Picha iliyopendwa zaidi.
Mpiga picha kabla hajafariki ngurumo za radi zilitawala,upepo mkali ulivuma,giza likaifunika dunia ya soka na ile picha ya Simba iliyowekwa ukutani ikaanguka juu ya mikono yake. Haya yalitokea kwasababu JAH alikuwa anaichukua roho ya binadamu aliyoipenda kazi yake.
Katika zile nyakati za mwisho mpiga picha akiwa kitandani,akiwa karibu na umauti ilibidi atoe machozi ya furaha kwasababu hana cha kumlipa JAH kwa kumpa kipaji cha kupiga picha na kumpa nafasi ya kuishika camera iliyobeba picha ya mnyama anayechukiwa zaidi jangwani.
Hisia za Mpiga picha huyu ni sawa na hisia za Wapiga picha wote waliokuwepo pale Mkapa Stadium kwasababu na wao walipata nafasi ya kumtukuza JAH,walipata nafasi ya camera zao walau kuipata picha ya mnyama aliyebeba tabasamu nzito la waumini wa pira biriani.
Basi zile ngurumo za radi,ule upepo mkali na lile giza na ile picha ya simba iliyoanguka kutoka ukutani viashiria hakika JAH hakukosea kutoa zawadi ya kipaji cha kushika camera.
@omarrkombo