suluhu Hassan
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Tulia Akson amemwapisha Mbunge wa kuteuliwa, Shamsi Vuai Nahodha kushika wadhifa huo leo Aprili 5 jijini Dodoma.

Nahodha ameapishwa kuwa mbunge kufuatia uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan aliofanya hivi karibuni baada ya aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Mbunge huyo alipomaliza kiapo chake, kama ilivyo kwa taratibu za kibunge, aliwasalimia baadhi ya wabunge na Waziri Mkuu kisha akaongozwa moja kwenye kiti ambacho kilikuwa kikitumiwa na Polepole.
 
Ameupiga mbovu[emoji16]
 
Sina picha mpya we dadaaa [emoji1787][emoji23][emoji23] halafu kupost picha inaendana na mood niliyokuwa nayo hiyo siku ebu niacheee auntie Makiwendo unamuelewa Anne kweli. [emoji1787]
Mwee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Rudia hata zile za kabati jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…