POCHE KUTI KAVU PSG
.
Imethibitisha kwamba watu ambao wana asilimia 80 za kufukuzwa kwenye viunga vya PSG ni kocha Muargentina Mauricio Pochettino sambamba na mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo, Leonardo.
.
Inaelezwa kuwa lengo la Pochettino kusajiliwa kwenye kikosi hicho ilikuwa ni kwenda kuipa taji hilo la Ulaya ndio maana wakasajiliwa wachezaji wengi bora ili kumpa nguvu ya kufanikisha suala hilo, hivyo kushindwa kwake ni sababu itakayomfanya kuondolewa yeye na mkurugenzi wa michezo.
.
Baada ya mechi, Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, alionekana kuwa na hasira sana kwa mujibu wa mwandishi wa habari aliyekuwa karibu naye. Inadaiwa tajiri huyo alichukua hadi jukumu la kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia waamuzi kwa lengo la kuwalaumu kwamba hawakuitendea haki timu yake.
.
Huenda Pochettino akarudi England ila mara hii kuifundisha Man United.